Serikali yakubali kuilipa Rites Sh. Bilioni 30

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Hatimaye serikali imekubali kuilipa kampuni ya Rail India Technical and Economic Services Ltd (Rites) Sh. bilioni 30 sawa na dola za Kimarekani milioni 20. Serikali imekubali kuilipa Rites kiasi hicho cha fedha pamoja na kuwa Rites inashutumiwa kuiendesha Tanzania Railway Ltd (TRL) katika mazingira ya kutatanisha. Pamoja na kulipa kiasi hicho cha fedha kama gharama za mabehewa matano yenye umri wa miaka kama 50 hivi, serikali pia italipa gharama za usafiri kwa maafisa wote wa ngazi ya juu wa Rites ambao wamekuwa wakifanya kazi hapa nchini kwa miaka minne sasa.

Serikali imefikia uamuzi huu kutokana na majadiliano mazito juu ya kusimamisha mkataba ambapo Rites iliibuka mshindi. Kabla ya kufikia makubaliano hayo Rites iliipa serikali notisi ya siku 60 kwamba kama haitalipa dola za Kimarekani milioni 30.2 kama gharama za kukodisha mabehawa hayo, basi Rites ingevunja mkataba. Waziri kivuli wa Fedha na Mambo ya Uchumi Mh Zitto ameshauri fedha hizo zisilipwe mpaka CAG azifanye kazi na kuzitolea ripoti accounts za TRL.
 
shamba la bibi tena jamani,hivi hawa viongoz i wetu ni machizi?au wanakula ma**v&*
 
Kwa TIJA gani (wamechangia kuzalisha nini ndio tukawalipe hicho kiasi cha fedha) walioiletea taifa ndani ya huo muda wao mchache nchini???

Saed Kubenea na Mzee Mwanakijiji hebu katumulikieni hili.
 
shamba la bibi tena jamani,hivi hawa viongoz i wetu ni machizi?au wanakula ma**v&*

Hii issue ya TRL inanikumbusha ile ATCL (Air Tanzania Company Ltd) ilipoingia kwenye partnership na South African Airways investments. Tanzania ilijiondoa kwenye mkataba baada ya kundua the partnership was useless. Miaka michache tumerudia yale yale kwenye TRL
 
dah...hadi miaka hii mitano iishe...nadhani zitakuwa zimebaki mbavu tu mwilini mwangu,ni hasira :frusty::frusty::frusty:...we acha tu!!!
 
cna cha kusema ila naomba mungu wacje wakabinafsisha na nchi 2kakosa pakuishi kwani itakapofikia cku ya kuvunja mkataba 2tahitajika 2kawa2mikie walioingia mkataba mpaka fidia yao itimie ndio 2pate ardhi ye2. ee mungu waangaze hawa waache uozo huu.
 
Mgao wao sh. ngapi? Maana sio kweli zote ni za RITES
 
hivi wenye taaluma zenu,there is no way scientifically tunaweza ku-analyse mikataba tunayoingia na hizi crap na kujua kama it will work out ama vipi?mi nachoka,sina hata nguvu ya kushangaa.kiwira tulimlipa ben sh ngapi vile?
 
Hii issue ya TRL inanikumbusha ile ATCL (Air Tanzania Company Ltd) ilipoingia kwenye partnership na South African Airways investments. Tanzania ilijiondoa kwenye mkataba baada ya kundua the partnership was useless. Miaka michache tumerudia yale yale kwenye TRL

Kibaya zaidi no one will be held responsible on this one too. Ni kama hayo ya ATCL, Mabomu, EPA na madudu mengine ya kikwete hakuna kuwajibishana as result hata kabla hatujasahau utumbo wa mwisho mwingine tena unatokea. Mimi siilamu tena serikali bali watanzania wote kwa ujumla. Hivi tunasubiri hawa wajinga wafanye nini ndio tujue hawafai?
 
Back
Top Bottom