Serikali yaomba madaktari nje ya nchi, BILIONI 200 ZATENGWA KUWALIPA

ni wazi serikali imeshindwa kukubaliana na madaktari wake na sasa vyombo vya habari vinaripoti kuwa serikali ina mpango wa kuagiza madaktari 1000 kutoka Iran.kimsingi niseme madaktari hao hawatoshi na pia hawawezi kukidhi mahitaji wa madaktari bingwa tunaoambiwa nao wamegoma.

kama serikali ilikuwa na urafiki na Iran kwa muda mrefu na kila siku tunaambiwa hakuna madaktari wa kutosha iweje wasiitwe miaka yote hiyo hata kabla ya mgomo ili kuhakikisha afya zetu hasa maeneo ya vijijini ziko salama?

nakumbuka kwenye mgomo wa kwanza tulisikia wanajeshi kutoka lugalo walikwenda muhimbili lakini wauguzi na kada nyingine za afya waligoma kufanya nao kazi,sasa baada ya hao waIran kuja tuna uhakika gani kuwa watapewa ushirikiano na wauguzi wa kitanzania?

kama serikali inaona imeshindwa kutatua mgogoro huu ni vyema ikautangaza kama ni JANGA LA KITAIFA na hivyo tuombe msaada wa kimataifa.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
"Bei ya kuweka kiraka kwenye suruali inapozidi bei ya kununulia suruali mpya"

Hao madaktari watanunuliwa dawa na vitendea kazi vya kuwaduamia wagonjwa au wanakuja navyo wenyewe?

Na serikali watawaambia nini hao madaktari kuhusu wale wakina mama walio rundikana kwenye wodi kama kuku kwenye nchi ambayo haina vita?

Tuone hao madaktari kama hawajawaunga mkono madaktari wabongo kwenye mgomo baada kuona hali halisi ya hospitali zetu.
 
Hii serikali Sikivu sana ilikuwa wapi kuwaagiza madaktari hao muda mrefu .........tunabahati sana Tanzania yaani tunaletewa madaktari 1000 Bureeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hahahahaaaaaaaaa Pole Tanzania pole sana Tanzania Wavivu wa kufikiri
 
Kumbe wakishauriwa hawataki, kweli alichosema Mch Msigwa, sasa kuna kila dalili kuwa ukishagundua umepotea, utapotea zaidi. Ndicho kinachotokea kwa sasa. Wataalamu wa moto husema msitu unapoungua waweza kudhibiti kwa moto pia
 
habari za leo wazalendo wote Mliotayari kuchangia mawazo ya kuijenga jamii . mimi ni mgeni katika mtandao huu wa kijamii. lakini hiyo hainipi sababu ya kushindwa kugundua makosa yanyofanyika mbele ya macho yangu karibu na hisia zangu kwa usikivu wa masikio yangu . kwa kweli "two wrongs cant make it write" kwa hivyo sidhani kama tunaweza kupata suluhisho zuri kama pande zote zinazo pingana zina hasira. nashauri watu tutulie na tutumie busara zaidi. kila la kheri kwa aliye elewa ujumbe huu
 
Hivi si watalipwa kwa fedha zao za kigeni(USD)?Kama ndivyo vipi uchumi wetu dhidi ya fedha hizi za kigeni zitakazohitajika ktk soko?Dollar 1 haitafika buku tatu kweli?
Na kwenye lugha itakuwaje?,serikali itawaajiri na wakalimani?aaahh huku sasa ni kutumia fedha zetu vibaya na wananchi sie tumetuliaaaa Kama tunanyolewa!!!kweli nimeamini wananchi tunatawaliwa na watu(viongozi)
wachache.
 
Loooh...hii sasa ni ishara ya kwamba tunaelekea gizani...ivi mtoto au ndugu wa kigogo yeyote akiugua atatibiwa katika hospitali ambazo wananchi wa kawaida wanahaha kusubiri huduma?hayo mamilion ya kuwalipa madaktari wa kujitolea kwa nn wasingekaa chini kabla na ku zi allocate kwa madaktari japo kwa asilimia chache ya matakwa waliyoomba madaktari na serikali imeshindwa kuyatimiza?achilia mbali yale iliyotimiza.
 
"bei ya kuweka kiraka kwenye suruali inapozidi bei ya kununulia suruali mpya"

hao madaktari watanunuliwa dawa na vitendea kazi vya kuwaduamia wagonjwa au wanakuja navyo wenyewe?

Na serikali watawaambia nini hao madaktari kuhusu wale wakina mama walio rundikana kwenye wodi kama kuku kwenye nchi ambayo haina vita?

Tuone hao madaktari kama hawajawaunga mkono madaktari wabongo kwenye mgomo baada kuona hali halisi ya hospitali zetu.

serkali hii inaondeshwa bila kichwa ndio maana rais anaweza kutoa wazo la kuleta madr. Toka nje . Sasa wafanyakazi wote tugome ili tuone kama ataweza kufika hiyo 2015. Bila kutolewa taya kama walivyomfanyia umafiosso dr. Ulimboka
 
Na walimu pia Songea walitangaza mgogoro na serikali juzi. Labda wataleta na walimu kutoka nje.
 
Hii serikali mbofu mbofu kweli kweli wanatumia nini kufanya maamuzi yao.
Kama watoto watoto tu.
Ubabe ubabe tu wanamkomoa nani?
Baada yakutatua tatizo moja kwa moja wanataka kutengeneza mazingira ya tegemezi hata kwa kitu walicho nauwezo nacho.

Nata,

If this is true then theory ya Didas Masaburi kwamba CCM wanatumia Makalio kufikiria then ni sawa?

Madaktari sio sawa na madereva wa boda boda ambazo zimeingizwa nchini na mafisadi Askari wa CCm wakaanza kutoa Mafunzo vijiweni badala ya kuwataka waende Veta na Vyuoni kujifunza udereva. Matokeo yake wengi hawana leseni na it's now the leading killer on the roads.

Mugabe tried this rubbish thinking with nurses and todate the medical services in Zimbabwe are almost non existent.

Huo upuuzi wa kutumia private hospitals and the useless Lugalo ni ndoto ya mchana. Hizo private hospital costs wanalipa kwa kutumia pesa kutoka wapi. Serikali Dhaifu ikune kichwa wakae round table na Medics kutatua tatizo you cant look for a quick fix kwa tatizo la sekta ya Afya.

Kama alivyosema Msigwa. The level which caused this mess can't dissolve it we require another level that is ccm should rest In Peace. Tuchague serikali ya chama kingine na sio lazima CDM otherwise the Isidingo opera goes on and on.

Kwa taarifa ya CCM Madaktari duniani hawatioshi. With my vast travels all over the world I have never come across a jobless Doctor so be careful, think thrice before you take your stupid and silly CCM decisions using Masaburi . Just learn what they did in Kenya last year! Doctors are back in govt hospitals in Kenya of course they were paid though half a mile?

This is really a crazy preposition ukileta Madaktari kutoka nje utawakodishia Nyumba Upanga for a minimum of 1000 Usd per month Usafiri kwa sababu ni dharura ,bado mshahara and air tickets, labda wataifishe migodi ya Dhaifu aliyowapa bure wazungu.
 
sasa watawapa hao madaktari ajira za kudumu au watawachukua kwa muda ili wawatie uchungu madaktari wa ndani ya nchi? sisim bwana kazi kweilikweli.
 
Wa kwanza kulaumiwa ni sisi wananchi tumekuwa wajinga kweli,tunapiga kelele sana tatizo vitendo hamna.
akina mama na wazee ndio wanaotumaliza hawataki mabadiriko wamesahau kwamba hata wao walifanyiwa mabadiriko ukutazama wao ndio wanaonyanyasika kwa kiwango kikubwa lakini ukiwaambia wakati wa mabadiriko ni huu hawakubali hali hii itakuwa hv
 
Back
Top Bottom