Serikali ya viwanda vs Kilimo kwanza

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Hivi ni kweli timekubaliana na sera hii huku kilimo bado kinachangia 1% kwenye pato la taifa? Tuna 80% ya ardhi ambayo inaweza kutumiwa kulima bila hata ya kuwepo kiwanda hata kimoja taifa likanyanyuka kiuchumi.

Viwanda ndio ni muhimu kua navyo tena vya kutosha lakini hebu hii 80% ya ardhi tumeifanyia nini? tumeridhika na 1% ya kipato kitokanacho na mali hii?
Niulize swali dogo tu; ARDHI NA VIWANDA KIPI NI MALI NZURI ZAIDI?

Sera ya kilimo haipo kabisa,haisikiki! Vijana wanaranda mijini, wanashindia mitandao ya kijamii kufanya timingi za ulaji huku 80% ya ardhi inazagaa!

Mchele,Unga wa mahindi,Sukari,Ngano,Maharagwe nk vyote bei ziko juu kwa sababu hakuna ubunifu katika sekta ya kilimo! Hakuna sababu ya msingi ni kwanini hizi bidhaa bei zake zinapaa ajabu.

Kwakua tumekubali kushindana na Dola ya marekani basi tutaendelea hivyohivyo, hakuna nchi dunia imeweza kupaa kwa kasi kama nchi ambayo uchumi wake unategemea kilimo lakini sisi tunakimbilia viwanda huku ardhi tunaiweka pending kwanza.Dah!

Hivi kwanini tusishupalie kilimo angalau tufikie hata 50% kwenye pato la taifa? Kwanini tusiweziweke Sera mbili sambamba yaani kilimo na Elimu wakati tunajiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye mapinduzi ya viwanda? Maana hata Umeme wetu bado ni wa kusuasua hivi viwanda titaendesha na nini?

Nafikiri juu ya hili siasa iwekwe pembeni,kama ni kubana matumizi basi salio lipelekwe kwenye kilimo?

Yaani ningekua Mimi ndie mkuu wa nchi ningeongeza udahili wa wataaalam wa kilimo na mifugo ikiwezekana na kuongeza idadi ya vyuo hasa wenye elimu ya kati yaani cheti na stashahada ili wasambae mpaka kwenye vitongoji, kitakachofuata ni kupanga mipango bora ya kilimo kwa ubunifu wa hali ya juu zaidi tuone kama hatujafikia tunakotaka! na hata viwanja baadae vingekuja nchi ikiwa katiza pumzi nzuri. Hizi million 50 kwa kila kijiji kwanini zisipelekwe kwenye miradi ya kilimo ikiwa ni pamoja na usambazaji wa pembejeo za kilimo za kutosha?
 
umeme wenye wa manati,halafu wanavyo imba viwanda utafikiri makinda ya ndege yanayo mwita mama yao awalishe!
 
Mijitu mingine ya ajabu sana, walikuwa wanadhihaki kilimo wakati wa Jk wakitaka viwanda leo yanajifanya kudhihaki suala la viwanda.

Ni wale wale walotuaminisha lowasa fisadi kwa miaka nane lkn leo wanatuhubiri kuwa lowasa mtakatifu.

Serikali ya Magufuli inakwenda na vyote viwanda na kilimo, wewe unafikiri kwanini milioni 50 zinakwenda kila kijiji kama si kwa ajili kilimo ambacho ndio shughuli inayofanywa na watanzania wengi. Au ndio kuwa mpinzani kilakitu kwako ni kupinga tu.
 
Unaweza kuonesha au kuthibitisha mahali popote ambapo kilimo kitakwenda sambamba na viwanda? Je, unaweza kithibitisha ni maeneo gani million 50 zimeelekezwa kwenye kilimo?
Vinginevyo unasumbuliwa na mihemko na huna hoja ni bora nikakupuuza.
 
Kilimo hakiwezi kututoa hapa tulipo ncha za sri lanka,Thailand,Malaysia waliachana na kilimo na kuhamia katika viwanda.Wakafanikiwa.Tanzania tunahitaji wakulima wakubwa sana wachache,siyo kila mtu kujiita mkulima halafu kilimo hicho hata chakula nyumbani hakimtoshelezi

Umeme wenyewe wa mgao...
 
umeme wenye wa manati,halafu wanavyo imba viwanda utafikiri makinda ya ndege yanayo mwita mama yao awalishe!
mwanzo mgumu ndugu, hapa inatakiwa kwa pamoja tujifunge mkanda na kupigania maendeleo ya taifa letu,, umeme usitufanye tukatishane tamaa wenyewe kwa wenyewe bali unatakiwa wewe kuwa mstali wa mbele kuipa moyo goverment yako na kutoa ushauli wa vipi tutaweza kuyatatua matatizo yetu, pia kwenye kilimo, jiulize wewe umelisaidiaje taifa lako katika hili, ''kwa umoja tutaijenga tanzania mpya;''
 
nani ujenge nae nchi?nyie muibe kura halafu mnidau uzalendo?kufeni kimpango wenu na muijenge kimpango wenu!
 
Mijitu mingine ya ajabu sana, walikuwa wanadhihaki kilimo wakati wa Jk wakitaka viwanda leo yanajifanya kudhihaki suala la viwanda.

Ni wale wale walotuaminisha lowasa fisadi kwa miaka nane lkn leo wanatuhubiri kuwa lowasa mtakatifu.

Serikali ya Magufuli inakwenda na vyote viwanda na kilimo, wewe unafikiri kwanini milioni 50 zinakwenda kila kijiji kama si kwa ajili kilimo ambacho ndio shughuli inayofanywa na watanzania wengi. Au ndio kuwa mpinzani kilakitu kwako ni kupinga tu.
na uvimbe na upasuke utajijua mwenyewe!
 
Mapinduzi ya kilimo ndio huleta viwanda. Hivyo tuwekeze kwenye mlo zaidi yaani kilimo kwanza, viwanda vitazaliwa vyenyewe tu.
 
mimi nipo willing kwenda kulima endapo nikipata guaranteed market ya mazao yangu kwa bei itakayolingana na risk na msoto uliopo kwenye kilimo,
ili soko liwe guaranteed serikali au watu binafsi wangeazisha viwanda vya kusindika mazao au basi kama wameshindwa watusaidie tu export nje
vinginevyo na chill tu hapa mjini nikifanya biashara za kutoa services ndani ya kiyoyozi

sio niende nikachafuke na tope halafu mazao yaniharibikie
 
nani ujenge nae nchi?nyie muibe kura halafu mnidau uzalendo?kufeni kimpango wenu na muijenge kimpango wenu!
mkuu iramba, kuchukia chama fulani kwa minajiri ya ubadhirifu wake na ikiwa ndio chama tawala hapa ni sawa na kumchukia baba yako mzazi unae ishi kwake. Tunachotakiwa sasa ni kuungana na serikari ya MH Magufuli katika ujenzi mpya wa uchumi wetu'
 
mbona daimond anamchukia babake,na life linasonga?unajua ni kwanini hana muda na babake!?we jenga nchi na huyo "baba" yako magufuli,sina muda na kushika vitu haramu
 
wala haina shida ya wewe kushika vitu haramu tena hata mimi pia, ILA WATOTO NA WAJUKUU ZETU NDIO WANAOHITAJIKA KUSHIKA NA KUFURAHIA VILE WATAKAVYO VIKUTA KUPITIA SISI, MAANA WAO HAWATOJUA KUWA NI HARAMU, BALI WATASEMA ''BABU IRAMBA AMETUFANYA TUISHI KATIKA NCHI NZURI KAMA HII'' '' na kama kunasheria ya kumuhukumu mzazi, basi tujuze ili iwekwe kwenye katiba''
 
Viwanda na kilimo vinakwenda sambamba.

Ukiwacha kimoja ukafanya kingine pekee utakuwa ni punguani wa hali ya juu.
 
Mijitu mingine ya ajabu sana, walikuwa wanadhihaki kilimo wakati wa Jk wakitaka viwanda leo yanajifanya kudhihaki suala la viwanda.

Ni wale wale walotuaminisha lowasa fisadi kwa miaka nane lkn leo wanatuhubiri kuwa lowasa mtakatifu.

Serikali ya Magufuli inakwenda na vyote viwanda na kilimo, wewe unafikiri kwanini milioni 50 zinakwenda kila kijiji kama si kwa ajili kilimo ambacho ndio shughuli inayofanywa na watanzania wengi. Au ndio kuwa mpinzani kilakitu kwako ni kupinga tu.
Hayo uliyoyaandika hayaendani na mwelekeo wa bajeti ambao Dr. Mpango aliusoma kwa wabunge dar. Hata hivyo, ule mwelekeo haukuliflect hotuba ya Rais aliyoitoa wakati anahutubia bunge-alisema kilimo ni kipaumbele lkn je kwenye mwelekeo umeonaje? Subiri pia bajeti tusikie kama ipo hvyo....
 
Mijitu mingine ya ajabu sana, walikuwa wanadhihaki kilimo wakati wa Jk wakitaka viwanda leo yanajifanya kudhihaki suala la viwanda.

Ni wale wale walotuaminisha lowasa fisadi kwa miaka nane lkn leo wanatuhubiri kuwa lowasa mtakatifu.

Serikali ya Magufuli inakwenda na vyote viwanda na kilimo, wewe unafikiri kwanini milioni 50 zinakwenda kila kijiji kama si kwa ajili kilimo ambacho ndio shughuli inayofanywa na watanzania wengi. Au ndio kuwa mpinzani kilakitu kwako ni kupinga tu.
Hebu tuambie any step forward iliyowahi kufanywa ili kuboresha kilimo katika awamu iliyopita ya miaka 10. Usanii na ufisadi tu.
 
Hahaha....KILIMO KWANZA AU UFISADI KWANZA?

Ni mapinduzi gani ya kilimo yaliyofanyika katika awamu iliyopita?

-Ni wakulima wa mkoa upi wanaoweza kuipongeza kwa mikono miwili sera ya Kilimo kwanza? USANII MTUPU.

Hili la viwanda bila reliable source of power ni sawa na kufungia maiti drip ili apate ahueni.

DAH..TANZANIA YANGU
 
Back
Top Bottom