Serikali yatangaza rasmi Mikoa mipya 4 na wilaya 19

Kwakuwa wilaya ya Mlele imeanzishwa ikimegwa toka wilaya ya Mpanda, na kwakuwa wilaya mbili za Mlele na Mpanda ndizo zinaunda mkoa mpya wa Katavi, na kwakuwa wilaya mpya ya Mlele ndio nyumbani kwa waziri mkuu Pinda, na kwahiyo basi wilaya ya Mpanda imegeuzwa kuwa mkoa wa Katavi.

Nitakuwa nimemtendea haki waziri mkuu nikimfahamisha kwamba kuanzishwa kwa mkoa wa Katavi hakuna tija yoyote kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa na Tanzania kwa jumla bali ni ufujaji wa mali ya umma, matumizi mabaya ya rasilimali, kiburi na ubinafsi wa viongozi kutaka kila kitu ama kila mradi apeleke kwao.

Kama mwl. Nyerere angekuwa mtu wa tamaa na ubinafsi kama hawa viongozi wetu wa sasa, basi mji wa musoma ndio ungekuwa makao makuu ya nchi hii! Viongozi wa sasa katika nchi hii ni wa hovyo sana katika kufanya maamuzi.
 
Nitafurahi nikisikia utitiri wa mikoa na wilaya utasababisha kushusha bei ya sukari
 
Baadhi ya Mikoa na Wilaya nyingi ni duni kwa maendeleo,lakini hali ya maisha. Umuhimu wa kuongeza mpya wakati zilizopo hazina chochote,hasa upande wa maendeleo. Mfano KASULU ambayo inaizaa BUHIGWE.KIBONDO inaizaa KAKONKO kwaukweli wilaya mama bado zina mahitaji makubwa sana. Sasa serikali lazima itawapa wananchi wakati mgumu sana.Wilaya nilizotaja lami hakuna,umeme ndiyo kwanza wa jenereta unadhani hizo mpya itakuwaje sasa.Ni mtazamo wangu,tu lakini kazi kweliii kweliiii JK,BILAL,PINDA N.K
 
Hivi ni vigezo gani wanatumia katika kuanzisha hii mikoa???? Karibu kila wilaya uliyobatizwa kuwa mkoa maisha ya wananchi yanasikitisha, halmashauri zake hazina pesa, miundo mbinu mibovu, hakuna hata hospitali bora, shuleni hakuna madawati, etc....sorry ni mlolongo mreeeeeeeeeeeefu wa mapungufu yaliyopo. Kwa nini serikali isiendeleze mikoa iliyopo kwanza kufikia kiwango cha miji ndipo wafikirie mengineyo..huku ni kuongezeana mizigo kwa mlipa kodi. Sasa kutatangazwa wakuu wa mikoa, wakurugenzi wapya, wakuu wa wilaya (ooops hili sina hakika nalo!!!) sasa hii si lawama jamani. Serikali ya hii nchi ni kilaza kwelikweli....Anyways bora maisha au maisha bora watever!!!!!
 
Jamani mbona haya maajabu mi katika maisha yangu sijawai kusikia mkoa wenye wilaya mbili

Na kweli, hizo wilaya mbili maana yake nini sasa?!!..baadae tena utasikia "serikali imetafakari kwa kina, na kuona kuwa kuna umuhimu wa kuzigawa wilaya hizo,hivyo kwa saa zitakuwa tano,badala ya mbili'?!
 
Duh kweli kiazi hakipikwi na gimbi hivi huyu jamaa ndio kusema anachanganyikiwa na mambo au niaje hii mikoa michache na wilaya zinalemea serekali kufikia mahali kuna watumishi wanafanyakazi kwa mkopo sasa yeye kwakuona hao marafiki na jamaa ambao mi naweza kuwaita vinasa kwakushindwa kuokoa jahazi la jamaalikiwa hatarini kuzama hawana shughuli ndio kaamua kutafuta mahali ya kuwapachika kweli jini likualo halikukuli likakwisha.
 
Safi sana, mie naona ndo ku disetrorilizi maendeleo zaidi ilivyo sasa sentrolaizidi wote tumejazana Dar, au mwanza nk. Serikali kwa kuhudumia mikoa hiyo migawo ya fwedha itakaribia hata huko. Kwangu mie ni vizuri zaidi.
 
Mimi naweza kuzungumzia mkoa mpya wa Manyara kiukweli hilieneo sikuona wala sitaridhika kupewa hadhi ya kuwa mkoa kwa sababu: kijografia hili eneo liko scarterd mbaya sana nikiwa na maana kwamba kutoka kijiji kimoja hadi kingine kuna km zakutosha sana ambazo zinamtosha mwananchi kufunga safari haswa kwenda kijiji cha jirani, kiuchumi eneo hili la mkoa halina shughuli za kijamii ambazo zinawezesha wilaya kupata mapato na linapata huduma nyingi kutoka mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, kijamii mkoa wa manyara bado hauna hospitali iliyo jitosheleza wala kituo kikubwa cha polisi matokeo yake wanategemea hospitali ya mkoa wa Arusha "mount Meru" na kituo cha polisi cha mkoa wa Arusha. Hayo ni baadhi ya mapungufu ambayo mimi nadhani hayajakidhi haja ya mkoa wa Manyara kuwa na hadhi ya kuwamkoa.....
 
Hizi pesa za kuhudumia hii Mikoa sijui zitatoka wapi? Kama za kuhudumia Mikoa iliyopo ni shida . Pesa za madakitari ni shida ! Za walimu ni shida ! Du Kweli ukiongozwa na boga lolote linawezekana

Mkuu angalia utakula BAN kumwita anayetuongoza ni boga! Ila mkuu nusura univunje mbavu! Kuna kichaa wangu jana kasema mtoto alizaliwa Tanzania hana kichwa akawekewa dafu la nazi sasa hivi ni anaongoza nchi! Jf ni mwisho!
 
Wazo zuri lakini kwa nini hawakuufanya mji wa Nzega kuwa Mkoa badala yake wakaifanya Katavi yenye wilaya mbili tu? Maana wangeweza kupata wilaya Tano kwa kuweka Mkoa wa Nzega...ambao ungekuwa na Wilaya za Nzega yenyewe, Bukene, Puge/Ndala, Igunga
 
Kwenye ukuu wa mikoa hiyo, tutarajia kuona majina kama, lawrence masha, monica mbega, hawa ng'humbi, getrude mongela, benson mpesya, n.k, malzia wengne.
 
Ndio uwandike kumbukumbu sasa usitarajii Kili kitu kitafanywa sawa na akili yako
 
Kama mikoa imeongezwa je na eneo lime panuliwa? Ama watu nao wameongezwa? Tumieni elimu kabla ya Kutowa maoni huduma itakuwa kama kawaida na itarahisisha mikoa hio katika mchakato wa maendeleo na miundo mbinu na ushindani wa maendeleo na nyie watanzania msizubi kila kitu serekali lazima muendeleze maeneo yenu
 
Back
Top Bottom