Serikali yatangaza rasmi Mikoa mipya 4 na wilaya 19

Wazo zuri lakini kwa nini hawakuufanya mji wa Nzega kuwa Mkoa badala yake wakaifanya Katavi yenye wilaya mbili tu? Maana wangeweza kupata wilaya Tano kwa kuweka Mkoa wa Nzega...ambao ungekuwa na Wilaya za Nzega yenyewe, Bukene, Puge/Ndala, Igunga

Dakitari,

Mji hauwezi kuwa mkoa au ulimaanisha wilaya?
 
Dah,hii serikali naona haina mpango mkakati endelevu kabisa.Mpango mzima wa kupeana ulaji!
 
Wazo zuri lakini kwa nini hawakuufanya mji wa Nzega kuwa Mkoa badala yake wakaifanya Katavi yenye wilaya mbili tu? Maana wangeweza kupata wilaya Tano kwa kuweka Mkoa wa Nzega...ambao ungekuwa na Wilaya za Nzega yenyewe, Bukene, Puge/Ndala, Igunga

Hii ingekuwa sahihi zaidi,maana mkoa wa Tabora bado ni mkubwa sana,nafikiri wa 1 au 2 TZ na eneo la sqkm za kumwaga..Haiingii akilini mkoa kama Katavi kuwa na wilaya mbili tu.Kweli kusogeza huduma karibu na Waziri Mkuu.
 
Tuache umbumbu jamani. Mbona mnakuwa kama watoto kwa michango yenu ya ajabuajabu. Kama huna hoja kaa kimya sio kila kitu uchangie

kweli ww ni kaka Mwisho! Utoto uliouona katika michango ni upi? Nafikiri ww ndo mtoto na inawezekana wa kigogo hapo unachekelea ukitaraji kupewa fadhila! Haya yote yana mwisho. Mkoa kama Mlele (Wilaya 2) lazima wamechakachua vigezo! wenyewe ni mkubwa, tatizo ni population na huduma za jamii. Mi naufahamu sana labda kama kigezo ni kwa PM! Mkoa umejaa mistu na mbuga ya Katavi, human settlement ina cover eneo dogo sana. Hii yote ni mwono hasi-WATANIKUMBUKA KWA HILI kwani hawana vingine vya maana ambavyo wananchi watawakumbuka kwavyo!
 
Hawa JK na Mtoto wa Mkulima wasituchanganye sie! Ma mikoa yote hayo ya nini jamani? Kwa pesa gani tulizonazo kuongeza gharama za uendeshaji serikali kwa kiwango hicho? Hivi hawa watu mbona wanataka kutuachia taabu baada ya wao kutoka madarakani? Inakuwaje wanaanzisha wilaya na mikoa kila kukicha kama shule za kata? Wanaharibu hata historia na mikoa yetu ya awali! Leo jukwaa limeni bore ile mbaya!
 
Wazo zuri lakini kwa nini hawakuufanya mji wa Nzega kuwa Mkoa badala yake wakaifanya Katavi yenye wilaya mbili tu? Maana wangeweza kupata wilaya Tano kwa kuweka Mkoa wa Nzega...ambao ungekuwa na Wilaya za Nzega yenyewe, Bukene, Puge/Ndala, Igunga

Bila shaka hapa ni kuwapa shavu watu fulani fulani tu kama wengi wanavyoongea humu. Hii inazidi kuthibitisha jinsi ambavyo CCM wanaimba uchumi wa soko wakati wanachofanya ni mambo kama ya kikomunisti/soshalisti. Wanaongeza na kutanua mashavu ya utawala bila kuzingatia kuwa katika mfumo wa soko tunaoujenga uchumi unajengwa na sekta binafsi. Serikali inatakiwa iwe ndogo kabisa ili kupunguza mzigo wa kodi kwa sekta binafsi.

Ili kufidia kuongezeka kwa matumizi ya serikali tutarajie bajeti ya mwaka huu kuja na ongezeko la kodi huku na kule. Utawala mkubwa huhitaji gharama kubwa kuuweka na gharama haitatoka pengine isipokuwa kwa walipa kodi.

Hizi ajira za ukuu wa mikoa/wilaya, kata, n.k. si ajira halisi bali ni mzigo kwa walipa kodi tu. Badala ya kuongeza hizo wilaya hizo fedha wangezitumia kwa kujenga bara bara. Mfano, mkoa wa Kigoma ambao hauna bara bara ya kuaminika umeongezewa wilaya tatu zaidi (Kakonko, Buhigwe, Uvinza). Fedha za kujenga makao makuu ya wilaya tatu na kuendesha utawala zingesaidia kuboresha miundo mbinu huko na kuacha utwala kama ulivyo.

Tunahitaji mabadiriko na tunayahitaji leo!!
 
Wazo zuri lakini kwa nini hawakuufanya mji wa Nzega kuwa Mkoa badala yake wakaifanya Katavi yenye wilaya mbili tu? Maana wangeweza kupata wilaya Tano kwa kuweka Mkoa wa Nzega...ambao ungekuwa na Wilaya za Nzega yenyewe, Bukene, Puge/Ndala, Igunga
Kwanza napenda kuipongeza serikali kwa usikivu wake kwa kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Wilaya/Mikoa hii mipya iliyotangazwa rasmi. Niwapongeze pia wananchi wa Wilaya/Mikoa husika kwa kufanikiniwa kusikilizwa kilio/maombi yao ya kutaka kupata maeneo mapya ya utawala kwa lengo la kuwasogezea huduma muhimu walizokuwa wanapata tabu sana kuzipata kutokana na ukubwa wa maeneo ya utawala ya hapo awali.

Naamini hatua hii ni muhimu sana katika kuharikisha maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Na hapa napenda wadau waelewe wazi kuwa uanzishwaji wa maeneo haya mapya ya kiutawala chanzo chake ni kwa wananchi wenyewe wa maeneo husika na wala sio serikalini. Serikali ilichofanya nikuyapokea maombi ya wananchi hao,kuyapima kwa uzito wake na kisha kukubaliana au kuyakataa.Na hapa utaona kwamba ni wananchi wa wilaya 21 walioomba wilaya mpya. Lakini baada ya kuyapitia,serikali imeona ni wananchi wa wilaya 19 ambao kwa sasa wanastahili kukubaliwa maombi yao. Kwa hiyo kama ni wa kulaumiwa ni wananchi wa maeneo hayo kwa kuomba maeneo hayo ya kiutawala na wala sio serikali. Serikali wajibu wake ni kuwahudumia wananchi wake kwa mujibu sheria na taratibu za nchi. Kimsingi,Suala la gharama za uendeshaji hilikwepeki kwa kuzingatia kwamba wananchi wa maeneo husika nao ni watanzania na wana haki ya kufaidi kodi zao na rasilimali za nchi yao.

Sasa nikija kwako mh. Ulichosema ni sahihi kabisa kutokana na hali halisi ya huko Mkoani kwako. Sasa ninachoomba utusaidie ni endapo wananchi wa huko Nzega nao walishatoa maombi yao ya kupata Mkoa wa Mpya Nzega kwa utaratibu rasmi ? Na je,unalijua vema eneo zima la Mkoa wa Katavi? Kwa kuwa moja ya vigezo vya uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala ni pamoja na ukubwa eneo husika. Inawezekana kwamba Katavi pamoja na kuwa na Wilaya Mbili lakini eneo lake na idadi ya wakazi wake ikawa kubwa.
 
kuongeza mikoa na wilaya ni bure kama hatujui tatizo nini linalosababisha nchi isiendelee
 
kwanza napenda kuipongeza serikali kwa usikivu wake kwa kilio cha muda mrefu cha wananchi wa wilaya/mikoa hii mipya iliyotangazwa rasmi. Niwapongeze pia wananchi wa wilaya/mikoa husika kwa kufanikiniwa kusikilizwa kilio/maombi yao ya kutaka kupata maeneo mapya ya utawala kwa lengo la kuwasogezea huduma muhimu walizokuwa wanapata tabu sana kuzipata kutokana na ukubwa wa maeneo ya utawala ya hapo awali.

Naamini hatua hii ni muhimu sana katika kuharikisha maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Na hapa napenda wadau waelewe wazi kuwa uanzishwaji wa maeneo haya mapya ya kiutawala chanzo chake ni kwa wananchi wenyewe wa maeneo husika na wala sio serikalini. Serikali ilichofanya nikuyapokea maombi ya wananchi hao,kuyapima kwa uzito wake na kisha kukubaliana au kuyakataa.na hapa utaona kwamba ni wananchi wa wilaya 21 walioomba wilaya mpya. Lakini baada ya kuyapitia,serikali imeona ni wananchi wa wilaya 19 ambao kwa sasa wanastahili kukubaliwa maombi yao. Kwa hiyo kama ni wa kulaumiwa ni wananchi wa maeneo hayo kwa kuomba maeneo hayo ya kiutawala na wala sio serikali. Serikali wajibu wake ni kuwahudumia wananchi wake kwa mujibu sheria na taratibu za nchi. Kimsingi,suala la gharama za uendeshaji hilikwepeki kwa kuzingatia kwamba wananchi wa maeneo husika nao ni watanzania na wana haki ya kufaidi kodi zao na rasilimali za nchi yao.

Sasa nikija kwako mh. Ulichosema ni sahihi kabisa kutokana na hali halisi ya huko mkoani kwako. Sasa ninachoomba utusaidie ni endapo wananchi wa huko nzega nao walishatoa maombi yao ya kupata mkoa wa mpya nzega kwa utaratibu rasmi ? Na je,unalijua vema eneo zima la mkoa wa katavi? Kwa kuwa moja ya vigezo vya uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala ni pamoja na ukubwa eneo husika. Inawezekana kwamba katavi pamoja na kuwa na wilaya mbili lakini eneo lake na idadi ya wakazi wake ikawa kubwa.
kama mjumbe wa shina vile.
 
Kwanza napenda kuipongeza serikali kwa usikivu wake kwa kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Wilaya/Mikoa hii mipya iliyotangazwa rasmi. Niwapongeze pia wananchi wa Wilaya/Mikoa husika kwa kufanikiniwa kusikilizwa kilio/maombi yao ya kutaka kupata maeneo mapya ya utawala kwa lengo la kuwasogezea huduma muhimu walizokuwa wanapata tabu sana kuzipata kutokana na ukubwa wa maeneo ya utawala ya hapo awali.

Naamini hatua hii ni muhimu sana katika kuharikisha maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Na hapa napenda wadau waelewe wazi kuwa uanzishwaji wa maeneo haya mapya ya kiutawala chanzo chake ni kwa wananchi wenyewe wa maeneo husika na wala sio serikalini. Serikali ilichofanya nikuyapokea maombi ya wananchi hao,kuyapima kwa uzito wake na kisha kukubaliana au kuyakataa.Na hapa utaona kwamba ni wananchi wa wilaya 21 walioomba wilaya mpya. Lakini baada ya kuyapitia,serikali imeona ni wananchi wa wilaya 19 ambao kwa sasa wanastahili kukubaliwa maombi yao. Kwa hiyo kama ni wa kulaumiwa ni wananchi wa maeneo hayo kwa kuomba maeneo hayo ya kiutawala na wala sio serikali. Serikali wajibu wake ni kuwahudumia wananchi wake kwa mujibu sheria na taratibu za nchi. Kimsingi,Suala la gharama za uendeshaji hilikwepeki kwa kuzingatia kwamba wananchi wa maeneo husika nao ni watanzania na wana haki ya kufaidi kodi zao na rasilimali za nchi yao.

Sasa nikija kwako mh. Ulichosema ni sahihi kabisa kutokana na hali halisi ya huko Mkoani kwako. Sasa ninachoomba utusaidie ni endapo wananchi wa huko Nzega nao walishatoa maombi yao ya kupata Mkoa wa Mpya Nzega kwa utaratibu rasmi ? Na je,unalijua vema eneo zima la Mkoa wa Katavi? Kwa kuwa moja ya vigezo vya uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala ni pamoja na ukubwa eneo husika. Inawezekana kwamba Katavi pamoja na kuwa na Wilaya Mbili lakini eneo lake na idadi ya wakazi wake ikawa kubwa.

Tukisema kila anayetaka kusogezewa huduma afanyiwe hivyo kwa kuanzishiwa wilaya au mkoa sijui tutafika wapi? Unashindwa kufahamu kuwa tatizo sio uwepo wa wilaya na mikoa ili wananchi wapate huduma kwa haraka ila tatizo ni miundombinu! Wanasiasa wakiendekeza kusogeza huduma kwa kuanzisha wilaya na mikoa itafika wakati kila kijiji kitakuwa wilaya! Serikali inatakiwa kuboresha miundombinu na kusogeza huduma husika kwa wananchi na sio kuongeza idadi ya watendaji wa serikali kuu na serikali za mitaa!
 
Tuache umbumbu jamani. Mbona mnakuwa kama watoto kwa michango yenu ya ajabuajabu. Kama huna hoja kaa kimya sio kila kitu uchangie WE NDO MBU3, HII NI SAWA NA KUUA WATZ!KUNA LOGIC GAN YA KUHADHISHA MIJI!ECONOMICALY NI UPUMBAV HUO
 
Jamani mbona haya maajabu mi katika maisha yangu sijawai kusikia mkoa wenye wilaya mbili

na kweli itakua kulipa fadhila kwa mtoto wa peasant kwani katiba yetu imempa mamlaka ya kupindukia na hata kuweza kufanya mambo yasiyo na tija kama hili.

Tafakari ... Chukua hatua!!!!
 
Hiyo wilaya ya Chemba iko Mkoa gani? Siioni popote katika hiyo mikoa, otherwise mniambie tangazo limekosewa. Na, iwapo Katavi ina wilaya mbili, kama tangazo linavyodai, hiyo Kalambo yenye makao yake pale Matai, iko mkoa gani? Please help
 
Yani tuna hasara na jk na uongozi wake wote!!
Yani cjui huyu jk anatafakari nini kwenye kichwa lake!

Wewe tukana na kuandika maneno ya kudharau kiongozi wa nchi kwa namna upendavyo wewe ila siku moja utakuja kujua nini maana ya kusajili simu,si vizuri kumsema mtu kwa maneno machafu unaweza tumia lugha nzuri kuchangia hoja na ukaeleweka,kuwa makini!
 
Wazo zuri lakini kwa nini hawakuufanya mji wa Nzega kuwa Mkoa badala yake wakaifanya Katavi yenye wilaya mbili tu? Maana wangeweza kupata wilaya Tano kwa kuweka Mkoa wa Nzega...ambao ungekuwa na Wilaya za Nzega yenyewe, Bukene, Puge/Ndala, Igunga
Mkuu HK,nadhani wananchi wa maeneo haya yaliyogeuzwa mikoa na wilaya mpya wange julishwa gharama za kuanzisha mkoa mpya na gharama za serikali kuimarisha huduma za jamii,afya,elimu,maji safi na miundombinu,naamini wangechagua huduma za jamii. Bado serikali yetu inafanya maamuzi kwa kutumia njia za kijima! Ningetarajia serikali itumie technolojia ya kisasa kuanza kupunguza gharama zisizo za lazima.
 
Back
Top Bottom