Elections 2010 Serikali ya Uswisi imetangaza kutaifisha mali zote za Dikteta Hosni Mubarak

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Written by amini // 12/02/2011 // Habari // No comments

Serikali ya Uswisi imetangaza kutaifisha mali zote za Dikteta Hosni Mubarak,ambaye jioni hii ameng’olewa madarakani na nguvu ya umma.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa,haijafahamika iwapo serikali za Uingereza,Marekani na nchi nyingine za Magharibi ambako Mubarak ana mali zake (na kujichumia utajiri unaokadiriwa kufikiwa dola za Kimarekani Bilioni 70) nazo zitachukua hatua kama hiyo ya Uswisi au la.Je mafisadi wetu hapa nyumbani wanajifunza lolote katika sakata hili?
I just hope they do!kuna haja ya maloya kujitolea kufuatilia rasilimali za viongozi wetu kuwa ni safi au utapele wa mali ya umma?.
People power yangowa Mubarak
 
Inasemekana jamaa ana mabilioni katika bank accounts mbali mbali. Hawa viongozi wa Afrika wanaudhi kweli kweli. Wananchi wake walio wengi wanaishi maisha ya dhiki kubwa lakini yeye anaiba mali na kulimbikiza katika bank accounts nchi za nje. Jana pia ilionyeshwa nyumba ya mtoto wake UK. Inabidi mali zake zote ziorodheshwe ili ijulikane utajiri wake na kisha mali hizo zirudishwe kwa walipa kodi wa Misri.
 
Mkuu ni kweli kabisa Wamisri maisha ni magumu maana hata mishahara yao ni midogo mno. Ukisafiri kwa ndege kupitia Cairo andaa pesa za kumpa mtu wa check- in kaunta vinginevyo uwe na hand luggage tu ila kama una begi la kucheck-in halipakiwi kwenye ndege wanabaki nalo hapo japo wewe hawakwambii. Utafika unakokwenda huna begi.
 
Written by amini // 12/02/2011 // Habari // No comments

Serikali ya Uswisi imetangaza kutaifisha mali zote za Dikteta Hosni Mubarak,ambaye jioni hii ameng'olewa madarakani na nguvu ya umma.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa,haijafahamika iwapo serikali za Uingereza,Marekani na nchi nyingine za Magharibi ambako Mubarak ana mali zake (na kujichumia utajiri unaokadiriwa kufikiwa dola za Kimarekani Bilioni 70) nazo zitachukua hatua kama hiyo ya Uswisi au la.Je mafisadi wetu hapa nyumbani wanajifunza lolote katika sakata hili?
I just hope they do!kuna haja ya maloya kujitolea kufuatilia rasilimali za viongozi wetu kuwa ni safi au utapele wa mali ya umma?.
People power yangowa Mubarak

Hawa Waswisi wasisubiri mpaka mtu anatoka madarakani ndo wataifishe mali zake. Wanapaswa sasa kuwawekea ngumu viongozi wote wanaofungua akaunti huko na kujilimbikia mapesa ili hali wananchi wao wanaishi maisha ya shida. Halafu hizo pesa watazirudisha Misri zikajenge nchi au?
 
Na mafisadi wa TZ wenye vijisenti nje ya nchi hao waziblock ndio tutawaelewa vingine nchi zilizoendelea ndio wanafaidi na hela zilizoibwa Africa.
 
Swiss banks have agreed to give back to Nigeria more than half a billion dollars looted from the country by late dictator Sani Abacha and hidden in their vaults. The $535m tranche - $70m has already been sent back - forms part of a $1bn package being returned by a number of countries.

BBC News | BUSINESS | Switzerland gives back Abacha funds
 
Back
Top Bottom