Serikali yashinda kesi ya samaki wa Magufuli

Mbona sijaelewa hii hukumu waliotiwa hatiani ni wawili mmoja alipe bil 21 ama jela 20 mwingine alipe bil 1 ama 10 jela.sasa mbona inatatiza mi naona ni bil 2 na sio 21 ili maana ipatikane
 
hatimaye serikali imeshinda kesi dhidi ya wavuvi haramu(wale wachina waliokamatwa na meli ikiwa imejaa shehena ya samaki)

Leo mchana serikali imeshinda kesi hiyo...na hukumu ilikuwa hivi:

Watuhumiwa wawili ndio wamekutwa na hatia,wengine wameachiwa huru.

Hawa wawili waliokutwa na hatia mmoja inatakiwa alipe billlion 21 za kitanzania au kwenda jera miaka 20.

Mwingine naye alipe billion 1 au kwenda jera miaka kumi pia ile meli iliyokamatwa, hakimu ameridhia ombi la mawakili wa serikali kuwa itaifishwe na iwe mali ya serikali ya Tanzania. (kwa sasa ile meli ipo hapa nchini, na sehemu iliyopo imeshaanza kuzama....hivyo basi nijukumu la serikali kuhakikisha meli hiyo ama inatengenezwa ama inauzwa mapema iwezekanavyo.
www.tanzaniatoday.co.tz/news/wachina-wa-magufuli-waidai-serikali-trilioni-13
 
Back
Top Bottom