Serikali ya Tanzania inatumia ipasavyo Tafiti za Wasomi wake?

Naungana na mkuu lumbe kwa kiasi, lakini nina mtizamo tofauti kwangu binafsi naona muda wa kufanya tafiti pindi mtu anapokuwa chuoni ni mdogo sana, na nadhani hata wakubwa wote wa serikali wamepitia huko that`s why they don`t have time kupitia hizo research I suggest to extend muda wa kufanya tafiti katika higher learning Institutions na serikali ikubali kugharamia hizo cos, kingine ninachoweza kusema most of Tanzanian we are not ready to die for others, what do I mean ni kwamba wengi wetu hatupo tayari kuwa risk kwa manufaa ya watoto wetu baadaye zaidi tukimbilia tafiti rahisi ambazo some times ndizo project wanazopewa classa four kwenye academic/international schools, kwa kuwa muda bado upo basi ni vyema basi sisi wacangiaji tukaanza kuwa risk taker tukipewa nafasi kufanya tafiti yoyote ile na ndipo hata hii serikali itakubali tafiti zetu yaani hata dawa za kuulia mende tununue wakati tuna materials zote hapa?.
 
Sijui hata kama watoa maamuzi wanajua hata umuhimu wa tafiti acha kuzitumia,Lakini naamini kuwa kama tafiti zingekuwa zinatumika nadhani msamiati wa njaa ungebaki kwenye vitabu maktaba usingesikika midomoni mwa watawala...matatizo ya maji na umeme ingekuwa ni kwa marejeo ya wanafunzi kwenye historia.
TATIZO KUBWA NI UWEZO WA MFANYA MAAMUZI KUELEWA NA KUTAFSIRI DHAMIRA YA MFANYA UTAFITI NA UHUSIANO WA TAFITI NA MUSTAKABARI WA NCHI,KISIASA,KIUCHUMI NA KIJAMII
 
tuwe wakweli kidogo by looking at another angle, wengi thesis na projects ni za kudesa, cooking data, na kudownload kutoka kwenye internet. Sasa hizo research zinazofanywa na graduates waliocook data, zinaweza kutumika kivipi ili hali kila mtu anajua aliyefanya hiyo research hajawaji kufanya yoyote reliable hata ya Masters degree ali cook data? graduates mwenye ku-cook data atawezaje kuresearch kitu chenye faida kwa nchi? uzoefu and skill ya kuresearch kaitoa wapi?

Nakubali kabisa kuwa kutokana na mfumo wetu wa elimu ya Bongo unapelekea watu kutokuwa creative katika mind zao pale linapokuja swala zima la kubuni na kuanzisha vitu. Wengi wao huwa wanafanya 'copy and paste' au kama ulivotumia neno la kucook-wanazama katika kutengeneza data ambazo zitakubaliana na formula zao ili mradi wapate maksi. Hii ni kusema kuwa mfumo huu wa elimu unatufanya watanzania kuwa wategemezi kiubufunifu wa kisayansi toka nchi za wenzetu. ukitaka kufaulu basi unatakiwa kuandika kutokana na resource za mwalimu, nje ya hapo umefeli na ndo maana kule mashule kuna kitu kinaitwa 'kukremu' na mtu huonekana ana akili sana pale atakapoonyesha uwezo wake wa kurudia kile mwalimu alichosema they are not teaching us to think out the box.

Kuna wakati fulani nilkuwa na wageni fulani katika chuo fulani mkoa fulani katika kufundisha wale wanachuo juu ya elimu ya afya kuhusu malaria, basi mara baada ya darasa wageni walishtuka wanafunzi walipouliza vipi kuhusu notes? Yaani hawakuwa na uwezo wa kwenda na kufanyia kazi wao wenyewe ili kupata info zaidi.

Licha ya kusema hayo, lakini akili yangu bado inakataa kuwa hakuna intellectuals walioweza kufanya kazi nzuri na manufaa kwa nchi na zikatupwa na pengine hata katika maktaba hazipo kabisa. Mi naona ukweli bado uko pale pale ipo kazi kubwa ya kuwajenga vijana wasomi kufikiri na kisha kutumia fikra zao pale wanapofikiri
 
Tafiti nyingi zimefanyika, zipo kwenye makabati zinapata vumbi, kuna sababu nyingi sana ya kwa nini hali inakuwa hivyo.sababu ni nyingi

Globalisation ni moja wapo, we are equating ourselves with first world countries, developed countries ako dunia ya kwanza , sisi tuko dunia ya tatu, they are in 21century we are in 18 century. Kila kitu tunapata kutoka kwao, kila kitu.ANZIA SOCIAL ISSUES MPAKA TECHNICAL ISSUES

tuliingia mkenge kwenye siko huria, na hii imetufanya tuwe watumwa tena, kwa kutaka wenyewe sio kwa kuvamiwa!
 
Nakubaliana na ww mkuu, nakumbuka kwenye kitabu kimoja cha Geog ii wame nukuu tafiti1 inayosema, iwapo bonde la mto rufiji lingetumika ipasavyo, Tz ingejitosheleza kwa chakula.
 
Kweli kabisa hii ni thread nzuri sana. Lakini mimi nina kajisuali kuhusu jamaa mnaowakandia baadhi watatafiti wa Bongo. Nawaombeni kwa hisani zenu mnitumie "any of your scientific critiques of any of the works of those your criticising" kwa mfano tafiti za REDET. Nadhani hii itakuwa hatua ya mwanzo yakusaidia tafiti zitumike ipasavyo nchini Tanzania.
 
Im kind of puzzled on some of the concerns raised on this thread how does one do a copy and paste on a research. Nachukulia mfano mtu umwambie aka chunguze chanzo magonjwa ya kipundupindu somewhere in Tanzania lets say kule kwetu Mburahati. Obviously unategemea majibu yake yawe na sababu za hapo na solution za hapo hapo kulingana na mazingira alioenda ku-investigate. Now how do you copy that from else where. Hapo sasa kama hiyo tafiti ni fake surely itaonekana kwa sababu aitotoa an argument to the problem nor a proposed solution to the problem kulingana na hali ya Mburahati. Au I am missing something hapa?
 
tuwe wakweli kidogo by looking at another angle, wengi thesis na projects ni za kudesa, cooking data, na kudownload kutoka kwenye internet. Sasa hizo research zinazofanywa na graduates waliocook data, zinaweza kutumika kivipi ili hali kila mtu anajua aliyefanya hiyo research hajawaji kufanya yoyote reliable hata ya Masters degree ali cook data? graduates mwenye ku-cook data atawezaje kuresearch kitu chenye faida kwa nchi? uzoefu and skill ya kuresearch kaitoa wapi?

Wataalamu hao hao leo hii wanathaminiwa sana katika nchi mbali mbali Ulimwenguni zikiwemo US, Canada, UK na nyingi nyinginezo. Nakumbuka hata Mkapa aliwahi kuwaita Watanzania wavivu alioambiwa inakuwaje Watanzania waliozaliwa, kukulia na kusomea Tanzania wanapohamia nchi mbali mbali na hata za magharibi wanachapa kazi mtindo mmoja? Hawa si wana tabia ya kutega tega kazi kuchapa domo saa zote sasa inakuwaje wakienda nje waajiri wao wanawathamini sana na kuwaona ni wafanyakazi wazuri? Akawa hana jibu lakini akaacha kabisa kuwaita Watanzania wavivu. Watu wanachukua masters na Phd zao na kuloea kutokana na mawazo kama haya ya kuwaponda Watanzania wasomi.
 
Tafiti nyingi zimefanyika, zipo kwenye makabati zinapata vumbi, kuna sababu nyingi sana ya kwa nini hali inakuwa hivyo.sababu ni nyingi

Globalisation ni moja wapo, we are equating ourselves with first world countries, developed countries ako dunia ya kwanza , sisi tuko dunia ya tatu, they are in 21century we are in 18 century. Kila kitu tunapata kutoka kwao, kila kitu.ANZIA SOCIAL ISSUES MPAKA TECHNICAL ISSUES

tuliingia mkenge kwenye siko huria, na hii imetufanya tuwe watumwa tena, kwa kutaka wenyewe sio kwa kuvamiwa!

CORRECTION: Tuliingia kwenye soko HOLELA siyo soko HURIA. Soko Huria linaongozwa kwa taratibi na sheria wakati soko Holela halina taratibu wala sheria zinazoeleweka mabo yake ni shaghalabaghala. Kwa sasa bado tuko kwenye kipindi cha mpito toka soko HOLELA kwenda kwenye soko HURIA.
Mfano imechukua miaka zaidi ya kumi na tano toka kuanza kwa soko HOLELA kwa serikali kuunda vyombo vya udhibiti.
 
Mada nzuri sana, wataalam tuungane kuunda Database ya research zote zinazofanywa na watanzania in Tz na abroad.
vyuo vikuu vilazimishwe kusubmit hizo reaserch for plagiarism ,research
ikipass ndiyo mtu anatunukiwa digree yake,else jina linatangazwa la kihiyo aliyekopy kazi za watu kwa asilimia ngapi,
software ya kuchek for plagiarism ipo na inatumiwa na vyuo vya ulaya, eg Greenwich universisty ,NCC education uk, etc

after 5yr viongozi wote watakuwa makini na research zetu za bongo,kwani sasa viongozi wengi wako bize na vikao vyenye posho,na hawasomi ripoti wanazopelekewa mezani kwao.
 
tuwe wakweli kidogo by looking at another angle, wengi thesis na projects ni za kudesa, cooking data, na kudownload kutoka kwenye internet. Sasa hizo research zinazofanywa na graduates waliocook data, zinaweza kutumika kivipi ili hali kila mtu anajua aliyefanya hiyo research hajawaji kufanya yoyote reliable hata ya Masters degree ali cook data? graduates mwenye ku-cook data atawezaje kuresearch kitu chenye faida kwa nchi? uzoefu and skill ya kuresearch kaitoa wapi?


Sikubaliani na wewe, kwani you are too general !!! Unataka kusema hatuna wasomi Tanzania maana kama unamaanisha wote wamesoma kwa cooking of Data, then hata hao Professors wanaotoa hizo degree nao ni fake!!!, So we better close our Universities for giving fake degree!!??

Hapo hupo sahii kabisa na hujafanya utafiti wowote huna budi urudi shule tena wewe mwenyewe. Labda utoe mifano ya wanafunzi wanaopata degree fake na maprofessor wao wanaotoa hizo.

KI msingi tatizo la kutotumia tafiti za wataalam wetu, limelala kwenye politics. Mambo mengi yanaendeshwa kisiasa zaidi ya utaalam. Wewe ukifanikiwa kufanya utafiti wako, ambao hata hivyo utakumbana na vikwazo mbali mbali vya financial, data access n.k. mara ukipeleka kwa mkuu wako kwanza atataka iwe yeye ndiye amefanya, ikishindikana anatupa kapuni utafiti na utaambiwa surili. Hiyo subiri huenda hata 10yrs or more .
 
JAMAN MIM SITAKI KUSEMA ILA NAMSHUKURU HUYU ALIE ANDIKA HII ISSUE NA PIA KWA UCHUNGU NAPENDA KUSEMA KWAMBA ILI TAIFA LIENDELEE BASI TAFITI ZINAZO FANYWA NA WATAALAM WETU NI MUHIMU SANA KTK KUFANYA UCHUMI WA NCHI KUKUWA. HIVI EMBU JIULIZE INAKUWAJE NCHI KAMA INDONESIA WALIOKUWA MASIKIN KAMA SISI LEO WAPO JUU. 2.LABDA WATU HAWAJUWI HV UNAFIKIRI USA WALIKUWA MATAJIRI LAHASHA ILA NI AKILI NA UWEZO MKUBWA WA KUPANGA NAKUTENGA SIASA ZA UWONGO NA KUFANYA KAZI NA KUWA NASIASA ZAUKWEL NA VITENDO. JAMAN NILIWAH KUSOMA MAKALA MOJA NAKUONA KIAS GAN MARAIS WA NCHI KAMA USA WANAJIKITA KTK KUSOMA TAFITI MBALI MBAL ZA KIMAENDELEO, ILI KUZIFANYA HAI KIVITENDO, KWAKWELI INATIA MOYO PINDI PROF ATAONA RESEACH YAKE ALIYO IFANYA INATUMIKA KIVITENDO. SASA HAPA NI UJINGA UJINGA TU HAWANA TIME NA KAZ ZA MA PROF NA DKT WETU WANAJIFANYIA MAMBO KI INFORMAL, NYERERE KTK HOTUBA FULAN ALISEMA "JAMANI SISI TULIPOKEA UHURU WAKAT HATUNA WASOMI WAKUTOSHA NA TULIJITAID KWA UPANDE WETU LAKIN NYIE LEO MNAWASOMI WAZURI LAKINI HATAKANUNI TU MWASHINDWA KUZIFUWATA, MNAONGOZA NCHI AS IF HAKUNA WASOMI?", WE NEED A CHANGE NO MATTER WHAT THS NATION MUST CHANGE. God bless Tanzania and God bless u2.
 
Mada nzuri sana, wataalam tuungane kuunda Database ya research zote zinazofanywa na watanzania in Tz na abroad.
vyuo vikuu vilazimishwe kusubmit hizo reaserch for plagiarism ,research
ikipass ndiyo mtu anatunukiwa digree yake,else jina linatangazwa la kihiyo aliyekopy kazi za watu kwa asilimia ngapi,
software ya kuchek for plagiarism ipo na inatumiwa na vyuo vya ulaya, eg Greenwich universisty ,NCC education uk, etc

after 5yr viongozi wote watakuwa makini na research zetu za bongo,kwani sasa viongozi wengi wako bize na vikao vyenye posho,na hawasomi ripoti wanazopelekewa mezani kwao.

New mzalendo umegusia point moja kubwa sana hapo ni tatizo kubwa saana kwetu sisi wabongo na hasa wale watafiti wachanga, plagiarism, ni issue kubwa sana duniani na mtu unaweza kufungwa kabisa. Mfano mmoja ni pale University Of Bristol Uk, kuna mwaka mmoja dada mmoja alifutiwa masters degree yake yote baada ya ile final paper aliyosubmitt kuonekana 8% ni plagiarism tupu.

Point nyingine labda ni kukosekana kwa hiyo database ambayo inainclude kazi za watu mbalimbali nayo ni tatizo kubwa sana. Hii ingekuwepo pengine vijana wangeumiza akili zaidi wakijua kwanza ni kosa kurudirudia (copying) na pia ingewaboost kwani wangeona kuwa kazi zao ambazo ni mpya katika tasnia nzima ya academic zinatambulika na wao wanakuwa recognized kwani wadau mtakubaliana na mimi kuwa utajisikia raha sana pale mtu katika kazi yale anakurefer wewe kwa kazi yako uliyoifanya kabla na inawiana na ile ya kwake.
 
Ndugu wana JF hebu tuangalie naomba suala lazima la utumiaji wa tafiti zetu tunazozifanya hapa Bongo. Katika upeo wangu na mlolongo wangu wa kutafuta elimu nimekumbana na tafiti nyingi sana na mimi mwenyewe nikiwa mmoja wapo wa watu ambao wamebahatika kufanya tafiti mbalimbali ndani na nje ya nchi. Lakini kiukweli mpaka leo sijaona matokeo ya tafiti nyingi ninazozifahamu hapa kwetu.

Resource nyingi sana huwa zinatumika kufanya tafiti hizo lakini mara zinapopelekwa katika nagzi ya serikali ili kufanya maamuzi huwa hazianyiwi kazi ukizingatia na serikali za wenzetu. Na mimi naamini wenzetu wameendelea sana kutokana na hilo na ndo maana katika bajeti zao tafiti huwa zinapewa kipaumbele sana.

Ukipita katika maofisi ya Wizara mbali mbali utakuta makabrasha ya data mbali mbali lakini watu bado wanafanya kazi kwa kutumia miongozo iliyojengwa chini ya data zilizopitwa na wakati ndo kusema wanafanya kazi kutokana na mazoea tu.

Kitu kingine ambacho huwa kinaniumiza kichwa hivi utasikia sijui timu ya wizara ya kilimo ilikuwa Misri kujifunza kilimo cha umwagiliaji lakini wakirudi huku hawafanyii kazi kabisa bali kuonyeshana picha walizopiga katika mabembea huko nchi za watu.

Nawasilisha

check with my sign down here
 
Ni matatizo sana maana tazama hata magraduate wengi wao ni watupu sana katika tafit zao wapo kwa ajili ya kupata PhD tu hakuna jipya humo
 
Tatizo la waTz ni kwamba wanaoenda kujifunza jambo nje si watendaji/wataalamu bali ni adminstrators! Wakisharudi toka kujifunza makarabrasha wanayaweka kwenye mashelf na hawayatendei kazi! Haya mambo ya kukimbilia posho nje yanatuumiza sana nchi yetu!


hayo mambo siyo kwenda nje tu, hata ndani utakuta wanaohudhuria semina nyingi sio watendaji, na hiyo yote ni sababu ya posho tu. utakuta hata uhudhuriaji wao ni wa mashaka sana; wanasinzia, hawachangii lolote, kwa kifupi huwa hawajifunzi chochote. na hiyo ni kwa sababu anajua hataenda kutekeleza hicho alichokuja kujifunza. SIJUI TUANZISHE MITIHANI KWENYE SEMINA?
 
RayB & others,

Many thanks for this useful THREAD.

Sofar michango mizuri imetolewa. Ni kweli Serikali yetu bado haitimizi wajibu wake katika kutumia tafiti mbalimbali za Wataalam wake.
Kutokana na tatizo hili kuna haja ya Watafiti wa Tanzania kuungana na kuwa sauti moja.
Hivi ni lini tumesikia Watafiti wetu kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za utafiti wamekutakana kuongelea ufafiti fulani kwa kina na kisha kutoa maazimio maalum na kisha kuyafuatilia kwa ukaribu katika utekelezaji wake.

Ili kuhakikisha taarifa mbalimbali za utafiti zinawafikia Watanzania na kisha kupata nafasi ya kutekelezwa, pamoja na mambo mengine naomba nipendekeze yafuatayo:

1. Vyuo vyetu vikuu vianzishe ushirikiano wa karibu na kila mwaka wawe wanawakutanisha Wahadhiri wao na kupanga nini cha kufanya.

2. Taasisi zetu za utafiti kwa msaada wa serikali zianzishe kipindi cha televisheni ambacho kitakuwa kikielezea kwa kina matokeo ya tafiti zilizofanyika na nini Watanzania tufanye ili kufaidika na tafiti husika. Kipindi hiki kinaweza kuitwa kwa jina la KUTANA NA WATAFITI WA KITANZANIA. Kwa wiki moja zipatikane angalau saa tatu kila wiki kwa ajili ya kipindi hicho.
 
Moja ya point ilikuwa hivi serikali huwa inatenga hizo fedha kwa ajili ya shughuli hizo? Na kama ndio huwa zinatumika ipasavyo? Au ndo huwa zinateketea kwa sababu hakuna anayeuliza wala kutaka kuzitumia au hata kujua kuwa zipo watu wakataka kuzitumia?
 
Back
Top Bottom