Serikali yasalimu amri kwa Lema, waziri kivuli

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,884
6,885
Uchunguzi wa Mauaji
Katika hatua nyingine, Werema amekiri bungeni kwamba Serikali imekuwa dhaifu kwa kutochunguza vifo vya raia ambavyo vimekuwa vikitokea katika mazingira yenye utata na kuahidi kwamba taratibu zinafanywa ili uchunguzi ufanyike.

"Nakiri kwamba tulilegalega kidogo kwa kutofanya uchunguzi wa mauaji yaliyotokea bila kujua sababu zake, lakini tumejiandaa shughuli hiyo itaanza karibuni".

Alisema uchunguzi wa vifo hivyo utafanywa na Mahakama za Korona (Coronerย’s Court) ambazo zilikwishaundwa tangu mwaka 2004 kwa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali namba 252 la Julai 16, 2004.

"Jaji Kiongozi kwa kushirikiana na Jaji Mkuu waliwateua mahakimu wote wakazi kuwa makorona (viongozi wa Mahakama za Korona), hivyo watu wa kufanya kazi hii (ya uchunguzi) wapo. Tutatumia taarifa hizi zilizotolewa, ipo ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora na yingine ili kujua nini hasa kilichotokea," alisema Jaji Werema.

Kwa muda mrefu Chadema kimekuwa kikishinikiza kufanywa uchunguzi wa mauaji kadhaa ambayo kinadai kuwa yalifanywa na polisi katika sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Arusha, Tabora na eneo la Mgodi wa Nyamongo mkoani Mara.

Lema, akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani juzi, alihoji sababu za kutoundwa kwa mahakama za uchunguzi wa mauaji hayo.

Alisema uundwaji wa mahakama hizo ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (The Inquest Act) Sura ya 24 na kwamba Waziri Mkuu wakati anahitimisha mjadala kuhusu Bajeti ya ofisi yake, alikubaliana na ushauri wa kambi ya upinzani kwamba Serikali itaanzisha mahakama ya kuchunguza mauaji hayo.

"Kambi rasmi ya Upinzani inachotaka sasa ni kuona utekelezaji. Je, ni lini waziri mwenye dhamana atatangaza uteuzi wa kuundwa kwa mahakama hiyo katika Gazeti la Serikali ili wauaji wahukumiwe? Tunataka uchunguzi ufanyike haraka ili haki itendeke mapema," alisema Lema.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo, Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania, kifo chochote ambacho kimetokea katika mazingira ya shaka kinatakiwa kuchunguzwa. Uchunguzi huo ni pamoja ule wa kidaktari ili kubainisha sababu halisi ya kifo husika na hatua ya pili ni uchunguzi wa kimahakama kwa kutumia mahakama ya korona ili kujiridhisha kwamba kifo hicho hakijatokana na vitendo au sababu za kijinai.

Mwananchi
 
Katika hatua nyingine, Werema amekiri bungeni kwamba Serikali imekuwa dhaifukwa kutochunguza vifo vya raia ambavyo vimekuwa vikitokea katika mazingira yenye utata na kuahidi kwamba taratibu zinafanywa ili uchunguzi ufanyike.

"Nakiri kwamba tulilegalega kidogo kwa kutofanya uchunguzi wa mauaji yaliyotokea bila kujua sababu zake, lakini tumejiandaa shughuli hiyo itaanza karibuni".

Kwa kauli hii ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kwamba serikali inakiri kwamba ni dhaifu na legelege. Kwa maana hiyo yasemwayo na wabunge wa vyama vya upinzani yana ukweli mtupu.
 
Kwa kauli hii ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kwamba serikali inakiri kwamba ni dhaifu na legelege. Kwa maana hiyo yasemwayo na wabunge wa vyama vya upinzani yana ukweli mtupu.

Kwa kauli hiyo na yeye Mwanasheria Mkuu wa Serikali anakiri ama kazi imemshinda au hajui kazi yake.
 
Namkumbuka kiraza Lukuvi alipojaribu kumponda Lema alafu leo wanasalimu wenyewe,kweli CDM is beyond words,big up!
 
kama Serikali inalegalega kwenye usama wa wananchi wake , je inamtumikia nan? natamani watz tungeungana tukaondoa haya mabepari,mabeberu madarakani
 
Ile sinema ya Lukuvi kupinga ilikuwa political show tu na kukurupuka si unajua wanasiasa wetu wanafikiri upinzani ni kupinga kila kitu alifanya hivyo ili aonekane kwa boss wake, lakini Lema alizungumza mambo ya msingi kabisa yanayogusa maisha ya kila siku baina ya asikari polisi na wananchi si tunayaona.
 
Mtu muungwana hukiri makosa yake pale yanapojitokeza. Mimi nampongeza Werema kwa kuwa sensible. Sasa kama kuna wanaodhani huo ni udhaifu kwa serikali au ushindi kwa Lema mimi sijui!
 
Wao wana pesa, Sisi tuna Mungu, tunaamini Ukweli siku zote ni Mshindi.
 
Mtu muungwana hukiri makosa yake pale yanapojitokeza. Mimi nampongeza Werema kwa kuwa sensible. Sasa kama kuna wanaodhani huo ni udhaifu kwa serikali au ushindi kwa Lema mimi sijui!
Kukiri udhaifu ni uungwana lakini hakuondoi udhaifu wenyewe.
 
sasa watachunguza vipi wakati wao ndio wahusika wa moja kwa moja? Raia wengi sana wanauliwa kwa kusingiziwa majambaz!
 
Serikali ya kipopompo, ni upopompooo mpaka bungeni. Hatutegei wao kutuletea +ve aideas. Ni upopompo mtupu.
 
werema hata simwamini huyu jamaa alishawahi kusema haitawezekana kuwa na mchakato wa katiba mpya...leo anasema hivi kesho anakuja na mawazo mengine..ila cha moto wamekiona sana...
 
Katika haya mapambano ya kuikomboa Tanzania ni wazi kabisa upinzani hasa wenzangu wanachadema watashinda kutokana na kwamba wanaupeo wa kuona mbali na hawaogopi kusema nini kifanyike. Sasa kwa serikali yetu ya Kikwete ambayo haiko tayari kukaa na wenzao na kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili wananchi basi maandamano ni ya msingi na mwisho wa siku watasikia kama hivi...! Aluta Continua.
 
Mtu muungwana hukiri makosa yake pale yanapojitokeza. Mimi nampongeza Werema kwa kuwa sensible. Sasa kama kuna wanaodhani huo ni udhaifu kwa serikali au ushindi kwa Lema mimi sijui!

Mkuu, Nakubaliana na wewe kwa hili.
Nadhani ndo utamaduni tunaopaswa kuujenga penye ukweli tuwe wazi kuukubali hata kama umetoka upande wa upinzani, na hapa basi Nami nampongeza Werema kwa hilo.
 
Amebadili msamiati tu alipaswa kusema SERIKALI IMEKUWA LEGELEGE
<font color="#000080"><b>Kwa kauli hii ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kwamba</b></font><font color="#800000"><b> serikali inakiri kwamba ni dhaifu na legelege.</b></font><font color="#000080"><b> Kwa maana hiyo yasemwayo na wabunge wa vyama vya upinzani yana ukweli mtupu. </b></font>
<br />
<br />
 
Nguvu ya hoja unaweza tu kuizuia kwa muda lakini itaendelea kukutafuna kama kansa na baadaye ukweli utadhihirika.... Huyu lukuvi ni Kilaza kazi aliyopewa imemshinda hana elimu ya kutosha.
 
Back
Top Bottom