Serikali ya malawi kushusha thamani ya pesa yake kwa asilimia hamsini.

Nzoka yihenge

Member
Jan 14, 2011
46
29
Nimesikia kupitia tbc habari kuwa malawi itashusha thamani ya pesa yake kwa 50% ili kuokoa uchumi wake. Wadau wa masuala ya pesa naomba nifungueni nipate kuelewa ni kwa namna gani hii inaweza kuokoa uchumi wa nchi.
 
Huo ndio ujinga usiokubalika kiuchumi duniani kote humu. Kwanza tuangalie njia za kuimarisha uchumi, uzalishaji wa bidhaa za kuuza nnje na upunguzaji uagizaji bidhaa toka nnje. Hii ya kushusha thamani ya pesa ndo kwanza naisikia.
 
Bora wale wanaoweka akiba zao kwa Dola za Kimarekani. Wao wataendelea kupeta. :usa2:
 
Malawi imechukua hatua hii kufuata taratibu walizopangiwa na IMF, taratibu ambazo marehemu Mutharika alizikataa akiogopa inflation, kupunguza thamani ya hela yako kuna effect ya kupunguza gharama za exports na kuongeza gharama za imports.
 
kwa hiyo kama wanazalisha sana na kuuza nje basi itawasaidia !
 
Malawi imechukua hatua hii kufuata taratibu walizopangiwa na IMF, taratibu ambazo marehemu Mutharika alizikataa akiogopa inflation, kupunguza thamani ya hela yako kuna effect ya kupunguza gharama za exports na kuongeza gharama za imports.

Kama nchi ina uzalishaji na exports nyingi kupunguza thamani za fedha yako actually kunaweza kusaidia ku boost exports kwa sababu zinakuwa cheaper kwa wenye dollars. Ndiyo maana Mmarekani anampigia kelele mChina kila siku kwa sababu mChina anaifanya hela yake isiwe na thamani sana artificially na makusudi.

How much to devalue, by which method and speed is a delicate dance which may determine the success or failure of the measure.

Matatizo ya nchi zetu hizi tunapunguza thamani hela kwa sababu ya mikopo, hatuna uzalishaji.
 
Huo ndio ujinga usiokubalika kiuchumi duniani kote humu. Kwanza tuangalie njia za kuimarisha uchumi, uzalishaji wa bidhaa za kuuza nnje na upunguzaji uagizaji bidhaa toka nnje. Hii ya kushusha thamani ya pesa ndo kwanza naisikia.

kwa ninavyojua from economic view,nchi inaweza kushusha thamani ya pesa(depreciation of the currency),hii inasababisha bidhaa za ndani(exports) kupata soko kubwa la nje ya nchi,coz bidhaa zako zinakua very cheap kwa sababu pesa yako ni ya thamani ya chini, na baada ya bidhaa zako za ndani ya nchi kwenda kununuliwa kwa wingi nje,hii inasababisha kukua kwa kipato kwa nchi yako and then uchumi wa nchi una improve,sio rahisi sana kwa nchi zinazoendelea(developing countries) kuliona hili kwa haraka sana ingawa linawezekana,coz kukua kwa uchumi kuna involve factor nyingi kidogo sio tu "depreciation of the currency",na hili la kushusha thamani ya pesa huwa linaweza kuambatana na disadvantages kama vile kupanda kwa bei ya vitu ndani ya nchi(next time tutaelezana ni kwanini bei znaweza kupanda),so inatokana na economic policy gani ya nchi kwa wakati huo inatumika ili kukubaliana na suala la kushusha thamani ya pesa yako,kama unakumbuka, Mgogoro kati ya aliekua gavana wa benki kuu miaka ya nyuma kidogo Mzee Mtei(muasisi wa CHADEMA) na baba wa Taifa(KJN),ilikua ni kusudio la Mtei kuomba kushusha thamani ya pesa lkn Nyerere akagoma,lkn nia ya Mtei ilikua ni ku promote Exports,kwa leo naishia hapo maana usingizi unanivizia hapa........................!
 
Kwa hiyo CHADEMA indirectly inashabikia kushusha thamani shilingi yetu? (MTEI MWASISI. WA CHADEMA)
 
Back
Top Bottom