Serikali yapata hasara 93bn/- barabara ya Dodoma- Manyoni
Na Mwandishi wetu
16th June 2009
Barabara ya Dodoma- Singida.
Serikali imepata hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 93.4 kutokana na ujenzi wa barabara ya Dodoma-Manyoni-Singida yenye urefu wa kilometa 244 kuchelewa kukamilika.
Naibu Waziri wa Miundombinu, Ezekiah Chibulunje aliliambia Bunge jana kuwa kutokana na hasara hiyo, gharama za mradi huo sasa, zinatarajiwa kuongezeka kutoka kiasi hicho cha fedha kufikia Sh. bilioni 205.4.
Chibulunje alisema hasara nyingine iliyopatikana kutokana na kuchelewa kwa mradi huo, ni wananchi kuchelewa kupata huduma bora ya barabara mapema kama ilivyokusudiwa.
Kutokana na hali hiyo, alisema serikali iliamua kukatisha mkataba na mkandarasi aliyepewa zabuni hiyo kutokana na kuchelewesha ujenzi wa barabara hiyo.
Naibu Waziri huyo, alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Nzega (CCM), Lucas Selelii aliyetaka kujua sababu zilifanya ujenzi wa barabara hiyo kuchelewa, hasara zilizopatikana na lini mradi huo utakamilika.
Alisema kati ya fedha zilizokadiriwa upya kugharimu ujenzi huo, Sh. bilioni 144.613 zinatarajia kutumika kujenga barabara hiyo sehemu ya Dodoma-Manyoni na Sh. bilioni 60.669 Manyoni-Singida.
Chibulunje alisema mkandarasi anayejenga sehemu ya Mhala-Manyoni yenye urefu wa kilometa 17 ni Estim Construction Company Limited, ambaye anatarajia kukamilisha sehemu hiyo ifikapo Novemba, mwaka huu na yule wa sehemu ya Manyoni-Isunna (kilometa 54); kampuni ya China Geo Corporation (CGC), atakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ifikapo Desemba, mwakani. Hata hivyo, alisema hadi sasa jumla ya kilometa 173 za kiwango cha lami katika barabara hiyo zimejengwa na kukamilika.
CHANZO: NIPASHE