Serikali yapiga marufuku wanafunzi kudaiwa michango

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SERIKALI imepiga marufuku wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kudaiwa michango au kurudishwa nyumbani kwa kukosa michango na kuagiza kazi hizo zifanywe na Bodi na kamati za shule.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Elimu, Kassim Majaliwa alisema hayo jana baada ya kutembelea Shule ya Msingi Hananasif jijini Dar es Salaam ambayo wanafunzi wake walisimamishwa masomo kwa kushindwa kuchangia matofali.

Alisema wanafunzi wa shule zote za msingi na sekondari hawahusiki kukusanya vifaa vya ujenzi au michango yoyote bali kazi hiyo inapaswa kufanywa na Bodi ambayo inasimamia jukumu hilo badala ya wazazi.

“Kazi ya mwanafunzi ni kuingia darasani na kusoma na utekelezaji wa masuala yoyote Bodi ndiyo inahusika, mwanafunzi haruhusiwi kutumika kukusanya michango labda kupeleka barua kwa mzazi wake tu, kitu kama hicho kisionekane tena popote,” alisema.

Alipiga marufuku michango holela inayopangwa na walimu na badala yake kuitaka Bodi au Kamati ya Shule kuamua michango hiyo na kuibeba wenyewe badala ya kuwaelekeza au kuwaagiza wanafunzi.

Akizungumzia sakata la wanafunzi wa shule hiyo, kurudishwa alisema ni marufuku mwanafunzi kuhukumiwa au kurudishwa kwa sababu ya kukosa michango na kusema kuwa suala la ujenzi wa uzio wa shule ni la Serikali ya Kijiji na uongozi wa shule hiyo.

“Hatutegemei tena kuona wanafunzi wanakwama kwa ajili ya michango mana ni ya shule na si ya Serikali, hivyo nisisikie tena mwanafunzi amesimamishwa kwa sababu lengo la Serikali ni kila mwanafunzi kupatiwa elimu,” alisema.

Alisema mfumo na utaratibu uliotumiwa katika shule hiyo haukubaliki kwa sababu wakati mwingine walimu wamekuwa wakichangishana fedha za kumlipa mlinzi hali ambayo si sahihi na kuwataka maofisa Elimu kusimamia shule zao ili jambo kama hilo lisijirudie tena.

Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Taaluma katika shule hiyo, Hamis Mohamed alisema shule hiyo ilimtaka kila mwanafunzi kuchangia matofali mawili kwa ajili ya ujenzi wa uzio, ili kudhibiti uhalifu unaofanyika katika shule hiyo ukiwemo ubakaji.
 
Serikali hii au nyingine? Maana yake mtadaiwa zaidi mpaka mkome kuzaa, ila wachangishaji wanatakiwa kufanya MAMBO KIMYA KIMYA TUuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!
 
tatizo sio waalimu ni kamati na Bodi za shule je zipo tayari kuchangia hao walinzi au wazazi wapo tayari sehemu kubwa ya jamii za tanzania tumezoea kutupa mzigo kwa waalimu!lakini chanzo huwa ni kamati za shule sababu nimefundisha nafahamu hilo wazazi huwa ni wagumu sana kutoa fedha za chaki na michango ya kumlipa mlinzi nakadhalika sasa mlinzi akiona kimya anawakaba waalimu wamlipe!waalimu wakiwabana wazazi wazazi wanasema serikali inatoa fedha kumbe wala hakuna fungu la mlinzi wala matumizi mengine na majibu ya serikali ndiyo kama hayo any way tz yetu hii michezo hiyo naifahamu sana inavyofanyika ila mzigo na lawama zoote huwa zinaishia kwa waalimu mie nadhani waziri alitakiwa akutane na kamati ya shule kwanza kabla ya kuanza kuwalaumu waalimu au angekutanisha kamati za shule na waaalimu au kama inawezekana walinzi wa shule nao waajiliwe na serikali na hata shule zijengwe na kulindwa na serikali mwalimu ibaki kazi yake kufundisha tuchaki na mambo mengine yote vitolewe na serikali kuna shule nimeshawahi kusimamia mtihani darasa la saba nilikuta waalimu hawana chaki wanaandikia mihogo mikavu!jamani huko vijijini msiombe waalimu wana shida sana!
 
Back
Top Bottom