Serikali yatangaza rasmi Mikoa mipya 4 na wilaya 19

hii issue ni ya Pinda, siku zote anawaza mpaka Ikulu ihamie mpanda. what for? ongeza idadi ya watendaji hizo wilaya mpya ndo ziwe duty stations. ma DC n other politicians ni mzigo.
 
Hivi kuna utafiti wowote uliokwisha fanywa kuassess maendeleo ya hii mokoa mipya iliyoanzishwa recently?? maana nahisi kama ni mzigo zaidi kwa serikali na hivi kila kukicha twaambiwa hakuna pesa!!
 
wapuuzi sana hao, walifikiri watavuta tention zetu kwenye kugawa wilaya na mikoa, tuna matatizo mengi hatutaki takwimu za idadi ya wilaya au mikoa, tunataka maendeleo.

Kweli bwana hawa watu wanatuchanganya tuu!
 
Inawezekana kwamba serikali ilikuwa na nia nzuri ya kuongeza mikoa na wilaya zake. Lakini kwa sasa inaweza kuhairisha kutokana na hali ya fedha. Serikali ina majukumu mengi yaliyo ya dharula na mengine muhimu. Si vizuri kufanya yote katika hali hii.
 
hongera serikali kwa kutukumbuka kanda ya ziwa. Kilichobaki ni kuona utekelezaji wa ujenzi wa makao makuu mapya ya wilaya na mkoa (bariadi na geita)ikiambatana na miundombinu inayokidhi kigezo cha mkoa/wilaya
 
Huo mkoa wa katavi ni hasara...kuna haja gani ya kuanzisha mkoa mpya Wenye wilaya mbili...Kama si ubaguzi na umimi....haitofautiani na uamuzi wa Msuya kuifanyaa Tatars ndogo ya Mwanga enzi zake kuwa Wilaya.....na juhudi zake za kuifanya, same ,Mwanga ...ziwe mkoa zijitenge toka Kilimanjaro.......ubinafsi tu unatuumbua...Kama kujijenga Kiwanja cha ndege Katavi wakati uwanja wa ndege mbeya haujakamilika...
 
Tukianza majadiliano ya vipengele vya katiba mpya, haya ni mambo ambayo tunatakiwa tuwe nayo makini kabisa. Hatuwezi kuendelea na hali hii ambapo maamuzi ya watu wachache yanalibebesha taifa gharama kubwa kiasi hichi. Je, Bunge lilihusishwa kwenye uamuzi huu wa kuundwa mikoa na wilaya mpya? Je, hivi ndivyo vipaumbele vya taifa kwa wakati huu?
 
Shangazi , mjomba , rafiki watapata ajira

This is nothing but expansion of Goverment which has nothing do with development. It is pure political move towards CCM power grab security.

Hakuna haja ya kukatakata nchi katika vipande vipande vya kiutawala bali ni kuinganisha na miundombinu itakayoweza kufanya sehemu kubwa kuwa reachable. Hawa wanasiasa wapya 23(4 wakuu wa mkoa na 19 wa wilaya) hawana lolote la maana zaidi ya kuongezea mzigo wa matumizi serikali wakati hivi sasa ikiwa hoi bin taaban kuwalipa kwa wakati hao waliopo.

Tokea nimekuwa na akili zangu sikupata sikia katika utawala wa Nyerere nau Mwinyi kasi kubwa ya kukatakata nchi kumegwamegwa na kuanzisha bogus regions kama ambavyo nimeshuhudia katika kipindi cha Mkapa na JK. Nafikiri suala la mikoa liwekwe wazi katika katiba maana tunapoelekea utakuja sikia nchi ina mikoa 300 ili tu kutengeneza nafasi za ulaji za watakaokuwa madarakani. Re-districting ni muhimu sana kama inafanywa kwa malengo ya kuboresha huduma.

Tunaweza kuwa na Mikoa 20 tu Tanzania bara ila tuakwa na district nyingi kufikisha huduma karibu ya wananchi. Na wakuu wa mikoa wote wawe wanachaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura while wakuu wa wilaya wawe 'Mameya' ambao nao wanachaguliwa kwa kura. Rais awe responsible kuteua mawaziri na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao pia wathibitishwe na bunge uaminifu wao kwa wananchi.
 
Mimi walipolazimisha mipaka ya mkoa wa Manyara sikuwaelewa kabisa.....na aliyechangia alikuwa Waziri mkuu wa wakati huo......hii ya sasa naona na huyu wa sasa nae akaingia ngomani pia

large_detailed_administrative_map_of_tanzania_with_all_cities_roads_and_airports_for_free.jpg
 
Tuache umbumbu jamani. Mbona mnakuwa kama watoto kwa michango yenu ya ajabuajabu. Kama huna hoja kaa kimya sio kila kitu uchangie

kwani we huu mchango wako sio wa ajabu.si bora ungekaa kimya.!!!
 
Nadhani wamelogwa, huhitaji shahada ya uchumi ili kujua kuwa kuongeza mikoa na wilaya ni kuongeza matumizi. Katiba mpya iondoe ukuu wa wilaya/mkoa. To start with, hakuna cha maana wanachokifanya, better have a whole elected local government with a governor like head answering to his/her electorate.
 
Ikitokea Chadema anashika nchi huu mfumo wa serikali wataufumua na hizi mikoa mpya zote zitapunguzwa...

Nikiwa hai nitarudi kuwapa kura yangu na fmilia yangu hata wakwe zangu ntawalazimisha wawape-wakikataa wawaache wanangu! Eboh!
 
Vipi Nakaaya atapata ule ukuu wa wilaya alio ahidiwa wakati anatoka chadema
 
Inayoelekea Kila PM atakyekuja nyumbani kawo uatakufanya Mkoa. Huu ni mwendelezo wa Mkapa na CCM yake
1. Sumaye alikuwa PM Tuakapata Mkoa wa Manyara
2. Pinda amekuwa PM tumepata mkoa wa Katavi na wila zake mbili (SIC!)

Guess who will be the next PM ili Tanzania tufikishe mikoa 31? (kwasasa
Tanganyika ina mikoa 25 na ZNZ 5)Kama Mwendelezo ndiyo huu kuna wakati Wilaya
ndiyo itakuwa Mkoa. E.g Mkoa wa Ukerewe una Wilaya moja ya Ukerewe au Mkoa
wa Mafia una wilaya moja ya Mafia!
 
Back
Top Bottom