Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi

This is just shameful! He corrupted them and I'm glad the "corruptor" of Africa is no more. He had an opportunity to make changes he clang to power for too long. We love Gaddafi more than his own gadamned people! Tushushe na bendera basi kwa siku saba kuomboleza!
Mzee Mwanakijiji, with due respect, kuishi kwenye nchi za watu kwa muda mrefu sio justification of thinking like them!. Naamini unakijua kilichomtoa Ghadafi na sio Western symphathy kwa watu wa Libya, I'm very sure you know better the games people play on us!.

Beggars kama Tanzania cannot be chooses, bendera tumezishushia mioyoni kwa kuwahofia mabwana zetu (UK, US na hao mabwana wa vita) wasije wakatushukia!.

Ndio maana nikacomment sijapenda Ghadafi alivyouwawa, so do Saddam na hata Osama!.
 
Pasco

My Take.
Kwanza nampongeza Waziri Membe kujitokeza waziwazi kuonyesha Tanzania kama nchi, tunamlilia Ghadafi.
Rafiki ni wakati wa dhiki, Membe alitakiwa hayo aliyoyasema leo kuhusu Ghadafi, angetakiwa ayasema pale Mabeberu na wale vibaraka wao, walipoanza chokochoko Libya.
Ningefurahi kama Membe na Tanzania, tungeonyesha kulaani uwamizi wa demokrasia ya Kiafrika inayoshambuliwa na wakoloni mamboleo na mabeberu wa ulaya wenye uchu na utajiri wa Afrika na kuwaondoa viongozi vikwazo kwa kisingizio cha kulinda demokrasia.
Kauli ya Membe kuwa Marehemu alikuwa mtu mzuri kwa Bara la Afrika, came 'too late' ila hata hivyo Tanzania imefanya uungwana wa kutoa kauli hii kwenye kifo hiki, ili angalau kuituliza 'karma' ya Ghadafi isitushukie Watanzania kwa ukosefu wa fadhila.

Binafsi, sijafurahishwa na kifo cha namna ile cha Ghadafi, vile ambavyo sikufurahishwa na kifo cha Osama, Saddam , Doe, ets. Kwa kifupi sipendi kabisa hata kuona tuu rangi ya damu ya binadamu!.

RIP Ghadafi!.

Hivi huo uzuri wa Gaddafi uko wapi?? Jamaa huyu si ndiyo alichanga na Fashist Idd Amin Dada kutuulia ndugu zetu kule Kagera??? Au unasema hatuna fadhira kwa vile nasikia ametujengea misikiti??? Iweje sisi tumpende kuliko watu wake?? Inakuwaje sisi tunajifanya tunamjua vizuri kiliko watu wake!!! The Guy just Engineered his own death period!!! The only thing he never though he will die that way. Aliwaita watu wake rats, sasa yeye walipomkamata kumbe alikuwa amejificha kwenye mtaro wa takataka.
 
Mkuu Nyambala, naomba nitofautiane na wewe kwenye seriousness ya Membe. Lets be honest, kwana anatofauti na Mkulu?.

Kwa vile Ben alitoka MFA akapanda ghorofani, then JK naye akatoka MFA na kupanda ghorofani, that means 2015 ni zamu ya Membe kupanda ghorofani kama watangulizi wake.

Kwani Tanzania tunahitaji serious leaders wa aina gani?. Mimi naombea sana CCM imsimamishe Membe. Ningekuwa active kwenye media ningetamani vyombo vyetu vya habari vifanye trend setting kwa kumseti Membe ali ampokee JK ili Tanzania tumpate kiongozi mwingine kama JK!
Membe go go go!

Ila binafsi nimefarijika na kauli ya Membe leo. kuutambua mchango wa Ghafi kwa Bara la Africa.

Pasco,
Membe is not a presidential material at all!

Kama unampenda kwa mapenzi binafsi, nadhani unaweza kwenda kunywa naye chai kama alivyopata kushauri baba wa taifa.

Raisi wa awamu ya tano atatoka kaskazini!
 
Huyu Mheshimiwa Membe alishaonyesha upande tangia awali kabisa na wengi (hata wale wasio watafiti wa mambo) wanajua ni kwa nini anafanya hivyo. Kwa hiyo ni lazima yeye binafsi na kundi lake wasikitike kwa kifo cha huyu bwana.
Kama kweli Membe anachukia mauaji, mbona hakutoa tamko lolote wananchi wa Arusha wasio hata na siraha walivyouwawa?
Anaitakaje serikali ya mpito kudumisha amani wakati walivyopandisha bendera nusu mlingoti aliwakemea, ni kwa nini asingeliwataka tangia wakati huo wamuonee huruma Ghadafi!?
Kama kweli Ghadafi alikuwa na nia ya kuunganisha Africa ni kwa nini hakushirikiana na wanamapinduzi wa mwanzoni (Nyerere, Nkrumah, Nesser, nk). Na si ndio huyo huyo aliyesema Nigeria igawanywe (tena juzijuzi tu)?
Nami naungana na Pasco kuwa binadamu wameumbwa ili kuishi na kifo cha asili kipo palepale kwa hiyo sio vizuri kabisa binadamu kumuua binadamu mwenzie ...lakini nchini mwangu Tanzania adhabu ya kifo HAIJAFUTWA! Tuwe wakweli!

Wanabodi,

Wenye access na TBC, angalieni live, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bennard Membe, ametoa msimamo wa Tanzania kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya, Col. Muammar Ghadafi.

Waziri Membe, ametoa msimamo huo leo asubuhi katika kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa moja kwa moja na TBC-1.

Waziri Membe amesema
  1. Tanzania haijafurahishwa na kifo hicho kwa vile Watanzania hatuna utamaduni wa kufurahia kifo chochote. Na kifo cha umwagaji damu ni kifo kibaya. (Japo Tanzania haijafurahia kifo hicho, ila pia haijalaanio mauaji hayo).
  2. Membe amesema, kwa vile Ghadafi ilikamatwa akiwa hai, huo ni uthibitisho kuwa aliuwawa mikononi mwa waliomkamata. Tanzania ingependa kuona Ghadafi akifikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kumtendea haki.
  3. Tanzania imeitaka serikali ya mpito ya Libya kudumisha amani na kuanza maandalizi ya kuunda serikali ya mpito kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  4. Pia amesema, Umoja wa Afrika, utatoa tamko lake leo, nalo halitakuwa tofauti na msimamo wa Tanzania, kutounga mkono mauaji ya Ghadafi ila nao utasisitiza kuundwa kwa serikali ya mpito na kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  5. Amesema hizo shamrashamra za kushangilia kifo cha Ghadafi zinazoonekana mitaani Libya ni short lived, kwa vile pamoja na mapungufu ya Ghadafi ya kutoruhusiu demokrasia, wanaompenda pia ni wengi kutokana na maendeleo makubwa aliyoiletea Libya hivyo isitegemewa maadam Ghadafi amekufa sasa ndio amani ya kudumu itapatikana Libya.
Waziri Membe, aliendelea kumsifia Ghadafi kwa michango yake kwa umoja wa Afrika na kueleza jinsi alivyotaka kuunganisha bara la Afrika kuunda United States of Africa ambapo alijenga makao makuu yake mjini Sirte, mahali alipozaliwa.

Membe pia alisifia maendeleo makubwa yaliyopigwa na Libya katika ujenzi wa nyumba za kisasa na miundo mbinu bora kabisa barani Afrika, na kueleza kuwa Tangu mwaka 2006, amekuwa akiwaalika viongozi wa Afrika kila mwaka kupiga kambi huko Sirte. (Naamini ni kula maraha).
.....
.....
Binafsi, sijafurahishwa na kifo cha namna ile cha Ghadafi, vile ambavyo sikufurahishwa na kifo cha Osama, Saddam , Doe, ets. Kwa kifupi sipendi kabisa hata kuona tuu rangi ya damu ya binadamu!.

RIP Ghadafi!.
 
Ukiwa kiongozi wa nchi,lazima uangalie maslahi ya nchi kwa kila kitu unachofanya.sasa membe anatetea maslahi gani? Wenye akili walisha soma alama za nyakati from the begining na kujiweka upande wa waasi kwa kuwa walijua gadafi hana siku nyingi angeangushwa.hizi porojo porojo za membe zinatusaidia nini? Unafikiri tunaweza ku trade chochote na serikali ya ntc kwa sasa? Use your commön sense membe,or who are u serving??
 
Sijakuelewa! Hakuwa sahihi kuwaambia kushusha bendera ama?

Membe hakuwa sahihi!

Wakti NTC wameshamng'oa Ghadaffi toka Tripoli na kusimamisha Bendera ya NTC,balozi wa Libya hapa Tanzania alishusha bendera ya iliyokuwa serikali ya Ghadaffi akaweka ile ya NTC. Membe alimjia juu balozi kuwa ashushe bendera ya waasi maana Tanzania bado haiwatambui waasi wa NTC! Nasikia yule balozi hakushusha bendera hiyo na alikuwa sahihi!

Ndiyo maana leo tunamwambia Membe aache unafiki! Yaani kwa vile Ghadafi keshakufa ndiyo sasa anajifaragua kuwatambua waasi wa NTC na bendera yao???!!!Membe is nothing but a mere hypocratic guy!
 
wewe umetumwa na membe kuanza kampeni. kama alishindwa hata kumshauri gaddaf ang'atuke, anasikitika nini.
Rais wetu 2015 atatoka upinzani, si upande wa magamba. I dipict would be SLAA WILBROAD Mwenye umri kama wa michael sata

Sawa anamfanyia kampeni ya kumwangusha na si kumpa uraisi, maana anasema JK na Membe ni watu wa uwezo unaofanana.
 
After all Membe is not far from what Gadafi has been doing. He is among them (CCM) . What would you expect him to say? His statement does not show any sign of real mourning ,rather a mockery of some kind. He is not confident any more , as the center is not holding any longer. Its a matter of time and he is worried that the time is too short .
 
Mzee Mwanakijiji, with due respect, kuishi kwenye nchi za watu kwa muda mrefu sio justification of thinking like them!. Naamini unakijua kilichomtoa Ghadafi na sio Western symphathy kwa watu wa Libya, I'm very sure you know better the games people play on us!.

Unayajua mawazo yangu kabla ya kuja kuishi nchi za watu? au labda wewe kutokuishi nchi za watu kunakufanya ufikirie unavyofikiria?
Beggars kama Tanzania cannot be chooses, bendera tumezishushia mioyoni kwa kuwahofia mabwana zetu (UK, US na hao mabwana wa vita) wasije wakatushukia!.

Tulikuwa maskini huko nyuma tuliweza kuwakatalia tulipoamini haki haitendeki. Tuliburuzwa kupinga China viti vya kudumu lakini msimamo wetu ulikuwa wazi hata kumkosesha Salim nafasi ya Ukatibu Mkuu wa UN! Tulivunja uhusiano na Uingereza na Ujerumani Mashariki. mara zote hizo tulikuwa maskini.. what changed?

Ndio maana nikacomment sijapenda Ghadafi alivyouwawa, so do Saddam na hata Osama!.

Hakuna mtu anayependa walivyouawa kama wasingetaka hayo yawakute wangeweza kufanya mambo tofauti; unafikiri Gaddafi alikuwa anainge Bengazi sawa na Sirte? kwanini wananchi wa Benghazi wamchukie hivyo? Kilichotokea leo ndicho kilichotokea kwenye French Revolution na ndicho kilichotokea kwenye American revolution. Viongozi wanapokataa kuwaskiliza wananchi wao na kufanya vigumu wao kubadilishwa wananchi wanabakia na nini mikononi mwao? Yote haya yangeweza kuepukika kabisa kama Gaddafi na Gaddafi pekee angefanya maamuzi tofauti hata mwaka mmoja uliopita! Hakufanya na sasa kalipa! Najisikia vibaya kuwa ili kumfikia Gaddafi wamepotea wananchi wengi sana wa Libya! Why didn't he just leave like Ben Ali au Hosni Mubarak?
 
Hivi huo uzuri wa Gaddafi uko wapi?? Jamaa huyu si ndiyo alichanga na Fashist Idd Amin Dada kutuulia ndugu zetu kule Kagera??? Au unasema hatuna fadhira kwa vile nasikia ametujengea misikiti??? Iweje sisi tumpende kuliko watu wake?? Inakuwaje sisi tunajifanya tunamjua vizuri kiliko watu wake!!! The Guy just Engineered his own death period!!! The only thing he never though he will die that way. Aliwaita watu wake rats, sasa yeye walipomkamata kumbe alikuwa amejificha kwenye mtaro wa takataka.

Gadafi alikuwa na imani kwamba walibya wengi wako upande wake ndo maana alikuwa anatoa kauli za kujiamini sana wakati uasi unaanza.

Bahati mbaya sana inaonekana walibya wengi hawakuwa upande wake. Kwa jinsi walivyojimwaga mitaani kusherekea kifo chake ni dhahiri kwamba walikuwa wamemchoka!
 
Membe alitegemea ufadhili toka kwa Gaddafi ili aikwae Magogoni Lodge!............nyoka wa mdimu huyu

"Unajua nyoka wa mdimu ana hila sana; anapenda kukaa kwenye mdimu, lakini hali ndimu, ila akija mtu anayetaka kuchuma ndimu humshambulia, sasa yeye kiwanda kinataka kujengwa Mchinga, lakini anakizuia," alisema Mudhihir
 
mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanajf, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'
huo ni mtazamo wako libya haikuwa huru kama ilivyo tanzania ya sasa.kifo cha gadaf ni mwanzo wa libya mpya yenye ustawi wa kweli
 
"Wenye access na TBC, angalieni live, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bennard Membe, ametoa msimamo wa Tanzania kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya, Col. Muammar Ghadafi."

Tamko gani hili, It is too late, wangemshauri vizuri kusepa mapema. Useless?
 
Wanabodi,

Wenye access na TBC, angalieni live, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bennard Membe, ametoa msimamo wa Tanzania kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya, Col. Muammar Ghadafi.

Waziri Membe, ametoa msimamo huo leo asubuhi katika kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa moja kwa moja na TBC-1.

Waziri Membe amesema
  1. Tanzania haijafurahishwa na kifo hicho kwa vile Watanzania hatuna utamaduni wa kufurahia kifo chochote. Na kifo cha umwagaji damu ni kifo kibaya. (Japo Tanzania haijafurahia kifo hicho, ila pia haijalaanio mauaji hayo).
  2. Membe amesema, kwa vile Ghadafi ilikamatwa akiwa hai, huo ni uthibitisho kuwa aliuwawa mikononi mwa waliomkamata. Tanzania ingependa kuona Ghadafi akifikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kumtendea haki.
  3. Tanzania imeitaka serikali ya mpito ya Libya kudumisha amani na kuanza maandalizi ya kuunda serikali ya mpito kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  4. Pia amesema, Umoja wa Afrika, utatoa tamko lake leo, nalo halitakuwa tofauti na msimamo wa Tanzania, kutounga mkono mauaji ya Ghadafi ila nao utasisitiza kuundwa kwa serikali ya mpito na kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  5. Amesema hizo shamrashamra za kushangilia kifo cha Ghadafi zinazoonekana mitaani Libya ni short lived, kwa vile pamoja na mapungufu ya Ghadafi ya kutoruhusiu demokrasia, wanaompenda pia ni wengi kutokana na maendeleo makubwa aliyoiletea Libya hivyo isitegemewa maadam Ghadafi amekufa sasa ndio amani ya kudumu itapatikana Libya.
Waziri Membe, aliendelea kumsifia Ghadafi kwa michango yake kwa umoja wa Afrika na kueleza jinsi alivyotaka kuunganisha bara la Afrika kuunda United States of Africa ambapo alijenga makao makuu yake mjini Sirte, mahali alipozaliwa.

Membe pia alisifia maendeleo makubwa yaliyopigwa na Libya katika ujenzi wa nyumba za kisasa na miundo mbinu bora kabisa barani Afrika, na kueleza kuwa Tangu mwaka 2006, amekuwa akiwaalika viongozi wa Afrika kila mwaka kupiga kambi huko Sirte. (Naamini ni kula maraha).

My Take.
Kwanza nampongeza Waziri Membe kujitokeza waziwazi kuonyesha Tanzania kama nchi, tunamlilia Ghadafi.
Rafiki ni wakati wa dhiki, Membe alitakiwa hayo aliyoyasema leo kuhusu Ghadafi, angetakiwa ayasema pale Mabeberu na wale vibaraka wao, walipoanza chokochoko Libya.
Ningefurahi kama Membe na Tanzania, tungeonyesha kulaani uwamizi wa demokrasia ya Kiafrika inayoshambuliwa na wakoloni mamboleo na mabeberu wa ulaya wenye uchu na utajiri wa Afrika na kuwaondoa viongozi vikwazo kwa kisingizio cha kulinda demokrasia.
Kauli ya Membe kuwa Marehemu alikuwa mtu mzuri kwa Bara la Afrika, came 'too late' ila hata hivyo Tanzania imefanya uungwana wa kutoa kauli hii kwenye kifo hiki, ili angalau kuituliza 'karma' ya Ghadafi isitushukie Watanzania kwa ukosefu wa fadhila.

Binafsi, sijafurahishwa na kifo cha namna ile cha Ghadafi, vile ambavyo sikufurahishwa na kifo cha Osama, Saddam , Doe, ets. Kwa kifupi sipendi kabisa hata kuona tuu rangi ya damu ya binadamu!.

RIP Ghadafi!.
Watu unaosema hukufurahishwa na vifo vyao na kuondoshwa kwao ebu jiulize wao waliuwa watu wangapi hasa Gaddafi??????????
Biblia inasema washikao upanga watauwawa kwa upanga, ukua watu tayari umeisha jilaani kufa pia kwa upanga!!!!!!!!!! Gaddafi aliona watu wake ni panya hivyo akaamaua kuwauwa, yeye pia amekuwa panya katolewa kwenye culavati!!!!!!!
 
personaly nilijikuta namchukia gadaff pindi yalipoanza maandamano hasa kwa namna alivyopambana na waandamanaji
 
Mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea Libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanaJF, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'

Ntakupinga kwa hili:
Tanzania kama nchi tumeshawahi kuparamia hizo sovereign states either directly(Uganda) or indirectly(Malawi,Zaire).....na hili liliongozwa na mtanzania makini kuliko wote ....Nyerere........ni suala la maslahi ya kinchi tu
 
Haya masikitiko ya Membe ni kwa ajili ya watu wa Libya waliolala barabarani wakisherehekea mwisho wa Ghadafi au kwa Ghadafi mwenyewe aliyeingia madarakani kwa mapinduzi na akaa kwa miaka 42? In his right mind Membe anaweza kutuambia kama aibu ya kuburuzwa kwa maiti ya Ghadafi was avoidable?

Africa nzima, hakuna la kujivunia kuona maiti ya Ghadafi ikiburuzwa barabarani, equally, hakuna la kujivunia kuona watu wa Benghazi wakitandikwa risasi na kuitwa 'rats'. All under the nose of AU!
 
Mkuu Nyambala, naomba nitofautiane na wewe kwenye seriousness ya Membe. Lets be honest, kwana anatofauti na Mkulu?.

Kwa vile Ben alitoka MFA akapanda ghorofani, then JK naye akatoka MFA na kupanda ghorofani, that means 2015 ni zamu ya Membe kupanda ghorofani kama watangulizi wake.

Kwani Tanzania tunahitaji serious leaders wa aina gani?. Mimi naombea sana CCM imsimamishe Membe. Ningekuwa active kwenye media ningetamani vyombo vyetu vya habari vifanye trend setting kwa kumseti Membe ali ampokee JK ili Tanzania tumpate kiongozi mwingine kama JK!
Membe go go go!

Ila binafsi nimefarijika na kauli ya Membe leo. kuutambua mchango wa Ghafi kwa Bara la Africa.

Ni yale yale masaburi tu. Mbona hamsifii gadafi alivyomsaidia idd amin kuivamia tanganyika?? Pumba
 
Back
Top Bottom