Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi

Kwahiyo unasema hata TZ tuteke nchi kwa PICK UP?.Alikataa kuwatambua kwa kuzingatia sheria za kimataifa na si vinginevyo.Kitendo walichofanya waasi wa Libya si cha ubinadamu.Huwezi ukamuua kwa aibu hivyo kiongozi wenu.waarabu si watu waungwana hata kidogo.
umenena vema mkuu,wasubir kodi watakapo anza libya yao bila gadafi
 
My Africa, my leader, hata kama ulitaka Iddi Amini atuchape bado wewe uliamini katika uliyokuwa ukiyasimamia, tatizo lako kubwa hukuandaa democracy process baada ya mapinduzi, hata Mwl. JK angeng'ang'ania madaraka mpaka leo si haba mambo kama haya yangeweza kumtokea, ANGALIZO, walibya walikasirika sana na hasa wapinzani wake wakuu wa kule Benghazi baada ya kuona juhudi za kumpandikiza mtoto wako akurithi, ni mambo haya ambayo nasisi tunayasikia, mtu uliesoma nae, ukilaza wake ukawa unaujua halafu kwa mgongo wa baba yake mara unasikia ni muheshimiwa fulani na kesho waziri mara kawa rais ni kitu inayouma sana na ndo hapo watu huweka rehani uhai wao. Anyway RIP Gaddafi, ulikomaa na ndo maana wamekuua, sasa jamaa ni kujichotea mifuta na mara walibya wataanza kulipa bili za umeme. Do u guyz kno kwamba ukiacha afya hawa jamaa umeme na maji ni bure, ukioa unapewa kianzio cha karibu Mil 100, Mahindi mabichi unakula japo ni jangwani kwasababu jamaa alivuta maji toka mediterenian halafu akasambaza libya.
 
Gaddafi alikosea kama mwanadamu wa kawaida, ila kwa habari ya upendo kwa nchi yake na Afrika alitupenda sana, amesaidia sana kuweka umoja na mshikamano Afrika lakini juhudi zote za kuanzisha OAU baadaye AU na lengo ni kutaka kuhakikisha sisi wa Afrika tunajenga heshima kwa wazungu lakini alikuwa peke yake, sasa ni kama vile kauliwa baba wa Afrika, narudia tena alifanya makosa sikatai ila siku zote mti ulionyooka sana ndani ya msitu ndio hukatwa, Gaddafi kawindwa sana na wamefanikiwa NATO, sasa ngoja tuone jinsi uchum i wa Libya unavyoporomoka na yule Dogo aliyeshangilia na kuonyeshwa akiwa na furaha eti yeye ndiye kamuua Gaddafi ana kazi ya ziada damu itamfuata yeye mwenyewe atajuta alichokifanya,. Gaddafi ni kiongozi aliyefanya mazuri na mabaya ila wameona mabaya kwa jicho la ubaya. RIP Gaddafi msalimie Nyerere
 
Mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea Libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanaJF, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'
Siongelei kuuawa kwa huyu mtu. Lakini naomba nikuulize sovereign state kwa faida ya nani? watawala au raia? Mnataka mkiua kama polisi wenu walivyoua huko Nyamongo msiulizwe na yeyote kutoka nje kwa upuuzi huo wa sovereign state siyo?! Mkidhulumu mashamba kama Mbalali na kwingineko Dunia ikae kimya. Hivi ni nani anayewatetea wanyonge ktk mataifa yetu? Siku wabongo watakapokataa kwa nguvu hizo sovereignty zenu za walafi na wezi pekee mtaitafutia hiyo sovereign state yenu kwenye mashimo kama fuko msiione...Wanyonge wanapodhulimiwa hamjali lkn ulaji wenu ukiguswa mnakuja na misemo yenu ya kinafiki...
 
Kwahiyo unasema hata TZ tuteke nchi kwa PICK UP?.Alikataa kuwatambua kwa kuzingatia sheria za kimataifa na si vinginevyo.Kitendo walichofanya waasi wa Libya si cha ubinadamu.Huwezi ukamuua kwa aibu hivyo kiongozi wenu.waarabu si watu waungwana hata kidogo.

Membe alikuwa anapoteza muda kutowatambua waasi wakati maboss wake (NATO Members) wamewatambua waasi looong time. The whole issue against Gaddafi regime was awkward mana NATO walivunja utaratibu kwa makusudi kusaidia waasi, kwa hilo tu Membe kama mwanadiplomasia ilitakiwa aweameshasoma upepo wa maboss wake
 
Mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea Libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanaJF, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'
Nanyinyi mjiandae, na mlivyo vibonge sijui hata kama mteweza kupenya kwenye culverts km Gaddafi kwa jinsi mlivyo mabwanyenye kwa fedha za kifisadi. Nguvu ya umma nasisitiza, nguvu ya umma haizuiliwi kwa mizinga, magari ya washawasha wala mabom ya machozi.
 
Sijui ni wangapi humu wangependa Gaddafi awe rais wao... na kama wapo kwanini hawakuwa na ujasiri wa kuishinikiza serikali ya Tanzania kumpa hifadhi Tanzania kama wengine tulivyowashauri? Wangempa na uraia kabisa ili aweze kugombea Urais wa Tanzania halafu wote tuongozwe na Kitabu cha Kijani...
 
Mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea Libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanaJF, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'

Ya Libya yamekuuma sana, lakini ya Arusha, North Mara na mengineyo nchini hukuonyesha dalili za kusikitikia, tukueleweje Mbunge wetu kama una uchungu na nchi pamoja na wananchi wake?

:focus: Charity begins at home :canada:​
 
wanafiki wakubwa hao yn wasubiri apigwe hadi auwawe hlf wajidai wanamlilia, UNAFIKI KM HUO MUNGU HAPENDI. NA ZAMU YA HY M.K.WERE INAKUJA si anajidai kupimapima mafuta ngoja aanze kuyachima rasmi aone kitu atafanywa.
 
jamani mkileta habari hapa jamvini semeni basi habari ikoje, siyo unaripoti tukio then huleti content ya habari yenyewe
 
jamani mkileta habari hapa jamvini semeni basi habari ikoje, siyo unaripoti tukio then huleti content ya habari yenyewe

"Wenye access na TBC, angalieni live, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bennard Membe, ametoa msimamo wa Tanzania kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya, Col. Muammar Ghadafi."
 
Mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea Libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanaJF, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'

Arusha, Igunga(karibu na kwako), Migodini, Maji Ya Sumu, Malaria, Njaa Ngorongoro Na Mengine Mengi Wewe Hukuona Kama Ni Vifo?? Lakini Leo Ya Libya Yanakusikitisha? Unasikitika Ili Watz Wasiige Kutoka Huko, usiogope hauna haja ya kuongea huku JF, fanya kazi yako kama mbunge vizuri na daima hautasikia wananchi wako wakikuandama, zaidi watakulinda.

Tofauti Yetu Sisi na nyie ni, Sisi wananchi tunawindwa kama Wanyama Pori, Wakati Nyie Mnalindwa.

R.I.P Ghaddafi
 
Back
Top Bottom