Serikali yatakiwa kuwa kali

vexaaa

New Member
Jun 30, 2012
3
1
Serikali imetakiwa kuwa kali zaidi katika kuhakikisha kuwa mazingira ya biashara nchini yanaboreshwa badala ya kukomea kuunda kamati ambazo hutoweka baada ya mda mfupi, kabla hata hazijaleta mabadiliko yoyote.

Hayo yamesemwa na shirikisho la viwanda Tanzania katika tafrija ya kuzindua ripoti mpya inayoelezea vikwazo vya biashara nchini iliyofanyika Ijumaa usiku jijini Dar es Salaam.

“Tulichokiona sisi kama sekta binafsi ni kwamba taarifa zozote mbaya zinapotokea, serikali huunda kamati ambazo hutakiwa kupendekeza hatua za kuboresha. Kwa bahati mbaya, baada ya muda mfupi kamati hizo zinapopewa kazi hiyo hutoweka, na ndio imekua kama desturi sasa, ni mabadiliko madogo sana huwa yakifanyika,” alisema Mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la viwanda Tanzania Christine Kilindu.

Aliongeza kuwa “katika uhalisia mabadiliko yafanyikayo ni madogo na yanamudu kwa muda mfupi sana. Mfano mzuri ni ule wa Kamati ya Sekta binafsi iligundua kuwa ripoti iliyowasilishwa kwa kamati ya uendeshaji ilitofautiana sana na uhalisia unaotokea katika maeneo ya biashara.

Ripoti iliyozinduliwa inaitwa “Mitizamo ya Viongozi wa Biashara Juu ya Mazingira ya Uwekezaji Tanzania – 2011”.

Shirikisho la Viwanda Tanzania, sauti ya viwanda, ni chama cha sekta binafsi ambacho lengo lake kuu ni kutetea uwepo wa mazingira bora ya biashara ili kuzifanya biashara nchini Tanzania ziwe na ushindani.

Biashara ya ushindani ni muhimu katika kuinua pato la nchi: kwani zinazalisha ajira na kulipa kodi ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi.
 
Back
Top Bottom