RayB
JF-Expert Member
- Nov 27, 2009
- 2,751
- 196
Ndugu wana JF hebu tuangalie naomba suala lazima la utumiaji wa tafiti zetu tunazozifanya hapa Bongo. Katika upeo wangu na mlolongo wangu wa kutafuta elimu nimekumbana na tafiti nyingi sana na mimi mwenyewe nikiwa mmoja wapo wa watu ambao wamebahatika kufanya tafiti mbalimbali ndani na nje ya nchi. Lakini kiukweli mpaka leo sijaona matokeo ya tafiti nyingi ninazozifahamu hapa kwetu.
Resource nyingi sana huwa zinatumika kufanya tafiti hizo lakini mara zinapopelekwa katika nagzi ya serikali ili kufanya maamuzi huwa hazianyiwi kazi ukizingatia na serikali za wenzetu. Na mimi naamini wenzetu wameendelea sana kutokana na hilo na ndo maana katika bajeti zao tafiti huwa zinapewa kipaumbele sana.
Ukipita katika maofisi ya Wizara mbali mbali utakuta makabrasha ya data mbali mbali lakini watu bado wanafanya kazi kwa kutumia miongozo iliyojengwa chini ya data zilizopitwa na wakati ndo kusema wanafanya kazi kutokana na mazoea tu.
Kitu kingine ambacho huwa kinaniumiza kichwa hivi utasikia sijui timu ya wizara ya kilimo ilikuwa Misri kujifunza kilimo cha umwagiliaji lakini wakirudi huku hawafanyii kazi kabisa bali kuonyeshana picha walizopiga katika mabembea huko nchi za watu.
Nawasilisha