Serikali yasitisha kubinafsisha Shirika la Madini Tanzania

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Sasa rudisheni Kiwira Coal Mining iliyokwapuliwa kifisadi na fisadi Mkapa chini ya STAMICO

Posted Date::6/16/2008
Serikali yasitisha kubinafsisha Shirika la Madini Tanzania
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

SERIKALI imesitisha mpango wa kulibinafsisha Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

Uamuzi huo wa serikali kusitisha mpango huo, unatokana na msimamo wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kuitaka serikali kuiondoa Stamico katika orodha ya mashirika yanayopaswa kubinafsishwa.

Akitangaza uamuzi huo hivi karibuni, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, alisema serikali iko katika mchakato wa kutekeleza ushauri huo wa wabunge.

Ngeleja alifafanua kwamba, kwa kuwa uamuzi wa kuibinafsisha Stamico ulitolewa na Baraza la Mawaziri, kinachofanyika sasa ni kuandaa taratibu za kulirudisha suala hilo katika baraza hilo ili litazamwe upya.

"Kuhusu ombi la kamati kutaka Stamico iondolewe katika orodha ya mashirika yanayobinafsishwa, hili nasema tumelisikia na tunalifanyia kazi," alisema Ngeleja na kuongeza:,

''Taratibu za kuiondoa Stamico katika orodha ya mashirika yanayopapswa kubinafsishwa zinaendelea na kwa kuwa uamuzi huu ulifikiwa na Baraza la Mawaziri, tunafikiria kulirejesha suala hili huko.''

Waziri Ngeleja alithibitisha kwamba, serikali haitabinafsisha Stamico kwa sasa kama ilivyoombwa na wabunge.

Kamati hiyo ya Bunge, mapema mwaka huu, iliitaka serikali kuachana na mpango wa kulibinafsisha shirika hilo na kutaka iliondoe katika orodha ya mashirika ya umma yanayopaswa kubinafsishwa.

Tangu kuwepo mageuzi ya uchumi katika miaka ya 1990, mashirika mengi muhimu ya umma kama Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Shirika la Umeme (Tanesco) na mengine nyeti, yamekuwa yakikodishiwa menejimenti mbovu za kigeni au kubinafsishwa kwa wawekezaji wahuni.
 
Back
Top Bottom