Serikali yaiokoa tena Reli

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,695
2,553
Serikali imeomba mkopo wa $ 83 karibia Tsh 98billioni kutoka serikali ya India ili kuinusuru kampuni ya TRL iliyopewa dhamana ya kundesha usafiri wa reli ya kati Tanzania bara , kampuni ambayo imekumbwa na matatizo ya kifedha baada ya kubinafsisha lililokuwa shirika la reli(TRC). (Tafsiri isiyokuwa rasmi kutoka THISDAY la Leo).

Hiki ni kielelezo tosha kwa kushindwa kwa PSRC na Serikali kuwasaidia watanzania kuondokana na matatizo waliyonayo kwa muda mrefu. Itakuwa vipi shirika liuzwe kwa kampuni ya briefcase ambayo siku chache baada ya kuuziwa shirika inakosa uwezo wa kuendesha shirika. Sitaki kuamini kwamba PSRC na Serikali walishindwa kutathmini uwezo wa kifedha wa kampuni kabla kukabidhi, kuna kila dalili ya kuonyesha kuwa watu wenye mikono michafu wamefanya vitu vyao hapa (Ufisadi).

Na inapokopa seriakali nani atalipa? kama sio sisi walipa kodi wakati Wahindi watakuwa wameshaamisha faida kwao, Pinda alikinga kifua mwanzoni mwa mwaka huu jamaa walikopeshwa na serikali zaidi ya Tsh 5bn kulipa mishahara sijui kama zimesharudishwa? leo serikali hiyo hiyo inataka kuingilia tena kukopa tena kunatofauti gani na ilipokuwa TRC. Hata kama serikali ina hisa bado haishiriki katika management ila katika kukopa wahindi wanaitaungiliza serikali huu ni ujinga lazima tuupinge kwa nguvu zote.

Wanapokuwa wawekezaji wazalendo je wanapata suport sawa na hii wanaopewa wahindi wa TRL? Haiwezekani jamaa wakute kila kitu halafu bado na pesa uwapatie wao kazi yao kuongoza siamini kama kuna watanzania wameshindwa kuongoza kama watapewa support kama ya hawa jamaa.

Ni wakati muafaka kwa serikali kukubali mashirika au kampuni zinazotaka kufa zife haraka kuliko kuziacha zichukue muda mrefu kufa wakati watanzania wataumia zaidi kama kampuni za namna hii zitakawia kufa, tazameni kesi ya Enron ilielekea kufa na ikafa haraka, jana kuna benki kubwa ya marekani imetangazwa mufilisi na hiatachukua muda utasikia mambo yamekwisha. Sasa bongo kampuni inaelekea kufa mnataka kuizuia isife kwa gharama za watanzania.

Vyovyote vile ni mtazamo wangu kutokana na habari iliyoandikwa na Thisday, wajumbe mjadala huko kwenu karibuni tunahitaji nondo za kiuchumi na biashara hapa, umbumbu wetu katika mambo haya unatugharimu.
 
Serikali yaiokoa tena Reli
Theopista Nsanzugwanko
Daily News; Thursday,September 18, 2008 @00:01

Serikali kwa mara nyingine imeokoa jahazi la Kampuni ya Reli (TRL) baada ya kuamua kuwalipa wafanyakazi wa kampuni hiyo malimbikizo ya Agosti na nyongeza kwa mwezi huu na hatimaye wafanyakazi kusitisha mgomo uliokuwa uanze leo nchi nzima.

Hatua ya serikali imekuja baada ya kuitishwa kikao cha wafanyakazi, Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu na uongozi wa kampuni hiyo na hatimaye serikali kuamua kuikopesha TRL fedha za kuwalipa wafanyakazi malimbikizo ya Agosti na nyongeza ya Septemba.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha wadau hao kilichofanyika Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Omari Chambo alisema serikali imechukua hatua ya dharura kuiwezesha TRL kulipa nyongeza ya mishahara kutoka Sh 160,000 hadi Sh 200,000.

Alisema nyongeza hiyo ni kwa Agosti na Septemba mwaka huu, fedha ambazo TRL itazirejesha ndani ya miezi mitatu ambapo watakuwa wamekamilisha taratibu za kupata vyanzo vingine vya mapato na kuanzia Oktoba mwaka huu, TRL itaendelea yenyewe kulipa mishahara hiyo.

“Kwa makubaliano hayo kati ya TRL na TRAWU, wafanyakazi wote wanaombwa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakati taratibu za malipo zinafanywa,” alisema Chambo bila kutaja kiasi cha fedha ambacho serikali imeikopesha kampuni hiyo.

Alisema kikao hicho kilichoshirikisha uongozi wa TRL, Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU) na Kampuni ya Kusimamia Mali za Shirika la Reli (RAHCO), ili kujadili namna ya kuyashughulikia madai ya wafanyakazi kuhusu nyongeza ya mshahara na malimbikizo yao baada ya makubaliano kati yao na menejimenti yaliyofanyika Machi mwaka huu.

Alisema makubaliano hayo ni wafanyakazi kulipwa kima cha chini cha Sh 200,000 kuanzia Agosti, jambo ambalo uongozi haukufanya hivyo na wafanyakazi kutoa notisi ya saa 48 kwa ajili ya kuanza mgomo leo. Alisema katika mazungumzo hayo, TRL walieleza kuwa hawana uwezo wa kifedha wa kulipa kiwango hicho kwa sasa, jambo lililoilazimu serikali kuingilia kati kwa mara ya pili baada ya Machi kuikopesha Sh bilioni 3.6 ili iwalipe wafanyakazi kima cha chini cha Sh 160,000 badala ya Sh 87,000 za awali.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake, Katibu Mkuu wa TRAWU, Silvester Rwegasira, alisema wamekubaliana na uamuzi huo uliofikiwa jana na sasa watalipwa kima cha chini cha Sh 200,000 na malimbikizo ya Agosti yatakayolipwa mwishoni mwa mwezi huu.

“Hakutakuwa na mgomo tena kesho (leo) na nikitoka hapa, nitaenda kuwajulisha wafanyakazi wote wa kampuni hii, lakini iwapo itafika mwishoni mwa mwezi huu na kampuni itashindwa kuwalipa wafanyakazi kama tulivyokubaliana, tutagoma bila kutoa notisi kama walivyofanya sasa,” alisema. Naye Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Narasim Jayaram, alisema amekubaliana na malipo hayo na watahakikisha wanarejesha fedha za serikali walizokopeshwa mapema kama walivyokubaliana.
 
Mbona hii serikali inafanya mambo ambayo haya,o katika mkataba wake na hii kampuni ya kihindi? Kama kampuni hiyo haina uwezo wa kuiendesha Reli yetu basi mkataba utenguliwe na mapema tusiendelee kuwalipa wahindi hao mabilioni ya pesa wakati hata kulipa mshahara wa wafanyakazi wao hawawezi.

Juzi tulisoma hapa kwamba wamenunua mabehewa mitumba toka India, sidhani mkataba huo uliwaruhusu wahindi hao kununua mabehewa ambayo yameshatumika, leo tena kwa mara nyingine tena tunaona serikali imewabebea mzigo wao kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi, je kulikoni? Je, kampuni hiyo imeshapewa 'mkopo' wa kiasi gani toka serikalini? Je, watakaporudisha pesa hizo watarudisha na riba au ni mkopo ambao hauna riba?

Kuna kila dalili ya Richmond nyingine, wahindi wanalipwa mabilioni ya pesa lakini hawafanyi chochote, Pinda na Kikwete mko wapi mtufafanulie nini kinaendelea ndani ya kampuni hiyo wa wahindi? Kampuni hiyo imeshaonyesha haina uwezo wowotev wa kuendesha TRC, kwa nini mnaendelea kuikumbatia? Je, kuna mikono wa mafisadi wanaokula ndani ya kampuni hiyo?
 
Tuliza boli mzee. Unaelewa maana ya public utility. Hizi ni huduma mabazo piga uwa ni za serekali yaani akipewa mtu binafsi anaweza kutmia nafasi hiyo kuwanyonya wananchi ni kama maji, umeme, reli . Serekali ni lazima iingilie ni mwiko kususa sawa.

Ninachosema kama hao wahindi hawana uwezo basi mkataba utenguliwe na serikali iendeshe TRC mpaka hapo atapopatikana 'mwekezaji' mwenye uwezo. Haiwezekani waendelee kulipwa mabilioni ya shilingi halafu wananunua mabehewa mitumba ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza faida yao na wakati huo huo hawana uwezo wa kuwalipa mishahara wafanyakazi wao.
 
Hiki ni kielelezo tosha kwa kushindwa kwa PSRC na Serikali kuwasaidia watanzania kuondokana na matatizo waliyonayo kwa muda mrefu. Itakuwa vipi shirika liuzwe kwa kampuni ya briefcase ambayo siku chache baada ya kuuziwa shirika inakosa uwezo wa kuendesha shirika. Sitaki kuamini kwamba PSRC na Serikali walishindwa kutathmini uwezo wa kifedha wa kampuni kabla kukabidhi, kuna kila dalili ya kuonyesha kuwa watu wenye mikono michafu wamefanya vitu vyao hapa (Ufisadi).

Na inapokopa seriakali nani atalipa? kama sio sisi walipa kodi wakati Wahindi watakuwa wameshaamisha faida kwao, Pinda alikinga kifua mwanzoni mwa mwaka huu jamaa walikopeshwa na serikali zaidi ya Tsh 5bn kulipa mishahara sijui kama zimesharudishwa? leo serikali hiyo hiyo inataka kuingilia tena kukopa tena kunatofauti gani na ilipokuwa TRC. Hata kama serikali ina hisa bado haishiriki katika management ila katika kukopa wahindi wanaitaungiliza serikali huu ni ujinga lazima tuupinge kwa nguvu zote.

Wanapokuwa wawekezaji wazalendo je wanapata suport sawa na hii wanaopewa wahindi wa TRL? Haiwezekani jamaa wakute kila kitu halafu bado na pesa uwapatie wao kazi yao kuongoza siamini kama kuna watanzania wameshindwa kuongoza kama watapewa support kama ya hawa jamaa.

Ni wakati muafaka kwa serikali kukubali mashirika au kampuni zinazotaka kufa zife haraka kuliko kuziacha zichukue muda mrefu kufa wakati watanzania wataumia zaidi kama kampuni za namna hii zitakawia kufa, tazameni kesi ya Enron ilielekea kufa na ikafa haraka, jana kuna benki kubwa ya marekani imetangazwa mufilisi na hiatachukua muda utasikia mambo yamekwisha. Sasa bongo kampuni inaelekea kufa mnataka kuizuia isife kwa gharama za watanzania.
 
Kama serikali inaweza saidia kwanini waliuza TRC?? si bora wangesaidia TRC ikanyanyuka na faida yote ikabaki hapa. Net group na City water wameondoka mambo yanaendelea.

Viongozi wa kiafrika wanasumbuliwa na ugonjwa gani mpaka washindwe kujiamini na kuamini watu wao. Mashirika waliyaua wenyewe kwa kuchagua watendaji wabovu na kuwakumbatia, mmeyauza wenyewe kwa fikra zenu fupi sasa mnawasaidia walionunua ili wapate faida bila hata ya kuwa na mtaji. Mbona wanao nunua mashirika sehemu nyingine duniani wanawekeza fedha? kunanini kwetu walete longolongo wapate fedha.
 
Serikali ituambie ukweli, nini kinaendelea kati yake na wawekezaji wababaishaji hawa wa TRL?Jamani mpaka wanalipiwa mishahara.
 
Sina shaka yeyote kwamba mkataba kati ya wahindi hawa wanaojiita wawekezaji ni wa kibabaishaji.Aidha wataalam wetu wamepewa rushwa au kwa umbumbu wao wameingizwa mkenge.Nadhani ni wakati muafaka kwa serikali yetu kuzinduka na kuchunguza kwa undani nini hasa kilitokea mpaka Wahindi hawa wakapewa mkataba wa kuiendesha TRL.Swala la serikali kuwalipia wawekezaji hawa uchwara mishahara ya wafanyakazi wao linanizunguusha sana akili.Mazingira haya yana mengi ya kujiuliza,lakini kuna nini hasa?
 
Date::9/18/2008
Uamuzi wa serikali kuikopesha kampuni ya TRL wapondwa
Na Kizitto Noya
Mwananchi

WAPINZANI wameponda uamuzi wa serikali kumkopesha mwekezaji wa kampuni ya TRL Sh350 milioni kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi wake na kuitaka imfukuze mwekezaji huyo kama hana uwezo wa kuliendesha Shirika hilo.

Wakizungumza na gazeti hili jana, viongozi wa vyama vya CUF, TLP, NCCR-Mageuzi na CHADEMA walisema uamuzi huo ni mbovu kwa kuwa ni aina nyingine ya ufisadi unaojitokeza katika matumizi mabaya ya fedha za umma.

Walisema kitendo hicho ni ufisadi kwa kuwa kinaonyesha uwezo mdogo wa mwekezaj huyo katika kuliendesha shirika na kutoa taswira kwamba mkataba wake uliingiwa kifisadi.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema ingawa ukiangalia kwa juu juu unaweza kuona serikali ina nia njema ya kuwasaidia wafanyakazi hao na kuzuia migomo, ukweli ni kwamba mkopo huo ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

"Hata kama serikali ilikuwa na nia hiyo kitu cha msingi ni Mkataba unasemaje? Je unaruhusu mwekezaji huyo kukopeshwa? na kwanini uruhusu kukopesha wakati mkataba huo umepatikana kwa zabuni?,"alihoji Mbatia.

Alisema kitendo cha Serikali kumkopesha mwekezaji huyo fedha za mishahara, kinazua utata na maswali mengi ikiwamo jamii sasa kutaka kufahamu namna mwekezaji huyo alivyoshinda zabuni hiyo.

"Maswali mengine ni: Hivi Serikali ilijua uwezo wa mwekezaji huyo kabla ya kumpa zabuni? Na huko mbele hatuoni giza nene kama lile la mikataba ya IPTL na Richmond?" aliendelea kuhoji.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF (bara) Wilfred Lwakatare alisema anaamini mkataba wa TRL una mkono wa ufisadi na ndio maana serikali haisiti kumkopesha fedha mwekezaji.

Alisema kitendo cha serikali kumkopesha mwekezaji huyo fedha za mishahara ya wafanyakazi wake kina utata hasa ikizingatiwa kuwa mkataba wa TRL uliingiwa kwa zabuni iliyoyashindanisha makampuni mengi.

"Inakuwaje mwekezaji aliyepata zabuni kwa kushindana na wenzake akose fedha hadi akopeshwe kama sio ushindi wake una walakini?" alihoji Lwakatare.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour, (TLP) Augustine Mrema alisema kuna kila dalili kwamba mkataba wa TRL ni wa bandia na una harufu ya rushwa.

Alisema hali inaonyesha kuwa mkabata huo sio halali na ndio maana hata mwekezaji huyo hajali kusema ameshindwa kuwalipa wafanyakazi wake akiamini kuwa serikali alioingia nayo mkataba huo itamsaidia.

"Mkataba huo ni bandia na kuendelea kutumia fedha za wananchi kumkopesha mwekezaji huyo ni aina nyingine ya ufisadi. Tunataka mkataba huo uchunguzwe ili TRL irejeshwe kwa wananchi kama mwekezaji huyo hana uwezo," alisema

Kauli ya Mrema imeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibrod Slaa aliyesema kuwa aina hiyo ya mikataba ndiyo inayoifilisi nchi.

Dk Slaa alisema inashangaza na ni utapeli wa waziwazi kuona mwekezaji aliyepewa zabuni kuzalisha, tena baada ya nchi kuona haina fedha ya kuendesha mradi, anaomba na kupata mkopo wa serikali.

"Huu ni utapeli na matumizi mabaya ya fedha za umma, kwa sababu kama tunaweza kulipa watu, kwa nini tulibinafsisha shirika?" alihoji.

Alisema kuna haja kwa serikali kumfanyia tathmini mwekezaji huyo ili kujua uwezo wake wa fedha na utalaam pamoja na kuchunguza mchakato mzima wote wa zabuni iliyompa ushindi mwekezaji huo ili kufanya maamuzi yatakayoleta tija kwa taifa.

Dk Slaa aliitaka serikali kuweka mikakati madhubuti wa kutafuta utashi wa maamuzi ya kisiasa akieleza kuwa ndilo tatizo pekee la nchi baada ya nchi kuwa na uwezo wa watalaam na fedha katika kuendesha miradi yake.


Naye Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) David Kafulila alisema kinachoonekana katika sakata la TRL na wafanyakazi wake kinaonesha kwamba ili mtu aweze kuekeza kuna sababu nyengine zadi ya mtaji.

Naye Salim Said anaripoti kuwa baadhi ya wasomi wa kitivo cha Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam wamesema uekezaji wa namna hiyo haufai na hauna tija kwa taifa kwa sababu hauendeshwi kiuchumi.

"Huyu ni mwekezaji alieshinda tenda ya kuekeza, sasa kama kila siku atakuwa anasaidiwa kutatua kero za wafanyakazi kuna tofauti gani na wawakezaji wa kizawa" alihoji Safari Baltazari.

Naye mchumi mwengine wa kitengo hicho kwa sharti la kutotaja jina lake alisema kinadharia wanaamini sana katika ubinafsishaji lakini kwa Tanzania tatizo lipo katika taratabu za kutoa tenda hizo.

Alifafanua kwa Serikali haiwajali wasomi wake katika kuingia mikataba mbalimbali jambo ambalo huipelekea kuingia hasara ya mabilioni ya shilingi.

"Serikali inaona tabu kumlipa msomi 50-100 milioni kufanya utafiti kuhusu mwekezaji kabla ya kuingia mkataba ili kuokoa hasara ya mabilioni ya shilingi" alilamika mchumi huyo.

Aleleza kwamba uamuzi wa serikali kumsaidia mwekezaji wa TRL kila mara ni sawa na mtu alienunua gari lake na kumpa dereva afanyie kazi kwa lengo la kuleta mapato na hatimaye anarudi kwa mwenye gari kuomba hela ya mafuta kila siku.

Naye Furaha Kijingo anaripoti kuwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaamu wamelaani kitendo cha serikali kumkopesha mwekezaji huyo fedha kwa ajili ya kuwalipa mishahara wafanyakazi wake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wakazi hao walisema kitendo hicho kinaashiria uwapo wa jambo ambalo limefichwa katika mkataba huo na serikali inahofia kumfukuza mwekezaji huyo kwa kuogopa kufichua siri ya jambo hilo.

"Sio siri lazima kuna jambo, ndio maana serikali inajifanya tunamkopesha kwani kama mtu hawezi kazi inatakiwa afukuzwe aletwe mwingine"alisema Ally Ndunguru mkazi wa Temeke.

Naye Hilal Mbelwa mkazi wa Tabata, alisema kama serikali ina uwezo wa kumkopesha mwekezaji fedha ili aweze kuendesha kampuni hiyo ni vema ikamfukuza na kuliendesha shirika hilo yenyewe.

Jana serikali, ambayo mapema mwaka huu ilikiri kutotekeleza jukumu lake katika mkataba na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), ilinusuru mgomo mwingine wa wafanyakazi wa shirika hilo wa kulikopesha fedha kwa ajili ya kulipa wafanyakazi kwae mishahara ya miezi miwili kwa kima cha chini cha shilingi 200,000.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi sita tangu Aprili 6 mwaka huu wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipotangaza kuikopesha kampuni hiyo Sh3.6 bilioni kwa ajili ya kuiwezesha kulipa nyongeza za mishahara.

Uamuzi wa serikali kuikopesha kampuni hiyo jana umekuja siku moja kabla ya wafanyakazi hao kuanza mgomo mwingine nchi nzima. Mgomo wa kwanza ulifanyika Machi 8 mwaka huu.
 
Date::9/18/2008
Uwekezaji wa aina hii hauna faida
Maoni na Uchambuzi
Mwananchi

UWEKEZAJI katika usafiri wa njia ya reli hapa nchini unaendelea kutia doa mchakato mzima wa dhamira ya serikali kuboresha huduma ya usafiri nchini, baada ya wafanyakazi na mwekezaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuingia tena katika mgogoro wa kimaslahi.

Mgogoro huo unatokana na menejimenti ya TRL kushindwa kutimiza ahadi zake kuwalipa wafanyakazi wake kima cha chini cha Sh200,000 kunzia mwezi Agosti, mwaka kama ilivyoahidi Machi, mwaka huu ulipotokea mgomo uliosababishwa na madai ya nyongeza ya mishahara.

Jumatatu wiki hii, wafanyakazi wa TRL wakiongozwa na chama chao, Trawu, waliipa menejimenti ya kampuni hiyo saa 48 kuwalipa tofauti ya mishahara yao kulingana na wavyoahidiwa vinginevyo wangeitisha mgomo wa nchi nzima mpaka hapo watakapolipwa haki zao.

Kutokana na unyeti wa suala hilo, serikali imelazimika kuingilia kati na kukubali kulipa mishahara ya miezi miwili kwa kima chini cha Sh200,000 na kwamba fedha hizo zinatolewa kama mkopo kwa kampuni hiyo. Hii ni mara ya pili kwa sekali kuikopesha TRL fedha baada ya kuikopesha kiasi cha Sh3.6 bilioni Aprili 6 mwaka huu kwa ajili ya kutatua matatizo ya mishahara baada ya wafanyakazi kugoma nchi nzima.

Kutokana na matatizo yanayoendelea kutokea katika kampuni hiyo, tunapata mashaka juu ya utaratibu mzima wa kumpata mwekeziji katika sekta hiyo muhimu kwa usafiri na uchumi wa nchi.

Haiwekezanai mwekezaji aliyetazamiwa kuboresha na kuendeleza usafiri wa reli nchini, kushindwa kutimiza malengo yake, ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Tunakumbuka wakati wa mchakato wa kumpata mwekezaji, wadau mbalimbali walikuwa na mashaka na mshindi wa zabuni hiyo kwa maelezo kwamba hawaamini kwamba ataboresha huduma hiyo, lakini serikali ikawahakikishia wananchi kwamba ana uwezo. Je, uwezo huo umetowekea wapi? Haiwezekani serikali kila wakati ibebe mzingo wa kumkopesha mwekezaji aliyetarajiwa kufufua huduma hiyo ambayo sasa inazidi kudorora.

Hata hivyo, kuna madai kuwa serikali ambayo inamiliki karibu nusu ya hisa katika kampuni hiyo, mpaka wakati mwekezaji anaanza kufanyakazi, ilikuwa hajatoa mgawo wake. Je, mambo hayo yana ukweli? Kama ni kweli, kwani haikufanya hivyo?

Pamoja na hayo, bado tunajiuliza kwamba, ilikuwaje serikali ilikubali kubinafsisha usafiri wa reli wakati duniani kote ndiyo nguvu ya usafiri na uchuni wa nchi?

Sehemu nyingi duniani usafiri wa reli ikiwa ni pamoja na miundombinu yake huwa chini ya serikali.

Lakini pia tunahoji kwamba, kama uwekezaji ni wa aina hii una faida gani kwa taifa? Kwa ujumla hali hii inaruhusu watu kuanza kujenga fikra kuwa kulikuwa na ufisadi katika mchakato huo.
 
Serikali hii haijambo kwa mazingaombwe. Sasa hapa wanamlinda(maslahi) mfanyakazi, au mwekezaji au bora liende?
 
Hii serikali hata haijifunzi kutokana na makosa yake ya nyuma. Baada ya mikataba ya IPTL, Songa na Richmond tungetegemea wawe makini sana katika mikataba iliyofuata ili wasirudia upumbavu waliofanya ambao umeliingiza Taifa hasara kubwa wa kuingia mikataba ambayo Watanzania tulikuwa tunalanguliwa kwa bei mbaya na makampuni yaliyopewa mikataba yalikuwa hayana uwezo wa kusimamia mikataba hiyo. Tungekuwa na uwezo tungefukuza serikali nzima kuanzia Kikwete na baraza lake la mawaziri lote. Haya makosa mnayoyafanya lini yatakoma? Ufisadi kila kukicha. kila mnachokifanya lazima kitawaliwe na ufisadi. Mnaipeleka nchi pabaya kwa uroho wenu.

TRL yaliza wapinzani

na Kulwa Karedia na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

HATUA ya serikali kuendelea kuinusuru Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi waliotaka kugoma, imeibua maswali huku baadhi ya wananchi wakitaka mkataba huo uchunguzwe.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alitaka mkataba huo upitiwe upya kwani kampuni hiyo imeonyesha kila dalili za utapeli.

Alisema lengo la serikali kulibinafsisha lililokuwa Shirika la Reli nchini (TRC), ilikuwa kuboresha huduma za usafiri pamoja na kuwalipa vizuri wafanyakazi wake.

Kwa sababu hiyo, Slaa alisema iwapo hata baada ya kulikodisha serikali ndiyo inayoendelea kulipa mishahara, hakuna sababu ya kuwa na mwekezaji huyo.

"Mkataba huo umeonyesha kila dalili za utapeli. Wawekezaji wameshindwa kuleta teknolojia mpya, wameshindwa kuwalipa wafanyakazi mishahara mipya, wameshindwa kila kitu na badala yake serikali ndiyo inayofanya kila kitu.

'‘Nafikiri tuamue kuuvunja mkataba huo au uchunguzwe tujue namna gani waliweza kupata zabuni hiyo wakati hawana uwezo," alisema Dk. Slaa.

Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, alisema anashangazwa na huruma ya serikali ya kuibeba kampuni hiyo ya wawekezaji, kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi kila mara, kwani kuna makundi mbalimbali, wakiwemo walimu wanaodai malimbikizo yao, lakini serikali imekuwa ngumu kulipa madeni hayo.

Profesa Baregu alisema umefika wakati wa serikali kuwaeleza wananchi mchakato wa kuipata kampuni hiyo ulikuwaje na kwa nini mazingira yake kiteundaji yanafanana na mkataba wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.

"Tuelezwe wakala aliyeipigia debe kampuni hii, maana haiingii akilini mwekezaji amekuja kuwekeza na mara mbili mfululizo, ashindwe kulipa mishahara ya wafanyakazi.

'‘Wananchi tuamke na tuhoji mkataba huu, kwani una kila dalili ya ufisadi. Kama anashindwa kulipa mishahara, ataweza kuiendesha kampuni? Ifike mahala tuangalie, kampuni inapaswa kuendelea kufanya kazi au la," alisema Profesa Baregu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema wananchi hawana imani kama fedha zinazotolewa na serikali zinaweza kurejeshwa kwa sababu hazijaidhinishwa na Bunge.

"Sasa kuna kila sababu ya serikali kutoa maelezo ni jinsi gani TRL inaweza kurejesha fedha hizi ambazo ni kodi za wavuja jasho wa Tanzania wakati hali ya kipato chao ni cha chini," alisema Profesa Lipumba.

Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha wapinzani kuipigia kelele serikali kwamba hawapaswi kukurupuka kumpa mtu au mwekezaji rasilimali muhimu ya taifa kama hii ya TRC, bila kufanya uchunguzi wa kina juu ya uwezo wake.

"Jinsi hali ilivyo, ni wazi tunaelekea kwenye matatizo makubwa, tofauti na ilivyokuwa mwanzo, haya ni mambo yaliyotokea Kenya na Uganda walipobinafsisha reli zao, sasa hali imekuwa ngumu mpaka serikali inatafuta wawekezaji wengine," alisema.

Naye Mwenyekiti wa Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alisema anashangazwa na uamuzi wa kumbeba mwekezaji huyo, wakati dalili zinaonyesha kuwa hana uwezo wa kujiendesha.

Mrema alisema mkataba wa TRL na serikali, hauna tija kwa taifa na kwamba ni bora shirika lingeendelea kuendeshwa na Watanzania wenyewe kuliko mwekezaji mbabaishaji.

"Serikali imebinafsisha mashirika kwa kigezo kwamba, Watanzania hatuwezi kuyaendesha, sasa kama hatuwezi kuyaendesha, mbona serikali imemleta mwekezaji huyo wa kigeni ambaye anashindwa kulipa hata mishahara ya wafanyakazi, kuleta mabehewa bora na kuboresha huduma za kampuni hiyo?" alihoji Mrema.

Alisema mkataba huo ni ufisadi mwingine na kuwataka wananchi kuanza kuupeleleza ni kina nani waliiwezesha kampuni hiyo kushinda zabuni na kuitahadharisha serikali kuacha tabia ya kuibeba kampuni hiyo, kwani kwa kufanya hivyo, inajidhalilisha mbele ya wananchi wake.

Akizungumzia mkataba huo, mkazi wa Mwenge, Jerome Steven, alihoji kwanini hadi sasa serikali haijauvunja mkataba huo kutokana na ubabaishaji iliokwishaonyeshwa.

Alisema serikali inapaswa kuueleza umma kwamba sh bilioni 3.6 ilizoikopesha TRL Machi mwaka huu, zilisharejeshwa, kwani ilitakiwa izilipe ndani ya miezi mitano.

Alipohojiwa na Tanzania Daima jana endapo serikali imeshatoa fedha hizo na kiasi ilichoahidi kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa miezi miwili, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kwanza alimjia juu mwandishi kwa kumuuliza swali hilo, lakini kama hiyo haitoshi, alikataa katakata kusema chochote kwa madai kuwa suala hilo halimhusu.

"Nasema huu siyo wakati wa kuniuliza suala hili, leo (jana) hapa tumekuja kuzungumzia masuala ya fedha za wafadhili kwa ajili ya bajeti yetu," alisema Mkulo.

Baada ya majibu hayo, Mkulo akiwa ameambatana na maafisa wake, aliamua kuondoka.

Juzi Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), kiliahirisha mgomo waliokuwa wameutangaza kuanza jana, baada ya serikali kuingilia kati na kuahidi kuwalipa malimbikizo ya fedha zao pamoja na mishahara mipya ya miezi miwili, kuanzia Agosti hadi Septemba mwaka huu.

Uamuzi huo wa serikali, ulitangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, baada ya kuongoza majadiliano kati ya menejimenti ya TRL, TRAWU na serikali.

Chambo alisema serikali imekubali kulipa mishahara ya wafanyakazi wote kima cha chini kutoka sh 160,00 hadi sh 200,000 kutoka Agosti hadi Septemba mwaka huu.

Alisema baada ya serikali kulipa malimbikizo hayo, TRL itaendelea kubeba mzigo wa kuwalipa wafanyakazi wake kama kawaida.

Machi mwaka huu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliingilia kati mzozo huo na kutangaza hatua ya serikali kuikopesha TRL sh bilioni 3.6 kwa kipindi cha miezi mitano.

Zaidi ya wafanyakazi 3,200 walitoa notisi ya saa 48 juzi kwa uongozi wa shirika hilo kuwalipa nyongeza za mishahara yao na malimbikizo mengine, vinginevyo wangeanza mgomo wa nchi nzima leo.
 
..hawa wahindi wa Reli inaelekea ni waganga njaa hawa, au matapeli.

..mbona sikuwahi kusikia mwekezaji pale Tanzania Breweries na Kiwanda cha sigara akiomba fedha serikalini?
 
Back
Top Bottom