Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Monday, 27 August 2012 | Ibrahim Yamola

SERIKALI inazifanyika kazi tuhuma 175 za kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zinazowahusu baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo na Wizara ya Nishati na Madini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema juzi Dar es Salaam kwamba tuhuma hizo ni zile zilizotolewa katika mkutano wa viongozi wa wizara hiyo na wafanyakazi wa Tanesco Mei 19, mwaka huu.

Maswi alisema katika tuhuma hizo zipo ambazo ni za ndani hivyo zinafanyiwa uchunguzi wa kina kabla ya kuchukua hatua.

"Watu wasiwe na wasiwasi juu ya kinachoendelea, lakini tunawaahidi kuwa watulie na kuna mambo mazuri yanakuja baada ya kumaliza kuzifanyia kazi," alisema Maswi na kuongeza: "Kuna vitu ambavyo vinaendelea ndani ya Tanesco ambavyo vinatakiwa kufanywa kwa uangalifu ili kuhakikisha hadhi ya shirika hilo inarejea."

Katika mkutano huo wa Mei, wafanyakazi wa Tanesco walimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo majina ya vigogo wa wizara yake wanaodaiwa kulihujumu shirika hilo.

Tukio hilo lilitokea wakati waziri huyo akiwa na manaibu wake, George Simbachawene na Steven Masele pamoja na Maswi, walipozungumza na wafanyakazi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Agizo la kukusanya majina hayo lilitolewa na Maswi muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya Shirika hilo, Abdul Mkama kutoa taarifa kwa niaba ya wafanyakazi iliyoeleza kuwa kuna vigogo katika wizara hiyo na wafanyakazi wengine wa Tanesco, wanaojihusisha na vitendo vya hujuma.

Katika mkutano huo, Mkama alisema Kamati yake ya Majadiliano inawafahamu kwa majina vigogo wa wizara hiyo wanaojihusisha na njama za kulihujumu shirika hilo kwa lengo la kuingiza wawekezaji wanaowataka katika sekta hiyo.

Miezi miwili baada ya tuhuma hizo, Bodi ya Tanesco ilimsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi William Mhando pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Nafasi ya Mhando imechukuliwa na Felchem Mramba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko na Usambazaji wa Tanesco.

Viongozi wengine wa Tanesco waliosimamishwa kazi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi, Harun Mattambo.
 
Katibu mkuu anatakiwa kuchapa kazi sio kuchapa domo! kazi hiyo amwachie Nape na Mnyika.
 
Ni mapema mno kusema lolote.Kuchunguza tuhuma na kuzithibitisha kisha kuzifanyia kazi ni mazoezi yanayohitaji umakini mkubwa.Tunasubiri tuone kitakachoendelea.
 
Nadhani sasa Maswi amekutana na Prof.Muhongo, wote ni wapenda misifa bila kutumia busara. Si Prof.Muhongo (a.k.a Mzee wa Gondwana) sio mchapa kazi la hasha bali ni kile kielement cha kupenda sifa ndo huwa kina mharibia....Sasa Maswi naye achape kazi kama mtendaji wa serikali na kufuata kanuni, taratibu na sheria za kazi kwa watumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom