Serikali yaanzia ARDHI UNIVERSITY kuajili wahadhili 'kisiasa'

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,166
Yaonekana Serikali hii inazidisha juhudi za kutoheshimu sheria au taratibu za utawala.

Kwa wale walioko Ardhi University (ARU) munafahamu vizuri tukio la hivi karibuni (baada ya lile la Prof. Baregu). Kuna muhadhili ameajiliwa kwa 'amri' ya utumishi badala ya Baraza la Chuo. Sikuweza kufahamu jina lake lakini ni taarifa rasmi ambayo nimeipata toka taarifa ya chama cha wanataaluma wa vyuo Vikuu wakionyesha kutoridhika na mtindo huu wa serikali.

Binafsi sijafahamu ni kwa nini jambo hili linazidi kujitokeza sasa hivi, ktk utawala huu uliowahi kuitwa wa 'ki-shikaji'. Ni ishara kwamba bila kuwa 'mshikaji' hupati nafasi au ajira ya maana. Sijui ni nani anaongoza Serikali! Nina wasi wasi baadaye hata U-profesa utapatikana kutoka utumishi.
 
Naona nimeshindwa kujieleza niliyoyaona.

Ni kwamba. Prof. Baregu aliponyimwa mkataba ilionekana Utumishi imeingilia ombi la Mkataba wake na kusema NO! Lakini kumbe mwenye madaraka ya kusema No/Yes ni Baraza la Chuo. Ni kawaida kwamba kila anayestaafu anaomba mkataba na kupewa na Baraza la chuo.

Mara hii hapo ARU kuna mtu yaonekana hakuhangaika kuomba Baraza la Chuo badala yake ajira yake imetoka tena Utumishi bila Baraza la chuo kufahamu kama sheria inavyotaka. Ndo malalamiko ya chama cha wana-taaluma.

Huyo muhadhili natafuta jina lake.
 
Mkuu aliyeajiriwa ni nani???? mbona taarifa yako haijakamilika? sisi tusio wa Ardhi tutajuaje? au thread hii umeanzisha kwa ajiri ya watu wa radhi?? halafu siyo WAHADHILI, ni WAHADHIRI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! tafuta habari kamili au funga thread
 
.....If you haven't made any research, you have no right to speak. Mambo mengine yanaletwa kiuzushizushi hivi!....
 
Yaonekana Serikali hii inazidisha juhudi za kutoheshimu sheria au taratibu za utawala.

Kwa wale walioko Ardhi University (ARU) munafahamu vizuri tukio la hivi karibuni (baada ya lile la Prof. Baregu). Kuna muhadhili ameajiliwa kwa 'amri' ya utumishi badala ya Baraza la Chuo. Sikuweza kufahamu jina lake lakini ni taarifa rasmi ambayo nimeipata toka taarifa ya chama cha wanataaluma wa vyuo Vikuu wakionyesha kutoridhika na mtindo huu wa serikali.

Binafsi sijafahamu ni kwa nini jambo hili linazidi kujitokeza sasa hivi, ktk utawala huu uliowahi kuitwa wa 'ki-shikaji'. Ni ishara kwamba bila kuwa 'mshikaji' hupati nafasi au ajira ya maana. Sijui ni nani anaongoza Serikali! Nina wasi wasi baadaye hata U-profesa utapatikana kutoka utumishi.

Kwanini iwe "kisiasa" na sio swala la maadili ya kazi, sheria za kazi, rushwa etc??? Name sawa but....Does everything have to have "siasa" behind it
 
Back
Top Bottom