Serikali ya mseto kati ya CHADEMA na CCM ndiyo tiba ya TANZANIA inayougua

Hakuna lisilowezekana chini ya jua! Uzuri kwa Tanganyika ni kuwa ikitokea Chadema au chama chochote cha upinzani chenye nguvu kikakubali kuwa vuguvugu na kuungana na hawa wezi, wauaji na majambazi wa ccm, lazima kitaibuka chama kingine kutetea maslahi ya wanyonge wa taifa hili...
 
Mseto wa nini? kuna njia mbili tu,Magamba waendelee kutufilisi kama taifa au CHADEMA washike dola

Na dalili zinaonyesha kwamba CCM kuendelea kushika dola kwa njia halali ni vigumu labda wafanye mabadiliko makubwa
 
Ndoto za kimagwanda magwanda hizi, baada ya kuona hawawawezi magamba hata kwa maandamano.
 
Hoja hupingwa na hoja. Kuna tofauti kubwa kati ya hoja za viongozi wa CDM na wafuasi wao. Inawezekana chama kikawa na viongozi makini kwa kujenga hoja lakini nyuma yao kukawa na kundi kubwa la watu wanaotumia milima nyama iliyo chini ya migongo yao kufikiri badala ya kichwa. Serikali mseto hulazimishwa na mazingira ya kisiasa kama ilivyotokea Kenya na Zimbabwe. Hayo yanaweza kutokea hapa pia. Mnadhani ikiwa hivyo wanachadema mtafanya nini? Achane kupiga picha hatua 2 mbele badala yake tumieni darubini kuona kilichopo kilomita nyingi mbele.

Sasa naamini kweli wewe umetumwa na magamba, maana hoja yako ni dhaifu sana lakini unazidi kuitetea tu eti kwa kisingizio kuwa hoja hujibiwa kwa hoja, nani wa kujibu hoja ya kijinga namna hii? Hapa hizi comments zinatosha kujibu huu upupu wako, kwa ufupi naomba ujue kuwa hakuna serikali ya mseto mnayoitafuta hapa, time for leaving power of our beutiful Tanzania is now..., acheni kutafuta mahali pa kujifichia kwenye makoti ya CHADEMA!

Kama kweli wewe ni mtu makini na unayefuatilia mambo basi ungekumbuka mdahalo maarufu wa Dr. Slaa wakati ule wa uchaguzi mkuu uliorushwa na ITV, utakumbuka jinsi Dr. Slaa alivyoshangazwa na demokrasia mpya ya kishenzi iliyopandikizwa Afrika ya serikali mseto na watawala wanaoshindwa chaguzi lakini wanataka kujificha huko (kwenye serikali za mseto) kuhofia kukosa ulaji na kushitakiwa kwa makosa waliyoyatenda wakiwa madarakani. Kama kweli unalijua hilo kwa nini useme CHADEMA wana viongozi wanaofikiri tofauti na maoni haya? Au unafikiri kuwa ****** ndiye atakayekuwa kiongozi wa CDM wakati wa muafaka huo wa kipumbavu? Yawezekana wewe ndio unayetumia hayo ****** yako kufikiri badala ya kichwa chako!
 
Taratibu, wala usitumie nguvu saana usije ukanyofoka mishipa ya shingo. Kaa upya na ujaribu kutafakari kwa kina ni nini huwa chanzo cha kuingia katika mchakato wa serikali ya mseto. Usifikiri mimi ni CCM kama akili yako inavyokutuma. Uwezekano wa CDM kuishinda CCM kwa kura haupo kwa sasa. Labda kwa miaka mingine 15 ijayo kama CDM itaendelea na nguvu hii hii iliyonayo sasa. Lakini inaweza kukaribia ushindi na kujiaminisha kuwa imeshinda. Wakati CDM watakuwa na imani kuwa wameibiwa kura, CCM yenye dola itabaki na msimamo wake wa ushindi. Unadhani hapo kitatokea nini kama si mgogoro unaoweza kupelekea kutafutwa kwa serikali ya mseto ili kunusuru roho za raia wasio na hatia. Tizama mambo kwa mapana si kwa ushabiki usio na maana.
 
Jamani embu tupange kwanza baraza la mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi wa hiyo mseto ndipo tutakapo uona ugumu wa ilo jambo.
 
Mnataka kuniaminisha kuwa kudumaa kwa Tz kumesababishwa na kukosekana kwa selikali ya mseto?
 
Ni jambo unaloweza kulitizama kwa mashaka na wepesi. Lakini kutokana na upepo wa kisiasa ulivyo hili si jambo la kushangaza kwani linaweza kutokea. Harakati za CDM zinaweza kufikia hatua ya kuundwa kwa serikali ya mseto katika chaguzi za usoni zijazo.

Bora hili litokee mapema ili kuleta chachu ya kuchochea maendeleo ya nchi hii. Naamini wale wanachama wa CDM wanaweza kuliona jambo hili kama upuuzi.

Hata kwa upande wa wale wa CCM wanaweza kuchukulia kuwa ni jambo gumu kwao. Lakini linaweza kutokea kutokana na nguvu na misigino ya kisiasa. Bora serikali ya mseto itokee kwanza kuliko CCM kuendelea kubaki madarakani milele.

CCM yenye watendaji wachache waadilifu inaweza kuwa na changamoto motomoto iwapo itaongezewa nguvu na watendaji kutoka CDM katika mseto. Hii inaweza kuwa tiba, au nusu tiba kwa Tanzania inayougua.
Hii itakua ujaribu kufanya cross section ya mchicha(CCM)na Mbuyu(CHADEMA).
 
Back
Top Bottom