Serikali yataka kumaliza tofauti za kisiasa Arusha kwa mazungumzo

mm naona njia njema kwa hawa watu ni huko mahakamani na kwa hili hakuna mazungumzo


nnapishana na ndugu yangu na waziri wangu, hawa wahuni si wakuzungumza nao amewaona makamba hawa ubabe walionao sheria tu ndio inayowafaa


Sawa taahira wangu. Anaetaka mazungumzo ni serikali na CCM. Aliyefungua kesi ni huyo huyo sasa mazungumzo ya nini? Kesi ikiisha asubiri kufunguliwa kesi ya ukatili dhidi ya binadamu ICC. Na wewe michango yote itapelekwa kama ushahidi wa uchochezi.
 
Nawaona hawa wawili wote wakiwa The International Criminal Court.

Mlipewa muda mrefu na Mtoto wa Mkulima akaahidi kuwa atasuluhisha.

Lowassa akasema pia msuluhishe mambo mapema maana Arusha siyo Tabora.

Makamba akamwijia juu na kumwaga utumbo wake. Sasa watu wawili wamekufa na wengine kujeruhiwa.

Kwa nini watu wasipelekewe Hague?

SOMEBODY MUST PAY FOR THIS.
kumbe rowasa ana akili kuwazidi wenzie,yeye aliacha party politics akaongea ukweli, wenzie naona mazezeta
 
Mwinyi alijiuzulu kutokana na mauaji yaliyotokea kule Shinyanga. Huyu Nahodha na wahusika wote wa haya mauaji ikiwemo wakuu wa polisi na FFU wa Arusha wanatakiwa wajiuzulu haraka sana na wale wote waliokamatwa waachiwe mara moja.

Na Mwinyi akaja kuwa Rais.....huyu KAPTENI nae aige mfano ili aukwae urais baadae(kwikwikwii)
 
Watu tumezoea viongozi wanafanya yale tunayawaza sisi tu. Natamani CHADEMA waingie madarakani alafu kutokee political unrest nione watashughulikia vipi.


mpumbavu kama wewe mwenye mawazo mgando na hasi kwa nini usichambe then ukaenda kulala!!!

unadhani chadema ni ccm......tatizo umezaliwa ukakuta wazazi wako ni watumwa.......unapoambiwa kuwa wazazi wako pamoja na wewe mko utumwani unakataa...... maana umezaliwa ukawakuta baba na mama yako wako utumwani......juha mkubwa mweeeeeee
 
Maoni yangu: Hawa Wazungu nina imani hawaji tena. Halafu tuwe tunalalamika kuwa Watalii hawaji. Taarifa za Ki-intelejia kilitakiwa kuangalia madhara yanayoweza kutokea.

1. Sasa Mmeuwa watu na wengine kujeruhi.
2. POLISI imetumia hela nyingi sana katika hili zoezi. Hela za walipa kodi.
3. Mmeleta usumbufu mkubwa sana kwa wananchi wa Tanzania.
4. Mmeleta usumbusu sana kwa Watalii.
5. Mmesababisha biashara za watu kudorola na nyingine kuharibiwa.
6. Mmeharibu sana soko la utalii Tanzania.
7. Mmeharibu jina la Tanzania kama nchi ya AMANI.
8. Dawa zitakazotumika kutibu hao walioumizwa, zimetumika bila ulazima.
9........................................




Kutoka kwa Maggid Mjengwa:

Vurugu Arusha Kuinufaisha Zaidi Kenya Kiutalii


Athari ya kwanza kubwa kiuchumi kwa yanayotokea Arusha ni kwa Tanzania kuinufaisha zaidi Kenya katika sekta ya utalii. Biashara ya utalii ni muathirika wa kwanza pale bomu la kwanza la machozi linapolipuliwa katika mji wa utalii kama wa Arusha. Pichani, watalii wanaonekana wakijifunika pua zao katikati ya jiji la Arusha jana mchana. Shughuli za kiuchumi zilisimama jana nzima katika jiji la Arusha. Katika nchi ambayo tayari lori lake la kiuchumi liko juu ya mawe, vurugu za kisiasa ndio kitu cha mwisho tunachokitarajia. Pande zote zinazohusika zitangulize busara zaidi katika kushughulikia tofauti zao. ( Picha ya hapo juu imepigwa naMussa Juma, mdau wa Mjengwa Blogu aliyeko Arusha na ambaye jana alikuwa chini ya mikono ya polisi.)

 
CCM ni wababaishaji, kuanzia rais wao, mawaziri, wabunge, viongozi wa polisi, jeshi n.k. Wenye akili zetu hatuwashangai. Tutaendelea kuwaelimisha wananchi ili waichukue nchi yao na kuitunza ipasavyo.
 
2.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia Mh. Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao Mkuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam mchana huu kuhusiana na vurugu zilizotokea jana wakati polisi walipozima maandamano ya wanachama wa Chadema mkoani Arusha jana. Mh. Shamsi Vuai Nahodha ametangaza kwamba katika vurugu hizo watu wawili wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa wakati wa zoezi la kuzima maandamano hayo jana. Ameongeza kwamba Serikali imeamua kuutatua mgogoro huo katika ya pande mbili zinazokinzana katika mkoa wa Arusha ambapo amesema njia nzuri ya kumaliza mgogoro huo ni kuwasuluhisha kwa njia ya Mazungumzo ili kuleta amani mpya katika mkoa huo. Katika picha kushoto ni Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ambaye ndiye aliyetoa amri ya kutoruhusu maandamano na kuruhusu mkutano wa hadhara kuendelea huku akisisitizia kwamba jeshi la polisi litaongeza ulinzi zaidi ili kuleta amani katika mkutano huo. wakati akizungumza wa waandishi wa habari siku moja kabla ya maandamano hayo.

kuleta amani ama kuvuruga amani
hivi huyu IGP Mwema anajua maana ya maandamano ya amani?
Kwa kifupi police ndio wamevuruga amani na si wafuasi wa CDM
 
Kilichotokea Kwenye Maandamano Arusha: Tafsiri Yangu (Maggid, Iringa).




Ndugu Zangu,


JUMA lililopita Watanzania, na dunia pia, tuliona kupitia televisheni na vyombo vingine vya habari, picha zikiwaonyesha polisi wetu wakipambana na waandamanaji wafuasi wa Chama Cha Wananchi, CUF. Ilisikitisha sana.


Pengine polisi ‘kupambana' na waandamanaji si neno sahihi. Mara nyingi tunachokiona ni polisi 'kuwaandama' waandamanaji. Hii ni pamoja na polisi kuwatawanya waandamanaji kwa virungu, mabomu ya machozi, risasi za mipira na hata za moto.


Jana tena, Watanzania na dunia, tumeona picha za televisheni zikiwaonyesha polisi wetu wakipambana ama kuwaandama waandamanaji wafuasi wa CHADEMA kule Arusha . Imeripotiwa na BBC kuwa kuna Watanzania waliopoteza maisha. Inasikitisha sana. Na unapoangalia picha hizi zenye kuharibu taswira njema ya nchi yetu ndani na nje ya mipaka yetu unajiuliza; KWANINI?


Kinachonijia haraka kichwani ni hofu ya mfumo. Linanijia pia neno ´MAANDAMANO´. Afrika MAANDAMANO ni neno baya sana ukilitamka mbele ya watawala. Kuandamana ni 'kuiandama' Serikali. Ni kama ilivyokuwa katika nchi za Kikomunisti kabla ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin. Kwa wasiojiamini ndani ya mifumo ya kiutawala Afrika, kuandamana ni sawa na kutaka ´Kuuvunja Ukuta´. Na kwa watu wa nchi zetu hizi, nao wameanza kuuona ukuta.


Kwa watawala Afrika, hakuna msamiati wa ' Maandamano' , kuna ' MATEMBEZI ya MSHIKAMANO'. Afrika hakuna dhambi ya kuandamana kuunga mkono au kupongeza kauli au jambo lililotendwa na upande wa utawala. Dhambi ni kuandamana kupinga. Tujiulize tena; nini maana ya maandamano?


Tunaamini katika demokrasia, maandamano ni namna pia ya kujieleza. Muhimu katika maandamano ni kuhakikisha kuwa yanakuwa ni ya amani na utulivu. Wenye kuandamana waandamane na wengine waendelee na shughuli zao. Na hapa ni jukumu la wenye kuandaa maandamano kwa kuwashirikisha polisi.


Kuwepo na utaratibu unaoeleweka. Wapi waandamanaji watakusanyikia kabla ya kuanza maandamano. Hivyo basi, wapi maandamano yataanzia, umbali wa kilomita ngapi, kwa kupita barabara zipi na wapi yataishia. Hayo yanaweza kufanyika kwa ustaarabu kabisa.


Jukumu la polisi litakuwa ni kuyaongoza na kuhakikisha hakuna vurugu zinazotoka miongoni mwa waandamanaji, na si kinyume chake. Kwanini kuwepo na hofu ya vurugu wakati wenye kuandamana ni wafuasi wa chama au kikundi kimoja cha kijamii kwa wakati mmoja, tena wakiwa na viongozi wao?


Katika nchi za wenzetu, polisi huwa na kazi ngumu na hata kufikia kuwaambia waandaaji wa maandamano kusitisha maandamano kama maandamano husika yatasababisha kuwepo na maandamano ya kupinga maandamano hayo katika wakati mmoja kutoka kwa kundi lingine. Sisi hatujafikia huko. Kwa mfano, Dar wafuasi wa CUF wakiandamana kwa amani, wafuasi wa CCM huwaoni kufanya maandamano ya kuwapinga CUF kwa wakati huo huo, na kinyume chake.


Dunia imebadilika, tunahitaji kubadilika pia. Jeshi letu la polisi lijipange upya. Kwa jinsi picha za televisheni zinavyoonyesha polisi wetu wanavyowapiga virungu na hata kuwarushia risasi waandamanaji wasio na silaha inaamsha hisia mbaya kwa Watanzania. Inaleta taswira mbaya ya nchi yetu kwa jumuiya ya kimataifa. Inasikitisha sana. Ni aibu kwa nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda sana. Tubadilike.
Maggid, Iringa


My Take: Mtani wangu Maggid, kwa hilo hapo juu, tupo pamoja kabisa. Hakukuwa na haja ya kuzuia maandamano. Ingelikuwa waliruhusu na kulinda watu wasifanye fujo, leo watu tungelikuwa tumesahau jana kulitokea nini Arusha. Huyu MEYA wa CCM aliyepachikwa hapo hicho cheo, aachie tu ngazi maana hiyo kazi yake tayari watu wamemwaga damu. Nampa pole sana.
 
f$@$%&*k it!!

Hii ni funika kombe mwanaharamu apite. No f$@$%&*?~^g way!
 
ukitaka kujua huyu jamaa(nahodha) ni juha alipaswa kuwa arusha na sio dar.....hapa anapiga domo sasa hvi wakati ndugu yangu Dennis na wengine wamepoteza maisha........ huu ni upumbavu mkubwa sana....


Hapo umenena mzee. Hivi ilikuwaje Nahodha na waziri wa elimu ya juu kukimbilia UDOM kwenye mgomo wa wanafunzi tu tena wa kata halafu yeye na IGP wake wanashindwa kwenda Arusha ambako ndiyo kwenye matatizo makubwa tena yanayohusu nchi na usalama kwa ujumla. Au wanataka kusema Arusha hakuna vyombo vya habari vya kulitangazia taifa??
 
mpumbavu kama wewe mwenye mawazo mgando na hasi kwa nini usichambe then ukaenda kulala!!!

unadhani chadema ni ccm......tatizo umezaliwa ukakuta wazazi wako ni watumwa.......unapoambiwa kuwa wazazi wako pamoja na wewe mko utumwani unakataa...... maana umezaliwa ukawakuta baba na mama yako wako utumwani......juha mkubwa mweeeeeee

Big up, watumwa wapo wengi, elimu iendelee, tutawotoa tu utumwani kwa kuitumia nguvu ya umma hata kama hawataki, maana bado wanathamini vipipi vya mabwana zao!
 
Hili ndo jiji la kitalii, kila kitu kinapatikana hapa. Hata fujo za polisi hapa ndo kwao.
 
Hii kauli ingetangulia mwanzo pasingemwagika damu. Baada ya kumwaga damu uko zanzibar tunakushukuru kwa kuja na kasi mpya bara ya kunyonya damu za watu wanaodai haki. Tuachie Tanganyika yetu urudi kwenu Zanzibar au nenda kabisa Afghanistan ukajiunge na ndugu zako magaidi wa Alqueda. Wizara yako si ya usalama wa raia ni ya usalama wa CCM
Mdebwedo!
 
PM Pinda alisema by 5th January wangemaliza mgogoro wa umeya Arusha ambao ndio chanzo cha yote hayo, lakini hakuna lolote!! Hii ni geresha nyingine.

Na pinda anapaswa kuwajibika kwa kushindwa kumaliza mvutano huo kama alivyoahidi.
 
Tubadilike. Hilo nalo ni neno. Lakini Maggid kwa nini unashindwa kuwaambia watawala WABADILIKE? Wananchi wamebadilika siku nyingi kutokana na KUSHINHWA KWAO NA MAJUKUMU WALIOWAPA wao wanaona wanatishiwa. WASHAURI KAMA UNAVYOFANYA HAPA WABADILIKE
 
nahodha aende zake huko, why now? hayo majumba mliyojenga, viwanda vyenu mliojimilikisha tukiamua vitabaki majivu tu. risasi zote zitaisha na tutabaki na mapanga na sime. Its a very bad governance.
 
2.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia Mh. Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao Mkuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam mchana huu kuhusiana na vurugu zilizotokea jana wakati polisi walipozima maandamano ya wanachama wa Chadema mkoani Arusha jana. Mh. Shamsi Vuai Nahodha ametangaza kwamba katika vurugu hizo watu wawili wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa wakati wa zoezi la kuzima maandamano hayo jana. Ameongeza kwamba Serikali imeamua kuutatua mgogoro huo katika ya pande mbili zinazokinzana katika mkoa wa Arusha ambapo amesema njia nzuri ya kumaliza mgogoro huo ni kuwasuluhisha kwa njia ya Mazungumzo ili kuleta amani mpya katika mkoa huo. Katika picha kushoto ni Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ambaye ndiye aliyetoa amri ya kutoruhusu maandamano na kuruhusu mkutano wa hadhara kuendelea huku akisisitizia kwamba jeshi la polisi litaongeza ulinzi zaidi ili kuleta amani katika mkutano huo. wakati akizungumza wa waandishi wa habari siku moja kabla ya maandamano hayo.

Wanafiki wakubwa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom