Serikali yaamua kubana matumizi; Mbowe kashinda hoja

Hatimaye serikali imeafiki malalamiko ya kambi ya upinzani juu ya kupunguza kubana matumizi baada ya kupitishwa azimio katika baraza la mawaziri linalowataka mawaziri wote wanapoelekea bungeni kupanda mabasi maalum tu na si kila mmoja kuondoka na mkoko wake pia na maofisa wote na wakuu wa idara yote nao imeamuliwa kuwa watakuwa wanaenda bungeni kwa mabasi maalum maana wakati wa bajeti imegundulika karibu magari yote wizarani yamehamia dodoma!taarifa rasmi itatolewa na pinda mara atakaporejea bungeni. Source bbc

Kiini macho hicho haijawahi kutokea kwanza aanze kwa kupiga panga bajeti ya vx
 
Haya weee!!Ccm SIO RAHISI WAJIONDOEE ULAJI KAMA NI KWELI LAZIMA KUNA MLANGO MWINGINE WA ULAJI WAMEUBUNI.tUSUBIRI
 
Katika wakati kama huu wa kujivua magamba ni vizuri wakatuaambia sisi walipa kodi iwapo kiongozi atakiuka makubaliano ya kubana matumizi sisi wananchi tumfanye nini. Mfano kiongozi akizungusha li VX V8 wakati anatakiwa kupanda basi. Wasituambie wataunda tume kumchunguza. Ila hawa watu mimi siwaamini kabisa, kuna mahali watatuliza tu walipa kodi sisi
 
.."Serikali Corrupt ni Serikali ambayo haikusanyi Kodi, itabaki kukimbizana na Wafanyabiashara Ndogo Ndogo wa Mitaani, ili hali inatoa Misamaha Mikubwa ya Kodi kwa Wafanyabiashara Wakubwa" - Julius Nyerere
 
kikubwa mmeelewa?
kwa sababu nyie magamba ndio mnaongoza kwa kuwa mabingwa wa rivasi mkiongozwa na mtoto wa mkulima asiye na huruma kwa wakulima.
 
Sasa hiyo inahusiana nini na Mbowe? jamaa kwa kudandia, hamuwachi.

Faiza Foxy, mbona ni rahisi kuelewa? Mbowe kama kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kambi yake ndiyo iliyobuka na hoja hii. CCM wakabisha sasa kama ndivyo wanashinda. Nukta. Hata hivyo sina hakika na chanzo cha habari.
 
Huo usafiri maalum ni kitendawili kingine, haujaelezwa itakuwajekuwaje. Inatakiwa wapande public transport to Dodoma, then pale kuwe na shattle min-bus kwa vituo kadhaa kuwafikisha mahotelini na makwao ikizingatia ratiba maalamu ya vikao vya bunge. Mbona nchi nyingi zilizoendelea zinafanya hivi? Sisi tuna nini cha zaidi mpaka kubweteka na ufujaji huu.
 
Hatimaye serikali imeafiki malalamiko ya kambi ya upinzani juu ya kupunguza kubana matumizi baada ya kupitishwa azimio katika baraza la mawaziri linalowataka mawaziri wote wanapoelekea bungeni kupanda mabasi maalum tu na si kila mmoja kuondoka na mkoko wake pia na maofisa wote na wakuu wa idara yote nao imeamuliwa kuwa watakuwa wanaenda bungeni kwa mabasi maalum maana wakati wa bajeti imegundulika karibu magari yote wizarani yamehamia dodoma!taarifa rasmi itatolewa na pinda mara atakaporejea bungeni. Source bbc

Uamuzi huu unawaumiza wafanyakazi wa kada ya chini hususani madereva ambao nao walikuwa wakijiongezea kipato kutokana na posho za malazi wakiwa Dodoma. Hakuna matumizi ya mkubwa yatakayopungua.
 
Hata mimi kichwa cha habari kimenichanganya, maana sioni jinsi Mbowe anavyoingia hapa. Mwandishi wa thread hii angeeleweka vema kama angeandika " Serikali Yasalimu Amri".
lengo ni kuwateka wasomaji ili wasome hyo thread,watu wanapenda vichwa vya habari vyepesi.Ukiipa habari yako kichwa kigumu hata kama kina endana kwa % zote watu hawasomi au kucoment
 
Huo usafiri maalum ni kitendawili kingine, haujaelezwa itakuwajekuwaje. Inatakiwa wapande public transport to Dodoma, then pale kuwe na shattle min-bus kwa vituo kadhaa kuwafikisha mahotelini na makwao ikizingatia ratiba maalamu ya vikao vya bunge. Mbona nchi nyingi zilizoendelea zinafanya hivi? Sisi tuna nini cha zaidi mpaka kubweteka na ufujaji huu.

a UTARATIBU HUU NI MZURI SANA NCHI ZA WENZETU WENYE UCHUNGU NA PESA ZA WALIPA KODI HUWA WANAUFANYA. TRANSPORT INAYOTUMIKA NI MABASI MFANO TOYOTA COASTER MAYAI YENYE KIYOYOZI, VITI SAFI NA AT LEAST MAWAZIRI KUMI NA MIZIGO YAO MIDOGO NDANI YAKE. KUKIWA NA UGENI WA KITAIFA WA MARAISI WENGI PIA HUBEBWA KWENYE BASI MOJA FROM HOTEL TO UWANJA WA TAIFA. IMETOKEA JUZI JUZI HP TZ. SIONI KWA NINI ISIFANYIKE KWA MAWAZIRI WETU WAKIENDA DOM. TENA IMECHELEWA.
 
****** anaishi bure tu pale Ikulu halafu hatuoni mchango wake kama vipi awe kama mpangaji tu na yeye alipie tubane matumizi tumkate mshahara wake!
 
Mtoa mada unadhani Mbowe atakuwa amesaidia ku-save kiasi gani cha pesa? Magamba huwa ni wajanja sana, hiyo kwa mtazamo wangu haitoshi kabisaaaaaaaaaa......
 
Back
Top Bottom