Serikali yashindwa kulipa wafanyakazi, yapunguza maslahi kimyakimya

Bora hata hao waliokatwa lakini kidogo wamekipata!! Huku wilaya ya Ludewa bado hatujalamba hata senti na tangazo lililopo ofisi ya mkurugenzi linatuambia hadi kuanzia tar 10 ndo watajua hatma ya hiyo mishahara...
Mweeeeeeh! Kumbe tupo wengi!
 
Hazina wako busy wanaadhimisha miaka 50 ya uhuru! Alitoa wazo hili la hizi sherehe alaaniwe kabisa! Eti tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele!!!!!
 
Hapa siyo ccm wala chadema ni ulafi tu..lini umesikia lema au zito kugoma kuchukua mshahara wa ubunge kwasababu ni mnono mno?wake up tanzanians

Mkuu kwa haya majina mawili nafikiri umesahahu manake ndiyo yaliyojitokeza waziwazi kupinga malipo manono ya wabunge!
 
habari hii ni ya kichochezi,uzushi,chuki na umbea.....haina ukweli hata kidogo....kawadanganye wadogo zako huko kijijini ambao hata ukiwaambia binadam ana miguu minne 4 watakuamini bila kukuhoji au kuhoji uhalisia
 
habari hii ni ya kichochezi,uzushi,chuki na umbea.....haina ukweli hata kidogo....kawadanganye wadogo zako huko kijijini ambao hata ukiwaambia binadam ana miguu minne 4 watakuamini bila kukuhoji au kuhoji uhalisia
Welldone Mr Mkulo, sasa tuambie ni lini utatulipa mishahara yetu ya mwezi oktoba maana leo ni tarehe 31 na kwa logic ya mwezi kuwa na siku 28 leo ni mwezi mwingine
 
Mwenzenu kaleta standing order, nanyi mnaopinga leteni ushahidi wenu. Vinginevyo mnadhibitisha kuwa mnatumiwa kulinda maslahi ya genge la m.k.were na wenzake.

Umeishiwa hoja lala ujambejambe kuliko kuleta ushuzi wako humu hakuna kitu kamna hicho posho zote zimelipwa na waliopanda mishahara wamelipwa hakuna aliyeshushwa mshahara we kimavi tu unawanga humu kenge weeeee
 
maafisa waandamizi(wakubwa)wanalipwa utilities(umeme na maji)385,000/= hadi 460,000/= kwa mwezi,housing allowance ni 600,000/= hii ni flat kwa wote kuanzia kwa waziri hadi katibu tawala wa wilaya,..yaani hayo marupurupu yanazidi mshahara wa kuanzia wa any graduate serikalini tena basic salary sio net...we will get there someday,.i believe...

Si hamtaki maandamano, sasa sijui mtafanya nini. Eti mbunge anapata seating allowance?. Na walimu wapate standing allowance.
 
ndugu yangu mimi ni mtumishi wa serikali kada mojawapo ya afya anachozunza mtoa mada ni sahihi kabisa, mimi mwenyewe nimeshtukia ''take home'' yangu imekatwa kwa tshs laki mbili; vuguvugu la madai lishaanza maeneo mbalimbali, lakini halina nguvu kwa sababu kada ya afya haina chama ambacho ni strong, badala yake wana lazimishwa kuingia chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGU) chama ambacho hakina dira wala mwelekeo kama kilivyo chama fulani cha siasa hapa nchini

Hivi ni lini wewe mfanyakazi wa Serikali utaamka na kuelewa kwamba HAKUNA chama cha kweli cha maslahi ya wafanyakazi ambacho kujiunga kwake ni kwa 'kuingizwa' au 'kupelekwa' au 'tumeambiwa chama chetu ni hiki au kile'. Matunda ya usingizi ni udenda tu, hakuna miujiza.
 
Unaweza kuona ni nanma gani sometimes jf ina vichwa vya ukweli na vichwa maji. Hii post ilitumwa june 2nd 2011 kipindi cha bugdet,watu wakachangia wakiunga mkono hoja wengine wakibisha, but ukweli umeanza kuonekana, mwezi huu oct mshahara umechelewa,na wengine bado hawajapata, hakuna ajira mpya,standing order imebadilishwa,allowance zimepunguzwa, na kila kitu kinafanya kimya kimya. Na bado subirini muone mwezi ujao.baathi ya idara za serikali budget zao zilipitishwa na kupangiwa fedha, cha kushangaza mpaka sasa hela inayotolewa ya bugdet za idara hiyo ni za mafungu mafungu kama vile mpaka mtu adundulize ndo akupe.matokeo yake mipango iliyopangwa na idara hizo kwa mwaka huu wa fedha haitekelezeki kisa hakuna pesa. Nasikitika sana tena sana kwa hali kama hii cause am one othe victims ktk taasisi ninayofanyia.serikali haitaki kusema ukweli. Inadanganya wadanganyika kila kukicha .,
 
Si hamtaki maandamano, sasa sijui mtafanya nini. Eti mbunge anapata seating allowance?. Na walimu wapate standing allowance.

allowance ya mwalimu ni kula uroda na mwanafunzi,hii walimu wanaiita marupurupu ya ualimu au kukamilisha gamba(cheti).upo hapo?
 
kuitetea serikari ya ccm yakubidi uwe chizi au uwe mwizi!
hako kahela ukienda nako sokon unarudi na mawazo ya kuibiwa kumbe imeisha kihalali, mlipuko wa bei!!!!!!!!!
 
Habari za kuaminika kutoka jikoni zinasema serikali imesitisha ghafla malipo yoote. Huu mjadala nimeukuta wakubwa wa kuaminika wakijadiliana na kubishana kuhusu kusimama kwa shughuli zao zote walizokuwa wamepanga hivi karibuni. Wailoko jikoni tafadhali mtujuze kama ni hatua za dharura za kuurekebisha uchumi, ni hali mbaya ya kifedha au ni kawaida kutokana na taratibu labda za ukaguzi?

Hivi ninavyoongea kuna watu wanahaha!

Waungwana mlioko huko jikoni na wapenda nchi tuwekeni sawa.
 
Inawezekaana ndio maana hata mishahara hatujapata kwa sababu serikali haina hela?kwanini serikali hamtaki kutoa ukweli wa fununu hizi?
 
Kuna harufu ya ukweli katika habari hii.

Mwezi uliopita niliwasikia wakulu flani wanafanya kazi bandari, wanalalamika kwamba shughuli nyingi zimesimama serikali haijawapelekea mafungu!!
 
Back
Top Bottom