Serikali yashinda kesi ya samaki wa Magufuli

Imekula kwetu ipasavyoooo!
sasa wachina wanadai zaidi hicho alicholeta TUNTEMEKE!
 
Last edited by a moderator:
Niko nasoma gazeti la Mtanzania nalinganisha na habari hii naona vitu viwili tofauti

Yaani wa-Tz tuna mambo ya ajabu sana! Kesi hii kwenye huu uzi ni ya mwaka 2012, sasa kinachokuchanganya ni kitu gani? Shida yenu hamjipi muda Wa kusoma na kuelewa, mkiona kichwa cha habari tu mnakimbilia kutoa comments!
 
kuanzia leo lile gazeti lililoandika Magufuli aangukia pua ntalichukulia kama kipeperushi.

Duh!!! unashabikia issue ya 2012 wakati taarifa sahihi za August 2014 serikali imebwagwa na tunatakiwa kulipa.
 
Yaani wa-Tz tuna mambo ya ajabu sana! Kesi hii kwenye huu uzi ni ya mwaka 2012, sasa kinachokuchanganya ni kitu gani? Shida yenu hamjipi muda Wa kusoma na kuelewa, mkiona kichwa cha habari tu mnakimbilia kutoa comments!

Sasa hapo unanielewesha au unanitukana? WaTz mna matatizo mengi sana ndo mana mnaongozwa na mtu asiyejua kwa nini mko hivyo
 
Duh!!! unashabikia issue ya 2012 wakati taarifa sahihi za August 2014 serikali imebwagwa na tunatakiwa kulipa.

sijui bilioni ngapi sasa. duh!

cheki hii site upate kujiongezea kipato.

http://monthlyyouth.com/?ref=375920
 
Sasa hapo unanielewesha au unanitukana? WaTz mna matatizo mengi sana ndo mana mnaongozwa na mtu asiyejua kwa nini mko hivyo

Uwiiii!! Mkuu umenishukia!! Sentensi hiyo ya mwisho imevunja mbavu aisee, nisamehe mdogo wangu!
 
Serikali isilipe alipe Magufuli au CCM

Sioni kama ni sahihi kumlaumu Magufuli katika hili kabla ya kujiuliza maswali yafuatayo:

1. Je haki imetendeka..?

2. Kama haki imetendekea, je, hii kesi ingechukua muda mfupi kama inavyotakiwa, hasara ingekuwepo..? Yaani, kwa jinsi ilivyokuwa straight forward, hii kesi ilipaswa kuisha hata kabla samaki hawajaoza..

3. Mahakama na mamlaka husika zimefanya kazi yao ipasavyo..? Hii inahusisha kufanya uchunguzi wa kina na kuwahoji wale wote waliokuwa na taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa meli hiyo..

4. Kwa upande wangu Magufuli alifanya maamuzi kama kiongozi au mwenye nyumba aliyekuta mwizi ndani ya himaya yake na kumpeleka kwenye vyombo vya dola.. Kwa hiyo ilikuwa kazi ya dola kufanya uchunguzi kwa haraka na kufanya maamuzi kwa haraka.. Sidhani uzembe wa kesi kuchukua miaka zaidi ya minne ni kosa la Magufuli...

Endapo hayo hapo juu ni kinyume na hali halisi, then you can blame Magufuli (in my perspective)..
 
Hizi taarifa niza uongo..wachina wameachiwa jana/juzi na kuamuriwa warudishiwe kilakitu ikiwemo samaki wenye dhamani ya b2 na meli yao iliyozama pamoja na hati zao za kusafiria wacha kupotosha mkuu

hatimaye serikali imeshinda kesi dhidi ya wavuvi haramu(wale wachina waliokamatwa na meli ikiwa imejaa shehena ya samaki)

leo mchana serikali imeshinda kesi hiyo...na hukumu ilikuwa hivi:

Watuhumiwa wawili ndio wamekutwa na hatia,wengine wameachiwa huru.

Hawa wawili waliokutwa na hatia mmoja inatakiwa alipe billlion 21 za kitanzania au kwenda jera miaka 20.

Mwingine naye alipe billion 1 au kwenda jera miaka kumi pia ile meli iliyokamatwa, hakimu ameridhia ombi la mawakili wa serikali kuwa itaifishwe na iwe mali ya serikali ya tanzania. (kwa sasa ile meli ipo hapa nchini, na sehemu iliyopo imeshaanza kuzama....hivyo basi nijukumu la serikali kuhakikisha meli hiyo ama inatengenezwa ama inauzwa mapema iwezekanavyo.
 
Hii kesi nilisha isahau....duuu😳.....

"The truth is hard to swallow when you're choking on your pride."
 
Hizi taarifa niza uongo..wachina wameachiwa jana/juzi na kuamuriwa warudishiwe kilakitu ikiwemo samaki wenye dhamani ya b2 na meli yao iliyozama pamoja na hati zao za kusafiria wacha kupotosha mkuu

kwa mwaka ambao hii thread ilipo anzishwa mtoa mada alikua sahihi kabisa.....someni na tarehe za post jamani msikurupuke.
 
Back
Top Bottom