Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi

wa afrika tunatakiwa kujikomboa upya kutoka kwa mabeberu haya kama ambavyo walifanya mababu zetu, tulisoma kwenye historia na tukawasifu lakini sasa tunaitaji wajukuu zetu waje watusifu kama ambavyo sasa tunawasifu kina mkwawa, isiki, abushiri, kinjekitile na wanginewe, awa walichoshwa na ukoloni wakaamua kutumia mbinu zote walizoweza hatimaye wakoloni wakasalimu amri wakautoa uhuru, leo hii wamekuja na propaganda za kueneza demokrasia duniani, hawa ni waongo wakutupwa kabisa kama auamini hili jikumbushe wapalestina walivyofanya uchaguzi wao kwa amani na uhuru na kukichagua chama cha hamasi kuwaongozi wakaja juju na kuwaita magaidi ,hata kama magaidi sindio hao waliochaguliwa kwa demokrasia, au demokrasia gani waliokuwa wanaitaka, ivi inawezekana vipi watu wanabeba silaha alafu gadafi awaache eti tukaambiwa wanaandamana kwa amani ila gadafi anawauwa, ivi leo wanafunzi wa UD Washike silaha waandamane alafu serikali iwaachie eti demokrasia ni kweli tutakuwa na serilkali apo, KWA WALE AMBAO WALIKUWA AWAJUI NA WAKAAMINISHWA UONGO WA ALJAZEERA, CNN NA BBC eti libya wanamaisha ya taabu sana basi wakumbuke makala ambayo ilikuwa inarushwa na ITV karibu wiki nzima kabla ya uasi wa kijambazi ikionyesha libya ilivopata maendeleo na maisha yasivokuwa ghari kupita nchiu zote za mashariki ya kati na afrika kwa ujumla leo hii unawezaje kumwita gadafi dikteta, dikteta kwa kuwapa maisha mazuri watu wake, wazungu waliogopa hata pale mwanae gadafi alitangaza kuwa wapo tayari kufanya uchaguzi wa haraka kwa kujua kuwa gadafi angeshinda kwakuwa aliungwa mkona na asilimia 90% ya walibya

Polite man you are very unpolite!!! Kiongozi yeyote no matter how good he is akishakataliwa na only a quarter of his people, live alone half of them, you should raise your eyebrows! Gaddafi pamoja na mengi aliyofanya Libya, alilewa nadaraka na kujisahau. Angalia sehemu tu kati ya fedha alizowaibia Walibya zaidi ya U$ 200 bilioni, achilia mbali vitega uchumi vingine duniani. Angalia alivyowapoteza Walibya waliokuwa wakihoji utawala wake.

ushabiki wa kidini unakufanya usahau historia. To you he is tour hero, but for Libyans he is a dictator and deserved to die the way he died! Mtasema yote, mimi na wewe hatumjuwi Gaddafi kuliko Walibya wenyewe. Unadhani umati ule wa Walibya wanaoshangilia mitaani hawana akili? Siku zote mabaya kidogo hufuta mazuri mengi. Hivyo miaka 42 ya utawala wake alipaswa kusoma alama za nyakati, isingekuwa rahisi ku-resist nguvu ya umma - alijidanganya kama wafanyavyo watawala wetu wengi baada ya kulewa madaraka. Ni fundisho!

Binafsi machozi yalinitoka kuona kiongozi mkubwa, jasiri, tajiri mwenye nguvu akichomolewa kutoka kwenye culvet, akipigwa na kudhalilishwa na watoto wadogo, akivuja damu mwili wote....loh ni simanzi! Mbaya zaidi anaoza kwenye makabati ya kuhifadhia makabeji sokoni! hao ni ndugu zake Walibya wanampa treatment hiyo mtu aliyewapa maisha bora. Hujiulizi kwanini???? Watawala wetu wawe na kiasi vinginevyo tutaishia kusingizia nguvu ya NATO etc. Usiombe people's power haiongopi!
 
Nanyinyi mjiandae, na mlivyo vibonge sijui hata kama mteweza kupenya kwenye culverts km Gaddafi kwa jinsi mlivyo mabwanyenye kwa fedha za kifisadi. Nguvu ya umma nasisitiza, nguvu ya umma haizuiliwi kwa mizinga, magari ya washawasha wala mabom ya machozi.

Hahahahahaaaaa! Hivi nguvu ya umma ikitumika, wewe utakuwa wapi? Mimi sina kitambi, sijui wewe mwenzangu ama baba, mama na ankal wako!
 
In 42 years of his rule, Gaddafi was digging his own grave!

Gaddafi was a true son of Africa na daima atakumbukwa na historia ya ma-Panafricanists wa bara letu! Amekufa kishujaa, na nisingetegemea tofauti na aina ya kifo alichokipata kwa mtu wa aina ya Gaddafi...
 
Ukoloni mambo upi ambao haujaingia Tanzania ? Pinda na hekari 800,000 kaweka mkataba .Madini yetu na watu wanavyo uawa na hao unaowaona kwamba hawajafika .Au unaongelea nini mkuu ?Wachina wanapiga hata polisi .Mchina mmoja kufa hata Membe na mke wa rais wanafika kuomba msamaha wakati ni ujambazi wa kawaida .Ukoloni upi kaka unao ongelea wewe ?

hilo la kuomba msamaha kwa wachina ndo linapigia mstari ukoloni mambokesho!
 
Gaddafi was a true son of Africa na daima atakumbukwa na historia ya ma-Panafricanists wa bara letu! Amekufa kishujaa, na nisingetegemea tofauti na aina ya kifo alichokipata kwa mtu wa aina ya Gaddafi...

Habari za Nzega mkuu? Pole sana na dhahama ya polisi. Hao ndiyo polisi wa Tanzania mkuu.
 
Gaddafi was a true son of Africa na daima atakumbukwa na historia ya ma-Panafricanists wa bara letu! Amekufa kishujaa, na nisingetegemea tofauti na aina ya kifo alichokipata kwa mtu wa aina ya Gaddafi...
Kingwangala ndio maana watu hutilia shaka ufahamu wako , Gadaf hakuwa PanAfricanists, na wala hakuwahi, maana wakati hata wakupigania uhuru hakuwa na Waafrika wenzake.
soma vizuri historia ya Africa zama za ukombozi hakuwahi kusaidia hata mawazo alijikita kule Arab League akila arua na tende.
 
Seriously, cant believe what I am reading here!!!
 
Mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea Libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanaJF, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'

mH kIGWAGALA....

KUBEZA MAAMUZI WA WATU WALIBYA KUKATAA UDIKTETA NA KUCHAGUA KUWA NA DEMOKRASIA KUNAONYESHA UWEZO MDOGO ALIO NAO WAZIRI MEMBE KUHUSIANA NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA..........

SI VEMA KUMWAGA DAMU...TUSIKITIKE KWA HILO TU BASI...LAKINI TUSIJIFANYE KIMBELE MBELE KUPINGA KILE WATU WA LIBYA WAMEAMUA........

KUWA NA RAISI KAMA MEMBE NI HATARI SANA....ATALIINGIZA TAIFA VITANI MARA MBILI KWA MWAKA.....
 
Kingwangala ndio maana watu hutilia shaka ufahamu wako , Gadaf hakuwa PanAfricanists, na wala hakuwahi, maana wakati hata wakupigania uhuru hakuwa na Waafrika wenzake.
soma vizuri historia ya Africa zama za ukombozi hakuwahi kusaidia hata mawazo alijikita kule Arab League akila arua na tende.
Nguvumali, kuwa Pan Africanist sio lazima uwe ulipigania uhuru, Ghadafi ni true son of Africa na Pan Africanist kwenye kuing'oa neo colonialism ambayo ni mbaya kuliko hata colonialism yenyewe!.
 
Huyo Gaddafi kama kweli alikuwa anapendwa hivyo kama mnavyotaka tuamini, iweje Walibya washangilie kuuwawa kwake? Mtu apendwaye huliliwa bana!
 
Gaddafi was a true son of Africa na daima atakumbukwa na historia ya ma-Panafricanists wa bara letu! Amekufa kishujaa, na nisingetegemea tofauti na aina ya kifo alichokipata kwa mtu wa aina ya Gaddafi...
Asante Dr. Kingwa na pole kwa yaliyokukuta mikononi mwa polisi.

Kwa jinsi ninavyokusoma kule kwa wenzetu, na kama unayoyasema na unayoyatenda yanatoka moyoni mwako na sio for political gain, then naanza kukuamini kuwa ndani ya CCM, wako mashujaa wachache ambao mkisimama kidedea, imaweza kutegemewa kuleta mageuzi ya kweli from within hivyo nakuona kama na wewe ni shujaa fulani!.
 
Naloli,
Hili sii swla la silka ya binadamu, tunazungumzia sheria na UTU wa mwanadamu..Ghadaff ailikuwa na makosa yake na ndio maana kaondolewa madarakani. Kuondolewa kwake ni swala la Walibya kama lilivyo swala hili lakini kwa nini wewe unashangilia mahala ambapo sheria haikutumika maana kinachoweza kutuunganisha sisi na Walibya ktk swala hili ni kuzama sheria zinasema nini?
Hivyo kwa mtu yeyote anayekiuka sheria iwe Ghadaff au NTC hatuwezi kumuunga mkono tu kwa sababu hatumpendi mtu wa upande wa pili kama wanavyofanya Marekani na nchi za magharibi. Na afadhali wao wanafanya Urafiki na nchi hizi kwa maslahi yao wakati wewe na mimi urafiki wa maslahi hatuoni sababu..

Watu wengi hapa JF wametumia sababu ya Membe kumpenda Ghadaff ni kwa sababu ya misaada alotupa na interest zetu lakini wanashindwa kuelewa kwamba kama Ghadaff huyo huyo angeweza kukidhi interest za nchi za magharibi angeendelea kutawala kwa mika amingine na pengine hata kumwachia mwanaye kwani sii wa kwanza kufanya hivyo kinyume cha fikra tulopandikizwa..

Maneno yako ya kwamba ukiua kwa upanga nawe utauawa kwa upanga ni maneno mazito sana! na siodhani kama unayazungumza kwa kutumia sheria ama hisia zako lakini kama kweli unaamini aliyeua kwa Upanga anatakiwa kuuawa kwa upanga bila kufuata taratibu za kisheria, basi ya nini tunakuwa na mahakama? ya nini watu mnasomea sheria ili hali mwanadamu anaweza kufanya maamuzi haya pale inapompendeza...

SUALA la ukiua kwa Upanga nawa utauwawa kwa Upanga si la Naloli bali vitabu vya DINI vinalieleza hilo na WAHENGA wetu nao wanaliweka wazi hilo.
Pili Silka ya Binadamu haiongozwi na Sheria wala Dhana ya UTU wa binadamu, silka ubebwa na factors nyingi ikiwemo tabia, mazingira mtu aliyokulia, utamaduni wa jamii mtu iliyomzunguka nk na cha msingi silka inaendana na( Ego and Mind) mwanadamu husika, ndio maana kuna binadamu ufurahia maumivu au mateso ya mwenzake (SADIST) na mwingine yupo radhi kuteswa au kudharauliwa kwa ajiri ya kutetea wenzake au jamii yake mf. MANDELA. Sillka haiongozwi na sheria, kanuni au taratibu. NIMEWEKA WAZI KUWA SILKA YA UBINADAMU HAIKATAZI KUONYESHA HISIA PALE UNAPOFURAHI AU UNAPO HUZUNIKA. Ndio maana nikabainisha MEMBE au Serikali yetu si yakutuamulia wapi pa kufurahi na wapi pa kuhudhunika.

Ni wazi Gaddafi ana mazuri mengi na mabaya mengi pia Ndio maana nikasema Wlibya ndio wanaomjua vizuri GADAFFI na (si NATO, TZ, MEMBE,AU NALOLI) hivyo walibya wenyekufurahi nawafurahi wenye kuhuzunika na waudhunike. HATA wa wa TZ pia kumbuka kuna waTZ waliopigana vita vya kagera walikuwa mstari wa mbele na walishuhudia wenzao wakifa kwa risasi na mabomu yalilyonunuliwa na GADAFI pia walishuhudia askari wenzao wakiuwawa na askari wa GADAFI sasa MEMBE au Serikali haiwezi kumuamuru au kumtaka askari huyo auzunike kwa kuuwawa kwa GADAFI, ndio maana nikawa wazi tuongozwe na silka ya ubinadamu ktk hili yule ambaye zitamtaka afurahi na afurahi zitakazo mtaka auzunike na auzunike.

SUALA la NATO kuvunja sheria kumtoa GADAFI mbona lipo wazi, mbona viongozi wengi wametolewa kwa ubabe na kuvunjwa kwa sheria? SUALA HAPA NI HAO WAKINA MEMBE NA VIONGOZI WOTE WA AFRIKA wasilete sanaa katika suala la AU unafiki wa Afrika kupitia umoja wetu wa AU ndio unao tutesa na unaona viongozi wote wamegawanyika kila nchi inatoa vijitamko uchwara. KIFUPI VIONGOZI TULIO WACHAGUA BARANI AFRIKA NI WANAFIKI NA WASIO NA UCHUNGU NA LENGO LA KUIJENGA AFRIKA IMARA sasa NATO inatumia udhaifu wao kuwaadhibu, hivyo kuniambia niangalie sheria Kuwa zimekiukwa kumuondoa GADAFI hivyo niudhunike sikuelewi. GADAFI kaa madarakani miaka 42 kashindwa kuwashawishi wenzake waweze kuwa na UMOJA wa AFRIKA imara hivyo GADAFI awalaumu wenzake(yeye alijitahidi sana) na wakina MEMBE na viongozi wenzao ndio wajilaumu kwa kumtelekeza mwenzao hadi NTC na NATO wakamuangukia.
SISI waafrika tumewatuma viongozi wetu watekeleze mambo ya maana kwa nchi zetu na bala letu wao wanakalia UFISADI na kung'ang'ania MADARAKA na kujitengenezea HIMAYA za kifamle ktk nchi zao wakichokwa na kufurumshwa na wananchi wao kwa msaada wa NATO na MAREKENi au nchi za MAGHARIBI kama mnavyo ziita mnataka tuwe na HURUMA mbona wao hawaonyeshi HURUMA kwa sisi wananchi masikini? wanatufanya watumwa.watwana na viumbe dhalili. LEO wakitolewa wao wanataka sisi tuungane kupinga sasa tupinge nini? tupinge MABWANA zetu kufurushwa na MABWANA zao? VIONGOZI hawa wametufikisha mahali kila mtu anajiona anafaa kuongoza yaani waTZ tupo 40mil lakini kila mmoja akiangalia nchi iendavyo anaona hata yeye anaweza kuwa RAIS au kiongozi wa nchi, maana uongozi si ni UFISADI na kujijengea himaya na kulitumia jeshi na polisi kukulinda sasa nani anashindwa kuongoza?

KILICHOMPATA GADAFI anastahili hilo alimaanishi NATO na washirika wao wamemtoa GADAFI kwa kufuata sheria au kuzingatia UTU la, bali kilicho mkuta ndio STAHILI yake. ALICHUKUA UONGOZI kwa kufanya MAPINDUZI ya kijeshi na wamemng'oa kwa kupitia MAPINDUZI ya kijeshi. Je kauli ya WAHENGA/ MAANDIKO YA DINI ukiua kwa upanga utauwawa kwa upanga haijatimia?

Ni kweli inauma na kuudhunisha kuwa Waafrika tunanyanyaswa na kuendeshwa na MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE watakavyo hadi wanafikia kuwatoa viongozi wetu wa afrika kimabavu. Lakini cha kujiuliza je viongozi wetu wanaotolewa kimabavu wapo madarakani kihalali au kimabavu? Je chaguzi zetu ni za haki demokrasia inazingatiwa yaani viongozi tunao wachagua na kushinda ndio wanaotuongoza au viongozi wetu ni wale waliochakachua uchaguzi na kushinda kwa hila( wenyewe wanasema ushindi wa kishindo)? Je viongozi wetu wanawajibika kwetu au kwa Marekani na Washirika wake? SASA KAMA WANAWAJIBIKA KWA MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE BASI NI HAKI WAMAREKANI WAKIWATOA MAANA HAWA SI VIONGOZI WETU BALI NI VIONGOZI TULIOPEWA NA MAREKENI NA WASHIRIKA WAO HIVYO WANAHAKI YA KUWATOA.
Jiulize toka Rais wako achukue nchi hii 2005 hadi leo kafika mara ngapi mkoani,wilayani au kijijini kwako? angalia pia kafika mara ngapi MAREKANI na nchi za ulaya? Je gharama ni kuja kwenu au kuenda marekeni na ulaya? je anachotoka nacho huko kinawafikia mkoani,wilayani au kijijini kwenu? JIBU UTAPATA ZIARA HIZO NI ZA KUJIJENGA BINAFSI AU KUIJENGA NCHI YAKE.

UNABII HUU KAMWE HAUTOFUTIKA UKIUA KWA UPANGA UTAKUFA KWA UPANG
 
Wanabodi,

Wenye access na TBC, angalieni live, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bennard Membe, ametoa msimamo wa Tanzania kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya, Col. Muammar Ghadafi.

Waziri Membe, ametoa msimamo huo leo asubuhi katika kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa moja kwa moja na TBC-1.

Waziri Membe amesema
  1. Tanzania haijafurahishwa na kifo hicho kwa vile Watanzania hatuna utamaduni wa kufurahia kifo chochote. Na kifo cha umwagaji damu ni kifo kibaya. (Japo Tanzania haijafurahia kifo hicho, ila pia haijalaanio mauaji hayo).
  2. Membe amesema, kwa vile Ghadafi ilikamatwa akiwa hai, huo ni uthibitisho kuwa aliuwawa mikononi mwa waliomkamata. Tanzania ingependa kuona Ghadafi akifikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kumtendea haki.
  3. Tanzania imeitaka serikali ya mpito ya Libya kudumisha amani na kuanza maandalizi ya kuunda serikali ya mpito kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  4. Pia amesema, Umoja wa Afrika, utatoa tamko lake leo, nalo halitakuwa tofauti na msimamo wa Tanzania, kutounga mkono mauaji ya Ghadafi ila nao utasisitiza kuundwa kwa serikali ya mpito na kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  5. Amesema hizo shamrashamra za kushangilia kifo cha Ghadafi zinazoonekana mitaani Libya ni short lived, kwa vile pamoja na mapungufu ya Ghadafi ya kutoruhusiu demokrasia, wanaompenda pia ni wengi kutokana na maendeleo makubwa aliyoiletea Libya hivyo isitegemewa maadam Ghadafi amekufa sasa ndio amani ya kudumu itapatikana Libya.
Waziri Membe, aliendelea kumsifia Ghadafi kwa michango yake kwa umoja wa Afrika na kueleza jinsi alivyotaka kuunganisha bara la Afrika kuunda United States of Africa ambapo alijenga makao makuu yake mjini Sirte, mahali alipozaliwa.

Membe pia alisifia maendeleo makubwa yaliyopigwa na Libya katika ujenzi wa nyumba za kisasa na miundo mbinu bora kabisa barani Afrika, na kueleza kuwa Tangu mwaka 2006, amekuwa akiwaalika viongozi wa Afrika kila mwaka kupiga kambi huko Sirte. (Naamini ni kula maraha).

My Take.
Kwanza nampongeza Waziri Membe kujitokeza waziwazi kuonyesha Tanzania kama nchi, tunamlilia Ghadafi.
Rafiki ni wakati wa dhiki, Membe alitakiwa hayo aliyoyasema leo kuhusu Ghadafi, angetakiwa ayasema pale Mabeberu na wale vibaraka wao, walipoanza chokochoko Libya.
Ningefurahi kama Membe na Tanzania, tungeonyesha kulaani uwamizi wa demokrasia ya Kiafrika inayoshambuliwa na wakoloni mamboleo na mabeberu wa ulaya wenye uchu na utajiri wa Afrika na kuwaondoa viongozi vikwazo kwa kisingizio cha kulinda demokrasia.
Kauli ya Membe kuwa Marehemu alikuwa mtu mzuri kwa Bara la Afrika, came 'too late' ila hata hivyo Tanzania imefanya uungwana wa kutoa kauli hii kwenye kifo hiki, ili angalau kuituliza 'karma' ya Ghadafi isitushukie Watanzania kwa ukosefu wa fadhila.

Binafsi, sijafurahishwa na kifo cha namna ile cha Ghadafi, vile ambavyo sikufurahishwa na kifo cha Osama, Saddam , Doe, ets. Kwa kifupi sipendi kabisa hata kuona tuu rangi ya damu ya binadamu!.

RIP Ghadafi!.
Na fedha ghaddafy alizotoa kujengea kiwanda cha cement huko Lindi zipo wapi?
 
Pasco
hii ni thread yangu ya kumuaga Shujaa huyu Buriani Benard Membe, Umepigana Vita Vilivyo Vitakatifu, Mwendo Umeumaliza, Imani Umeitunza, Madeni Yako Yaliyobakia Karma Itakulipia!
P
 
Back
Top Bottom