Serikali ya Tanzania ni nani? Mtu avyosema kwa manufaa ya uma ana maana gani?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,542
8,630
Watanzania wengi wameshafikia wakati wa kupelekwa kama watoto wadogo na "serikali". Nimeshangazwa na utaratibu wa wananchi kuchukuliwa mashamba, viwanja na kupewa wawekezaji. Ukiuliza ni nani kachukua unaambiwa ni serikali na ukiuliza ni kwa nini unaambiwa kwa manufaa ya umma.

Tuanze na serikali: Je serikali ni nani? je ni mawaziri na wafanyakazi walio Dar ambao wanajua kila kitu? au serikali ni watu?. Kama serikali ni watu basi ingeushisha wanakijiji na wakazi wa hayo maeneo na kuwaacha wafanye maamuzi. Kwani maendeleo hayatatoka Dar kwa wafanyakazi wa muda ambao kesho na kesho kutwa hawajui kama kazi watakuwa nazo. Je ni kwanini mfanyakazi ambaye yuko Dar ajali shamba la wanakijiji wa Kigoma wakati anaweza kupewa 10% yake na wawekezaji kwa kuwachukulia mashamba wanakijiji. Mfano Masha alikuwa waziri wa mambo ya nje na wakati huo akaenda Maeneo ya Kigoma na rukwa kuwaambia walowezi wa kirundi ambao wamekuja Tanzania kuanzia miaka ya 70's kwamba sasa ni raia na wanaweza kushi popote lakini ni lazima waondoke kwenye eneo hilo kwasababu serikali imepata mwekezaji na watapewa TSH 200 wakaanze maisha sehemu nyingine. Masha huyohuyo baada ya kushidwa ubunge akaja kuwa lawyer wa kampuni hiyo ya kilimo kwenye shamba ambalo alifanya mpango wananchi wale waondolewe. Masha ni mfano tu lakini ni mfano wa mfumo wa sasa ambao unatoa nguvu kubwa kwa watu wachache ambao hawana uchungu badala ya wananchi wanaoathirika.
Manufaa ya Umma: Tumekuwa tukiambiwa serikali imewafukuza wavuvi wa Victoria na kuwapa samaki wote wawekezaji kwa manufaa ya umma, serikali ikiwachukulia wawekezaji wadogo wa Tanzanite na kuwapa Tanzania one kwa manufaa ya uma. Ukweli ni kwamba sasa wananchi hawaoni matajiri wa kisukuma tena walikuwa wanafanya bishara na kujenga miji yao kuanzia mwanza mpaka shinyanga, hatuoni matajiri wa Arusha waliokuwa wananunua magari, wanajenga hoteli na kufungua biashara mbalimbali Tanzania. Huu uwongo wa kusingizia umma ni mbaya sana kwani ukweli ni kwamba uma ni wale waanchi!. Serikali inasema 80% ni ya wawekezaji 10% wanajilipa Dar na 10% wanaamua iende wapi? sasa migodi ya Gold watu wanaishia kupewa shule moja ya msingi kwa mwaka ya vibatari wakati tunakumbuaka matajiri wa Arusha na mwanza walivyokuwa wengi miaka ya mwanzo ya tisini.

Swali langu ni kwamba serikali ni nani kama sio wananchi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom