Serikali yatangaza rasmi Mikoa mipya 4 na wilaya 19

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,548
29,621
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19

SERIKALI imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72.

Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyang'hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging'ombe.

Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe (Njombe) na Katavi (Mpanda).

Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang'hwale. Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging'ombe wakati mkoa wa Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na Itilima.

Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe (Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba); Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko (Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).

Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti); Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang'hwale (Kharumwa); Nyasa (Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging'ombe).

Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge, Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21. Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions),wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, MACHI 8, 2012.

==================================================

My Yake: Je kuna umuhimu wa lazima kuwa na mikoa mipya?
 
Shangazi , mjomba , rafiki watapata ajira
 
Hayo ya kuongeza mzigo wa viongozi na gharama za uendeshaji ndio wanaweza mambo muhimu kama kuinua uchumi na kuongeza ajira ni ndoto ukija masuala ya kushughulikia na kutatua migogoro kama ya madaktari, waalimu na migogoro ya ardhi na madini wanafyata mkia na kuingia mitini
 
Unaongeza ukubwa wa serekali wakati hata hzo zilizopo ni ngumu kuzihudumia. Au ndio yale yale ya kuongeza ukubwa wa serekali ili kila mtu aweze kupata fadhila?
 
Hizi pesa za kuhudumia hii Mikoa sijui zitatoka wapi? Kama za kuhudumia Mikoa iliyopo ni shida . Pesa za madakitari ni shida ! Za walimu ni shida ! Du Kweli ukiongozwa na boga lolote linawezekana
 
Hapo sasa ukiwauliza nini kitaendelea wenyewe wanahamaki na kukushangaa eti wewe mtu wa ajabu sana, wakati tunapata uhuru tulikuwa na mikoa mingapi na wilaya ngapi ukilinganisha na sasa. Kumbe hawajua watu wenye akili wanaangalia ubora na sio wingi
 
Badala ya kutoa taarifa kuhusu mgomo wa madaktari wanatoa taarifa kuhusu mikoa na wilaya mpya. Prioritization!!!
 
vipi hii itapunguza matatizo yetu au ndio itaongeza???? Poor tanzania
 
Kuna mikoa mpaka tunavyoongea wamesha exhaust bajeti zao yaani now till July ni mwendo wa tia maji tia maji.
Sasa iyo mipya labda ingoje bajeti ijayo!
 
wakati tunajaribu kuungana kuwa kitu kimoja wengine wanapambana kutugawa kwa kuanzisha maeneo mengine ya kiutawala kwa manufaa yao wenyewe ya kisiasa.

ndugu zangu kiukweli mie sikubaliani na hili jambo la kugawa mikoa mipya nawilaya mpya.ni kwa nini wanaongeza sehemu za kitawala ili hali wameshindwa kutawala maeneo yaliyopo.madhalani ukienda moshi kuna wilaya ya moshi mjini na moshi vijijini ila hakuna makao makuu ya wilaya ya moshi v na hivyo hivyo hakuna mkuu wa wilaya ya moshi vijijini acha hizo nenda dodoma kuna wilaya za bahi chamwino na dodoma mjini zote makao makuu yake yako dodoma mjini ndo hapo unajiuliza wanaofanya hivyo wanaangalia nini cha zaidi.
 
Tuache umbumbu jamani. Mbona mnakuwa kama watoto kwa michango yenu ya ajabuajabu. Kama huna hoja kaa kimya sio kila kitu uchangie
 
hapa sasa ukuu wa wilaya ingekuwa unagombea ningesema nikachukue fomu japo nijiliwaze na ukuu wa wilaya,

lakini ndo yale yale, mahawara na watoto wao waliowazaa nje ya ndoa zao ndo watapewa nafasi za uongozi ambao hakuna wanachokifanya, me sielewi hii serikali inachofanya ni nini?

its about time tuigawe hii nchi, maana itoshe sasa kugawa mikoa na kuongeza mzigo kwa serikali moja ambayo haina uwezo wa kuihudumia si tu mikoa iliyopo, achilia mbali mikoa mitatu tu.

Suluhisho la pekee sasa ni kuigawa hii nchi zitoke nchi tatu kila mmoja kivyake au tuwe na serikali ya majimbo japo manne ambayo kila mmoja ata manage jimbo lake kama usa.

Aaaaah me nimechoka sasa jamani.
 
Back
Top Bottom