Serikali yaagiza Pikipiki 400 maalum za Wagingwa

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
4321650.jpg

Waziri wa Afra na Ustawi Dkt Haji Mponda (aliye juu ya pikipiki) akizundua jana jijini Dar es salaam Pikipiki maalum iliyotengezwa na Kampuni ya E Ranger ya Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kubebea wagonjwa ili kudhibiti vifo vya mama na watoto. Pikipiki hizo kila moja imegharimu Dola za Kimarekani 5,900.


6074984.jpg

Mmoja wa madereva walipata mafunzo ya matumizi ya pikipiki maalum za kubebea wagonjwa akionyesha jana jijini Dar es salaam jinsi ya kumsafirisha mgonjwa kwa kutumia usafiri huo huku akiwa na muuguzi nyuma.

Serikali imeagiza pikipiki maalumu 400 kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali za rufaa, zahanati na vituo vya afya. Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii Dokta Hadji Mponda amesema katika awamu ya kwanza Serikali imenunua pikipiki 30 zenye thamani ya dola za kimarekani 177,000 ambapo Mkoa wa Pwani utapatiwa pikipiki 7, Morogoro 7, Rukwa 6, Mbeya 5 na Dodoma 5.

Waziri Hadji amesema lengo la kununua pikipiki hizo ni kutekeleza mpango mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi na watoto. "Serikali imejizatiti kufikia malengo ya Milenia ambayo yanalenga katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili na vifo vya kinamama vinavyotokana na uzazi kwa robo tatu ifikapo mwaka 2015"alisema na kufafanua kuwa, tafiti za mwaka 2009/10 zimeonyesha kuwa vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi ni akinamama 454 kwa kila vizazi hai laki moja kutoka vifo 578 kwa kila vizazi laki moja mwaka 2004/5.

Alizitaja sababu zinazochangia kwa vifo vya kina mama wajawazito ni pamoja na kutokwa kwa damu nyingi kabla na baada kujifungua, uzazi pingamizi, uambukizo na shinikizo la damu linalosababishwa na ujauzito na matatizo ya kuharibika kwa mimba. Sababu nyingine ni pamoja na ugonjwa wa Malaria, Ukosefu wa damu na maambukizo ya virusi vya UKIMWI, kuchelewa kufanya maamuzi katika ngazi ya familia ikiwa ni pamoja na kuchelewa katika kituo cha kutolea huduma.

Waziri Mponda alisema Serikali imeona kuwa ili kuendelea kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiwango kikubwa imeboresha muundo maalumu wa pikipiki ambao utawezesha kuboresha huduma katika maeneo mengi kwa mara moja.

Alisema kuwa pikipiki hizo zimeonyesha mafanikio makubwa katika nchi za Kenya, Malawi, Afrika Kusini, Sudan Kusini, Ethiopia na Guinea. Bibi Zuhura Ahmed Mkazi wa Dar es Salaam ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kusema kuwa itawasaidia kina mama wengi na hasa wa vijijini wanaokufa kwa kukosa usafiri wa uhakika. Aidha Serikali inatarajiwa kupokea pikipiki zingine 370 ifikapo mwezi nne mwaka huu kutoka kampuni ya eranger iliyopo nchini Afrika ya Kusini.

from: Srikali yaagiza pikipiki maalumu 400 za wagonjwa -
 
Sorry, title ni Serikali yaagiza Pikipiki 400 Maalum za Wagonjwa. Mods naomba mbadilishe.
 
He he ndio bajai za mama wajawazito hizo? Hivi zitawafuata huko vijikini au ?
 
Nilikuwa najiuliza hilo swali pia
 
Serikali inaongozwa na watu wapumbavu, Hizo pikipiki zipelekwe Magogoni ili wazijaribu kwanza kwa wake zao kama zinafaaa sio kuja kututolea wake zetu mimba au kutuharibia mimba za wake zetu.

Aliyekuja na akili za pikipiki kubeba wajawazito ni mpumbavu wa akili amedumaa akili, badala ya serikali kuagiza au kununua Ambulance wao kazi kuongeza matatizo na vifo vya watoto ambao hawajazaliwa. Go and take that Shit to Magogogni
 
Vipi vumbi njiani na mashimo, kwa hiyo wakati wa mvua pikipiki zinakuwa likizo, kweli serkali yetu inafikiria......
 
Pesa zilizotumika kununulia pikipiki hizi zingeweza kutumika kununua magari ambayo yangekuwa more comfortable, safe and efficient kwenye mazingira yetu kwa nyakati zote.

Serikali imekosea kufuata mawazo potofu ya kununua vitu kama pikipiki na power tillers kwa bei kubwa ambavyo haviwezi kuwa na ufanisi wowote zaidi ya kuwanufaisha watengenezaji na wauzaji.

Haitoshi tu kusema pikipiki zimeonyesha mafanikio katika nchi zingine bila kulinganisha kwa takwimu na matumizi ya vyombo vingine vya usafiri, kwa kuwa inawezekana hayo ni maelezo tu ya muuzaji katika kushawishi wateja.
 
Tanzania jamani ni nchi ya ajabu sana! sasa hapo nesi atakaa wapi kumsaidia mgonjwaa!!
 
Tanzania jamani ni nchi ya ajabu sana! sasa hapo nesi atakaa wapi kumsaidia mgonjwaa!!

Pa kukaa muuguzi hamna
pa kuweka drip na mambo ingine hamna..
Na pia kikubwa zaidi privacy hamna na hayo mashimo si kichanga kitachoropoka barabarani?
aibuu....
na hiyo bei ya 8,850,000 kwa moja inafanana kweli?
 
eeh mungu uwe na rehema na taznzania
lununua pikipiki kwa Dola za Kimarekani 5,900. badala ya kununua magari ya wagonjwa? huku ni kuongeza vifo vya mamawajawzito yote haya ten %
 
Huyu aliyeleta wazo hili kama ana amini kwalo, na niufumbuzi wa tatizo la wananchi wake ambao ni wagonjwa na atoe ushauri huu, hii bajaji itumike kwenye msafara wa rais maana yake tunaona siku hizi unakua na ambulace, so waitoe ile wa wake hii bajaji tuone kama hilo litawezekana.
 
Kuna mambo matatu muhimu ambayo yalipashwa kufanyiwa tathmini kabla ya hii decision ya kununua bajaji kwa waja wazito "ili kupunguza vifo vya akina mama na watoo. 1. Wakina mama na watoto wengi wanaopoteza maisha wakati wa kujifungua hutokea kwa wale ambao wameshaamua kujifungulia kwa traditional birth attendants.

Hawa tayari wameshafanya uamuzi wa kutojifungulia katika vituo vya afya. Kwao ujio wa bajaji hauna maana sana. Hata ungeleta ambulances. Suluhisho ni kutafuta na kutatua sababu zinazowafanya wafanye hayo maamuzi ya kutojifungulia katika vituo vya afya. 2. Vifo vingi vinatokea hospitalini kwa wale ambao tayari wameshafika hospitalini enen days after.

Suluhisho ni kuimarisha huduma ndani ya vituo na sio tatizo la transport. 3. Hizo bajaji hata kama zimefanya vyema katika nchi zingine, ingekuwa busara kuagiza kiasi fulani wakifanyie pilot study katika mazingira ya Tanzania kabla ya kuagiza lundo lote la bajaj 400.
 
Linaloonekana hapa mambo ya maadili sio kitu kinachoihusu sana serikali yetu. Ili baadhi ya watu waweze kufaidika na cha juu kitakachokatwa kwenye hilo deal,serikali imeamua kuagiza vyombo vya kuongeza vifo vya wagonjwa akina mama na watoto.

Tanzania ambulance zinazohitajika lazima ziwe off-roaders ukizingatia ubora wa barabara zetu. Na kama kweli kungekuwa na nia ya kutatua tatizo, hizi bajaji zote zingeenda mkoa mmoja, tuone utendaji.

TUKUBALIANE TU JAMANI TANZANIA HATUNA SERIKALI.
 
Back
Top Bottom