Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,172
Serikali yadaiwa sh bil. 7 na TTCL
na Bakari Kimwanga
SERIKALI pamoja na idara zake inadaiwa deni la sh bilioni 7.2 na shirika la simu la TTCL hali inayosababisha shirika hilo nchini kushindwa kujiendesha kiushindani zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Said Amiri Said, aliyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, ambaye alifanya ziara ya kiutendaji katika shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo wa TTCL alisema ili kuweza kujiendesha ni lazima serikali ilipe madeni inayodaiwa ikiwa ni pamoja na kulilipa shirika mtaji wa kujiendesha wa dola za Marekani milioni 230!
Said alisema hata kama kutakuwa na ugumu wa kupata fedha za mtaji, serikali itoe walau dola milioni 50, ili kuweza kuingia katika ushindani wa kibiashara na kampuni nyingine za simu za mkono.
Akizungumzia hilo, Profesa Mbarawa, alikiri serikali kufahamu changamoto zinazolikabili shirika hilo.
Lakini alisema kuwa serikali bado inaendelea na juhudi za kulipa madeni hayo ili kuweza kuleta ufanisi TTCL na idara zake.
Pamoja na changamoto hizo lakini kuwa na furahi kuona sasa tuna kitengo maalum cha kuendesha mkanga wa taifa wa mawasiliano sasa fanyeni kazi kwa kujituma na maarifa zaidi, alisema Profesa Mbarawa.
Akizungumzia lengo la ziara hiyo, alisema ni kujua changamoto zinazowakabili na kueleza mikakati mbalimbali ya serikali jinsi ilivyojipanga katika kuboresha huduma katika idara zake na kijamii.