Serikali yatimua wanafunzi UDSM

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Muda mfupi uliopita, waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, prof Jumanne Maghembe, amelitangazia Bunge kuwa serikali imefuta udahili wa wanafunzi takribani 300 wa Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Katika maelezo yake, Prof Maghembe alisema kuwa wanafunzi hao wametimuliwa baada ya kukaidi amri ya uongozi wa chuo iliyowataka warejee madarasani.
Miongoni mwa waliotimuliwa ni wale waliogoma kuanzia juzi (zaidi ya 250) na wengine 38 ambao jana walikamatwa na polisi katika vurugu na leo wamefikishwa mahakamani kisutu wakikabiliwa na kesi 3 rofauti.
 
Natumaini Maghembe ataelezea hizi habari zinazovuma hapa kuwa polisi wameua mama mjamzito mwanafunzi wa UD aliyekuwa anaendelea na maisha yake hapo shuleni!
 
It is about time that UDSM is being run as a private entity and no longer a government institution. Serikali imeshindwa kuendesha UDASA.
 
Sijui tutaendelea kufukuza wanafunzi lini? Aibu tupu! Tunaacha kuwafukuza kazi wanaotuibia, tunakimbilia kufukuza wanafunzi?

JK vipi rais wetu, migogoro inatatuliwa kwa mazungumzo na sio ubabe!
 
ni yale yale ya utawala wa Msolla! hivi kweli Tanzania hatuna watu wenye akili timamu ambao wanaweza kukaa chini na kutatua matatizo ya Mlimani? Tuombe wawekezaji waje kutuonesha jinsi ya kuendesha Chuo Kikuu cha Taifa...?
 
Lunyungu Mimi Nakutafuta Sana Kama Uko Maeneo Haya Ya Udsm

Sasa Hivi Najuka Utawala Tuonane Hapo Hill Park Kama Una Muda Numbre Yangu Ni 0713 620278


Sina muda mchafu wa kuonana na wewe lakini kwa faida yako .Nimevaa sharti makini la cardet , Jeas na timberland za nguvu .Naondoka Utawala naelekeo pale kituo cha Polisi .So kazi kwako na wambeya wenzio.

Wale wote waliodhani CCM ni msaada sasa wanajionea kwamba JK ana maonevu na wezi wote wanalindwa .Tunangoja kujua habari za kufa kwa mwanafunzi bado ni kimya kikuu hapa .
 
Is this measure not (too) excessive? Au ndivyo tulivyo...kutumia akili kidogo, mabavu mengi.

Wameingilia uchaguzi, wamefukuza viongozi, wamepiga mabomu wanafunzi bila sababu yoyote, kuna habari kuwa wameua mwanafunzi mjamzito, wamekamata wanafunzi usiku wa manane, hii ni hitimisho la udikiteta, ufisadi na "uuaji" wa Mkandara (ambaye ni mshauri wa Kikwete wa masuala ya siasa).
 
Mukandala amekanusha kufa kwa mwanafunzi yeyote, anasema alipatwa na mshituko mkutokana na mimba na yupo katika hospitali moja huko mikocheni anatibiwa
 
This is sad story, hawa UDASA wapoje na Waziri Prof. Mzima haoni kama kufukuza wanafunzi siyo suluhisho? Halafu wanasema walikamatwa wanafunzi 39, waliofikishwa leo mahakamani ni 38 tu, huyu mmoja yupo wapi? kama wameua kweli si waseme? Duu ufisadi hadi kwenye masuala ya jamii!!
 
Mukandala amekanusha kufa kwa mwanafunzi yeyote, anasema alipatwa na mshituko mkutokana na mimba na yupo katika hospitali moja huko mikocheni anatibiwa

Hata kama mimba imetoka bado ni uuaji huo. Damu iko mikononi mwa Mkandara na asileta maneno ya wanasiasa hapa kuwa amesikitishwa na vitendo vya FFU ambao yeye ndiye chanzo cha kuwaleta hapo chuoni in the first place.

Mkandara kuanzia sasa atapewa jina la muuaji hapa JF!
 
This is sad story, hawa UDASA wapoje na Waziri Prof. Mzima haoni kama kufukuza wanafunzi siyo suluhisho? Halafu wanasema walikamatwa wanafunzi 39, waliofikishwa leo mahakamani ni 38 tu, huyu mmoja yupo wapi? kama wameua kweli si waseme? Duu ufisadi hadi kwenye masuala ya jamii!!

Nziku,

Yaani wanajichanganya kweli kwenye suala la wanafunzi waliokamatwa na hiyo ya kifo cha mama mja mzito. Kuna taarifa kuwa wanafunzi wawili wa sayansi ya jamii hawajulikani walipo.

Inawezekana wameua zaidi ya mtu mmoja hapa!
 
Ila inashangaza ee

wanatafuta haki wanauliwa,wanafukuzwa wanatiwa marungu na wanatiwa polisi.Tena mwanafunzi tuu

Wezi wanaohatarisha maisha yetu,wanaoua kwa kutuibia mabilioni ya sh wanapeta tu
Chenge,Msabaha,karamangi,mkapa balali,azizi hawatiwa hata kiboko
duuuuuu
 
Sasa Prof Maghembe anataka kuingia katika Kundi la Mafisadi, maana kuwanyima watu haki yao ya Msingi tena wanafunzi tunao wategemea waje kuchukua au kuongoza taifa in future ni kitu cha kusikitisha na kisicho ingia akili kwa mtu mwenye akili kama wewe, labda ukiwa umepata Denge lua. Please acha kusikiliza taarifa Potofu za Prof Mkandara.
Plse Maghembe Raise up to you Status Mzee.
Kwa Mfano wanafunzi hawapatiwi maji kisa Pump mbovu kumbe ni creation ya mradi wa watu ili wa-supply maji. Ni jambo zuri, mbona shida zingine tunajitakia? au ndio njia za kuongeza ajira na Mabilionea wa Ari mpya?
 
Tena kuna habari nyingine kuwa wanafunzi 38 waliokamatwa jana wamefikishwa mahakama ya kisutu, wanakabiliwa na kesi 3 tofauti. wengine wamepata dhamana, wengine wamepelekwa mahabusu
 
Jamani hizi habari za kifo kama kweli zinatisha sana tena sana...can someone confirm..

Halafu wakati wa matatizo ya nchi huyu kisura wetu hutukomea...jana alionekana akikwaa KLM baada ya kumsindikiza waziri mkuu norway..... sijui kama ni kweli
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom