Serikali ya Museveni yaelemewa na ufisadi

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
Bunge la Uganda lililoketi kwa dharula limeazimia kwa kauli moja kuunda Tume ya kuchunguza Waziri Mkuu Amama Mbabazi Waziri wa Mambo Nchi za Nje Sam Kuteesa na Waziri wa Mambo ya Ndani Hillary Onek kwa tuhuma za kupokea rushwa ya mabillioni ya shillingi kutoka kwenye kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow ambapo inasemekana Sam Kuteesa peke yake alipokea £ 17 millioni sawa na UShs 70 billioni.

Bunge limewaamuru mawaziri husika kujivua nyazifa zao ili kuruhusu uchunguzi huru.

Juzijuzi mawaziri Sam Kuteesa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje Mwesigwa Rutukana Waziri wa Kazi na John Nasasira Kiongozi wa shughuri za serikali bungeni walipandishwa kizimbani kwenye mahakama ya maswala ya rushwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi nakuisababishia serikali hasara ya UShs 14 billioni fedha zilizopashwa kutumika kwenye mkutano wa Jumuia ya Madola uliofanyika 2007 CHOGM

Hapo awali aliyekuwa Makamu wa Rais Prof Gilbert Bukenya alinyimwa dhamana nakuswekwa lupango katika gereza la Luzira alikokaa kwa wiki moja Bukenya anatuhumiwa kukiuka sheria ya manunuzi katika ununuzi wa magari na pikipiki zilizotuka kwenye mkutano wa nchi za Jumuia ya Madola kwa masilai yake binafsi

Itakumbukwa Kuteesa na Mbabasi ni washirika wa muda mrefu wa Museveni na wamewahi kushikilia nyazifa za juu katika chama kinachotawala MNR kwa sasa serikali ya Museveni inaelekea kusikojulikana Nawasilisha
 
Narudia tena
Hakuna uhalisia wa kitu chochote hapo. hiyo technique anaitumia Museveni
baadaya ya kushauriwa na Jakaya ili kuwapiga changa la macho waganda
watulize speed ya maandamano ya "Walking to Work" na mengine ambayo
yanatishia mustakabali wake Ikulu.

Haya ni mazingaombwe kama tuliyofanyiwa na bunge na sasa CCM na
Magamba nightmare ambayo yanampunguzia presha president at the end
of the day.
 
Back
Top Bottom