Huu ni mwanzo tu wa mwisho wao . . Arusha ni yetu sasa baada ya mafisadi na wauaji kukimbilia kusikojulikana. Nguvu ya umma daima.
hii nimeipenda sana. hata hiyo ya majambazi usiku sijui kama wanaiweza maana mijioga kweli inatafuta wasio na silaha
ukweli usiopingika ni kuwa kuna mtu anaongoza serikali bila wananchi na kuna mtu anaongoza wananchi ila hana serikali
hii imekaa vizuri sana na imeeleweka na ndio ukweli ulivyo
Leo imedhihirika wazi kwamba unyama uliofanywa na CCM kuwaua wenzetu umeendelea kuisuta serikali na hivyo kukosa ujasiri wa kujitokeza hadharani hata tu kutembelea majeruhi pale Mount Meru hospital.
Hali hiyo imeendelea leo wakati wa kuaga miili ya wana ukombozi pale ambapo serikali imeingia tena mitini kuanzia Mkuu wa Mkoa Rc Shirima na mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Ni kana kwamba CHADEMA imepewa kuongoza serikali mkoani Arusha leo na ikafanikisha kwa ufanisi mkubwa kuliko hata serikali ya Mafisadi na wauaji. Leo imeonekana kumbe hamna haja ya polisi kwani wao wanaweza kufanya tu shughuli za kusaka majambazi usiku.
Aibu iliyoifanya serikali ya mkoa kutohudhuria mazishi naomba iwasute hivyo hivyo na wafanye maamuzi ya busara ya kujiuzulu kwa wale wahusika wa mauaji ili at least wajisafishe. Ila wasipojisafisha au kuchukua hatua madhubuti itakuwa ngumu mno kuaminika tena mikononi mwa wananchi wa Arusha na hata nchi nzima. Sijajua watatumia sabuni ya namna gani kujisafisha.Waendelee kukaa mafichoni hivyo hivyo na wasijaribu kuitisha vimikutano vyao vya kichovu tena.
Mwanzo wa ukombozi umeshaanza tayari na CCM kwa Arusha imetoweka na hopeful harakati hizi zitaendelea mikoa mingini hadi bendera ya mwisho ya CCM itakapokuwa imeshushwa.
Aluta Continua!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!