Serikali yaamua kufunga uwanja mpya wa Taifa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,955
22,131
Serikali yataka kufunga uwanja mpya wa Taifa





Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Sosthenes Nyoni

WIZARA ya Habari, Utamaduni na Michezo imesema huenda ikalazimika kusimamisha matumizi ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi pale atakapopatika mzabuni wa kuuendesha.


Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Florens Turuka alisema kuwa uamuzi huo unaweza kufikiwa kutokana na serikali kutumia gharama kubwa za uendeshaji wake tofauti na mapato yanayoingia.


"Tunaweza kusimamisha kabisa matumizi ya Uwanja wa Taifa mpaka hapo mzabuni atakapopatikana, hii inatokana na serikali kutumia fedha nyingi za uendeshaji wake huku mapato yanayopatikana hayatoshelezi,"alisema.


Alisema kuwa wizara yake inashangazwa na mapato kidogo yanapopatikana uwanjani hapo licha ya mashabiki wengi kuonekana kuhudhuria mechi hali inayowapa wasiwasi kuwa huenda kuna namna fulani ya hujuma inayofanyika kwa manufaa ya watu wachache.


"Unajua kuona ripoti ya mahudhurio ya watu ikiwa juu halafu mapato yanayopatikana ni madogo, hilo linatupa wasiwasi labda kuna hujuma fulani inayofanyika na ndio maana tunataka apatikane mzabuni tutakayemkabidhi mamlaka ya kusimamia ili uwanja uwe ni kwa faida ya umma na si watu wachache,"alisema Dk Turuka.


Dk Turuka alisema kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni kumalizika kwa muda wa zabuni iliyotangazwa ili waweze kupitia majina ya waombaji na kuangalia sifa zinazotakiwa kabla ya kumtangaza aliyeshinda.


Katika hatua nyingine, DkTuruka alisema kuwa leo anatarajia kuutembelea uwanja huo ili kuangalia kama kuna kasoro yoyote ili ziweze kurekebishwa
 
Wampe Kingunge maana ndiye Fundi wa mambo haya mfano wake ni Ubungo naParking za mjini
 
Wampe Kingunge maana ndiye Fundi wa mambo haya mfano wake ni Ubungo naParking za mjini
Hizo ndio zetu,badala ya kutafuta utatuzi na kuboresha, wao wanatafuta njia ya kurithishana kimtindo.
Waipe CCM kama walivyofanya kwa viwanja vingine, si watasema hao sasa wana uzoefu wa kuendesha viwanja kwa ufanisi.
 
Hizo ndio zetu,badala ya kutafuta utatuzi na kuboresha, wao wanatafuta njia ya kurithishana kimtindo.
Waipe CCM kama walivyofanya kwa viwanja vingine, si watasema hao sasa wana uzoefu wa kuendesha viwanja kwa ufanisi.
Mkulu
This has nothing to do with kurithishana kimtindo.
Ili kuweza kusimamia ule uwanja,inahitajika PROPER MANAGEMENT, nje na ile ya serikali,provided atakayeshinda hiyo Zabuni, awe na UWEZO NA UZOEFU isiwe yale ya ........
 
Mkulu
This has nothing to do with kurithishana kimtindo.
Ili kuweza kusimamia ule uwanja,inahitajika PROPER MANAGEMENT, nje na ile ya serikali,provided atakayeshinda hiyo Zabuni, awe na UWEZO NA UZOEFU isiwe yale ya ........[/QUOTE]


Bonnie, hilo ndilo linalotafutwa hapo! Kwanza tunajitangaza kuwa tumeshindwa,kisha tunawapa tuwatakao, halafu ulaji kwa ulaini.... ndio Tanzania hiyo.
 
Najua wanafuata ushauri kuntu waliopewa na mkomunisti mjasiriamali KINGUNGE.
Nchi tamu hii we acha tu
 
Najua wanafuata ushauri kuntu waliopewa na mkomunisti mjasiriamali KINGUNGE.
Nchi tamu hii we acha tu

Akipewa Kingunge hata mapato atakuwa hatangazi yeye zaidi zaidi atakuwa anatangaza hasara kama Ubungo pale eti madaraja yanavunjika mabus yanakuja machache....pale itakuwa visingizio vya mvua na jua kali limewaka watu wameshindwa kuja.
 
Akipewa Kingunge hata mapato atakuwa hatangazi yeye zaidi zaidi atakuwa anatangaza hasara kama Ubungo pale eti madaraja yanavunjika mabus yanakuja machache....pale itakuwa visingizio vya mvua na jua kali limewaka watu wameshindwa kuja.

...hahaha
pata picha akianza kutoa malalamiko kuhusu ukusanyaji mapato pale kivukoni atasema tangu mbagala iwe daborodi wateja wa kivuko wamepungua sana.
 
...hahaha
pata picha akianza kutoa malalamiko kuhusu ukusanyaji mapato pale kivukoni atasema tangu mbagala iwe daborodi wateja wa kivuko wamepungua sana.

hahahaha vile vile Kigamboni kule toka serikali itangaze kuufanya sehemu kubwa ya kisasa kwa kuchukua maeneo wakazi wengi wamehama Kigamboni kwa hiyo Pantoni linaendeshwa kihasara zaidi...
 
kwi kwi kwi.
nchi hii tamu sana.
nakwambia hata Mwanakijiji wakimpa kipande cha mkate atagundua kuwa chumvi kwenye mboga ni tamu zaidi ya kuungia asali kwenye mboga
 
Serikali yataka kufunga uwanja mpya wa Taifa


"Tunaweza kusimamisha kabisa matumizi ya Uwanja wa Taifa mpaka hapo mzabuni atakapopatikana, hii inatokana na serikali kutumia fedha nyingi za uendeshaji wake huku mapato yanayopatikana hayatoshelezi,"alisema.

Sasa si wafanye Auditing wangalie hayo mapato yanaenda wapi. Serikali haitakiwi kabisa kutumia pesa nyingi kwa ajili ya uendeshaji. Uwanja unatakiwa ujiendeshe wenyewe.
 
Yale yale tu tuliyoyazoea bongo!Mtu anasema eti watu wanafurika lakini mapato ni kidogo, sasa watazamaji wanakuwa wameingia kwa kuruka ukuta?Ni wazi kuna kitu tu hapo, na si kingine, wanaowekwa mlangoni na wanaouza tiketi wanacheza michezo ya kifisadi! watanzania tutafika kweli kwa hali hii? Mzabuni, mzabuni, naye tunaweza kuweka mwekezaji (utasikia tu!), maana wazawa hatuaminiki..tumestaajabia ya Ubungo Bus Treminal, tungoje kuyaona ya Uwanja mpya wa Taifa!
 
Sisi sijui lini tutakuwa serious, Yana hakuna tunachoweza. Kila kona kuna UFISADI.
Na hakuna tutakachoweza kama bado tunaendelea kuwa na viongozi kizazi kipya kama NYALANDU (naona hata kumwita Mhe. naidhalilisha nafsi yangu) wanaoongea pumba mbele ya kamera ya television kuhusu kuulinda ufisadi bila hata aibu.
Seriousness itakuwepo tuu,pale tutakapofanya mapinduzi ya kweli kwa kuondoa uongozi huu goigoi,usio na uzalendo,uliojaa rushwa na mambo yote ya ovyoovyo. Na kuweka uongozi unaowajibika kwa Taifa na watu wake.
 
Wandugu,,

Hivi haiwezekani kama serikali ni mbia wa uwanja, basi ni yeye awe anatoa ticket za kuingilia? Haiwezekani hizi ticket zikawa zimeunganishwa kwenye computer za Wizara ya fedha? Au lingelifanyika geti linalozunguka na kila anayeingia, basi afanye scanning ticket yake na geti linazunguka. Pia wangeliweza kuweka camera zinazoonyesha watu wanavyoingia. Hata wageni Rasmi lazima watumiwe ticket na wakifika pale ziwe scanned na ionyeshwe ni wageni waalikwa wangapi? Wahudumu pia lazima wawe na card maalumu zitakazoonyesha wameingia na kutoka mara ngapi.....

Nafikiri hiii kazi hata kama JF wangelipewa basi wangeliifanya na kwa ghalama nafuu. Ila kamchezo siku zote ni kalekale. Wanaonyesha kuwa hamna mapato na dawa ni kutafuta mzabuni. Kama Tenga haleti pesa si apelekwe mahakamani na aonyeshwe how come watu wengi kiwanjani na mapato kidogo. Akisema hajui basi ina maana kashindwa kazi. Nafikiri hii wanakula wengi na ni ka mnyororo karefu sana na Kingunge kashapewa kazi tayari na sasa wanachoifanya ni kutafuta sababu za kumpa huu mradi. Uchaguzi huoo unaingia wandugu, pesa lazima zitafutwe.
 
Mi nakwambia
akishapewa mzabuni hiyo tenda basi mtaona kila wiki kinapigwa kipute cha kimataifa (kukusanya hela ya kampeni).
kazi ipo na sisi tupo macho tunaangalia kila kona
hakuna kulala
 
uwezekano huo wa kutengeneza mageti yanayozunguka na at least kufanya count on every entry, lakini nani atakubali kufanya hivyo wakati wanataka kupata mwanya wa kula pesa kilaini??? hata huyo katibu mkuu anasema tu kufurahisha wananchi walishapanga kumpa mtu lakini watawaambia nini wadanganyika kuwa wanampa mtu?? si kusema gharama ni kubwa ili wakae kimya??

NCHI HIII JAMANIIIIIII !!!!!!!??????
 
Waliamua kujenga uwanja wa mabilioni, lakini wakati huo huo wakasahau kutafakari nani atauendesha uwanja huo!!! :confused:
Kwanini serikali isiuendeshe uwanja huo na kutoza ada kwa yeyote anayetaka kutumia uwanja huo kama ni TFF, Yanga, Simba n.k.. Hivi Serikali kweli haiwezi kuendesha uwanja huo!? au ndiyo serikali ya kifisadi haiwezi kuendesha chochote!!! :(
 
Back
Top Bottom