Serikali yahaha kudhibiti wizi wa kimafia mtandaoni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
MIEZI michache baada ya kuripotiwa wizi wa fedha kupitia mtandao wa kompyuta kwenye benki tatu kubwa nchini, serikali inahaha kutafuta wataalamu wa kukabiliana na tatizo hilo.


Jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Florens Turuka alitoa wito kwa watalaamu bingwa wa mtandao wa kompyuta kusaidia kuanzishwa kwa Kituo cha Taifa cha Mfumo wa Mawasiliano ya dharura ya kompyuta (CERT).


Dk Turuka alitoa wito huo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wataalamu wa masuala ya mawasiliano kutoka ndani na nje ya nchi na wadau wa mawasiliano, ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).


"Mawasiliano ni muhimu kwa nchi hasa zile zenye uchumi dhaifu. Lakini usalama katika mfumo wa mawasiliano ni muhimu zaidi katika kutoa na kupata mawasiliano," alisema Dk Turuka na kuendelea.


"...Naipongeza TCRA kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa zikiwamo ile ya Wakala wa Usalama katika habari na mtandaoni (ENISA), Symantec, Forum for Incident Responce and Security Teams (First) na zingine."


Alisema "Tanzania kama mbia wa ushirika wa kimataifa wa kupambana na uhalifu wa mtandao (IMPACT), inakaribisha watalaamu watakaoiwezesha kuanzisha Kituo cha Taifa cha Mfumo wa Mawasiliano ya Dharura ya Kompyuta (CERT),"


Kauli hiyo ya serikali imetolewa katika kipindi ambacho tayari kumekuwa na taarifa za wizi wa takriban Sh300 bilioni, kwenye benki tatu kubwa nchini kupitia wizi wa mtandao.


Gazeti hili liliwahi kuripoti matukio hayo ambayo fedha zake zilitoroshwa kwenda nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani, huku tayari kukiwa na watuhumiwa zaidi ya watano wakiwa na kesi za wizi wa aina hiyo mahakamani.


Kwa mujibu wa habari hiyo, wizi huo mkubwa ulitikisa benki hizo baada ya watu wanasaodakiwa kuwa na mtandao mpana wa kihalifu hadi nje ya nchi kutorosha fedha hiyo kupitia mtandao wa kompyuta.


Hatua ya serikali kutafuta watalaamu wa kuanzisha CERT inakuja wakati wizi huo ukiwa umetikisa biashara ya fedha nchini na kuistua TRA jambo ambalo lilifanya makachero wa Tanzania washirikiane na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kusaka kiasi hicho cha fedha kilichochotwa.


Akitoa mada ya utekelezaji wa CERT katika nchi mbalimbali, uhalifu na usalama katika mawasiliano ya mtandao, Mtalaamu wa kompyuta, Sivanathan Subramanimu alisema uhalifu wa mtandao ni tatizo sugu duniani.


Subramanimu aliyehudhuria warsha hiyo akiwakilisha Ushirika wa Kimataifa wa Kupamabana na Uhalifu wa Mtandao (IMPACT) alisema mwaka 2006 nchi nyingi barani Ulaya, zilitikiswa na uhalifu huo uliofanywa kwenye benki mbalimbali.


Mwenyekiti wa Bodi ya CERT nchini Hangary Suba Ferenc alisema Mfumo wa Mawasiliano ya dharura ya kompyuta ni njia pekee ya kisasa inayoweza kukabiliana na uhalifu huo.


Ferenc alisema hayo alipokuwa akiwasilisha mada ya Usalama wa Mawasiliano ya Mtandao na Utekelezaji wa CERT kitaifa katika warsha hiyo ya kikanda.


Meneja wa Kituo cha Mawasiliano Tanzania (tzNIC) Abibu Ntahigiye alitaja uanzishwaji wa matumizi ya .tz kama utambulisho wa Tanzania kwenye ulimwengu wa mtandao.


Alisema .tz ilitolewa na Shirikisho la Mtandao Duniani linalojishughulisha na utoaji wa majina na namba za watumiaji wa mtandao (ICANN), mwezi Aprili 2010.


"Faida za kutumia .tz ni nyingi. Kwanza inakutambulisha kuwa wewe ni mzawa wa Tanzania, lakini pia ina nafasi nyingi ambazo wateja wanaweza kujipata ikilinganishwa na domain zingine," alisema


Akizungumza katika warsha hiyo, Peter Sarwatt kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Mamlaka hiyo (TCRA-CCC) alisema mteja ana haki ya kupata huduma, lakini pia ana wajibu kuhakikisha anatumia huduma hiyo kwa kazi iliyokusudiwa.


".Mteja ana haki ya kupata huduma, lakini pia ana wajibu wa kuhakikisha anaitumia huduma hiyo kwa kazi iliyokusudiwa,"
Chanzo Serikali yahaha kudhibiti wizi wa kimafia mtandaoni

Haya wataalam wa Computer isaidieni Serikali yetu haina wataalam wa Cputer inaibiwa ovyo ovyo kazi kweli tutafika jamani yuendako?
 
Back
Top Bottom