Serikali ya JK inataka Kumchafua Nyerere?

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
Ndugu wanaJF

Katika kuelekea uchaguzi october 2010 nimeona hili niliweke wazi, Baba wetu wa taifa ameanza kuchafuliwa katika media mbalimbali ikiwemo jf na TAHASISI YAKE CHINI YA BUTIKU INAANDAMWA NA CCM KILA KUKICHA, inawezakana alifanya mabaya lakini kumchafua mtu ambaye ameishachukuliwa na Mungu sio haki.

Hii inaweza kuwa mbinu ya JK na sirikali yake kujitakatisha kuelekea uchaguzi.

JK baba wa Taifa kafanya mengi muache apumzike otherwise Mizimu yake itakuibukia siku za mbeleni

Ni hayo tu

WanaJF mnasemaje??
 
Alijaribu Che Nkapa kufuta "legacy ya Nyerere' hakufanikiwa ije iwe huyu wa leo?
 
ungetoa hiyo article inayo mchafua ili tuone na kupima unacho kisema. hata ikiwa heading tu za hizo thread., kama zipo nyingi.
 
Nadhani Baba wa Taifa alikuwa Nyerere tu. Wengine waliofuatia ni maraisi.
 
Kwani anachafuliwa au anajadiliwa kama wanasiasa wengine duniani ambao ni marehemu? Who is Nyerere after all?

Kosa kubwa alilolifanya - kwa maoni yangu -- ni kutuharibia dhana nzima ya demokrasia ya vyama vingi - pale aliposapoti CCM na kuifanyia kampeni badala ya kukaa neutral na kuitikia kilio cha kuwa Baba wa Taifa halisi.

Angekaa neutral sasa hivi tungekuwa na uwiano wa vyama -- yaani upande wa serikali na upinzani unaoleta maana -- kama vile ilivyo huko Kenya na Zambia, kwa mfano.
 
Kwani anachafuliwa au anajadiliwa kama wanasiasa wengine duniani ambao ni marehemu? Who is Nyerere after all?

Kosa kubwa alilolifanya - kwa maoni yangu -- ni kutuharibia dhana nzima ya demokrasia ya vyama vingi - pale aliposapoti CCM na kuifanyia kampeni badala ya kukaa neutral na kuitikia kilio cha kuwa Baba wa Taifa halisi.

Angekaa neutral sasa hivi tungekuwa na uwiano wa vyama -- yaani upande wa serikali na upinzani unaoleta maana -- kama vile ilivyo huko Kenya na Zambia, kwa mfano.

Alisapoti CCm kwa sababu alimuogopa Mrema ambaye kama angeshinda alihofu kuwa angemshughulikia kwa madhambi yake. Naamini kabisa sababu ni hiyo tu -- na siyo kujenga demokrasia nzuri nchini mwake. Naamini kabisa Mrema ange-move against him!
 
Ulieanzisha thread nadhani ulikuwa na mawazo kama yangu..

I am sorry lakini niseme sixth sense yangu inaniambieje..


This is how I see it..

Kuna hawa ma-kampenist Malaria Sugu et al, kuna A' Nuur, kuna mitandao yenye muelekeo ya ki- al Qaeda kama Mzalendo etc , and then unaeza kuona juhudi za hizi institutions na individuals zinavoipigia CCM chapuo..

For starters hii sio coincidence..GO and Figure.
 
Alisapoti CCm kwa sababu alimuogopa Mrema ambaye kama angeshinda alihofu kuwa angemshughulikia kwa madhambi yake. Naamini kabisa sababu ni hiyo tu -- na siyo kujenga demokrasia nzuri nchini mwake. Naamini kabisa Mrema ange-move against him!

huyu Mgonjwa wa akili huyu, alimtisha Nyerere ? u cant be serious.
Nyerere alipima ubongo wa jamaa na kuona kua ni mwehu kidogo, kuna kamtindio kaubongo kidogo, sasa alichohofia ni ikiwa wendawazimu wake ungelipukia akiwa Ikulu.
 
basi kama kila aliemaliza uharibifu wake aachwe apumzike kwa amani ya nini kupiga makelele ya kutaka akina Mkapa, Lowassa n.k washitakiwe kwa makosa waliyofanya si kila siku wanasemw JF humu wakati wameshajipumzikia, wacha watu wamjadili Nyerere on his other side ambayo inafichwa makusudi, calling people names can't stop them express their views...never!
 
...Kuna hawa ma-kampenist Malaria Sugu et al, kuna A' Nuur, kuna mitandao yenye muelekeo ya ki- al Qaeda kama Mzalendo etc , and then unaeza kuona juhudi za hizi institutions na individuals zinavoipigia CCM chapuo..
.
Daah, wakati mwingine mawazo huwa yanafanana ila tu mmoja anaanza kuyaweka hadharani! I was thinking the same!
 
Mimi nafurahi wanavyoandika kwani hatimaye historia yetu itaanza kuandikwa kwa ukweli kuliko hii ambayo watu wananong'onezana mafichioni. Of course, toka kaburini bado Nyerere ni tishio kwao kwani wananchi wakiamka na kuanza kumkumbatia Nyerere na Falsafa yake ya "maendeleo ni maendeleo ya watu siyo vitu" na mambo yale ya usawa na haki hawa watu hawataweza kusimama. Lakini vile vile ijulikane hakuna chama chochote cha siasa nchini leo hii ambacho kimetamka wazi na pasipokutetema kuwa kinamuunga mkono Nyerere isipokuwa CCJ na kuwa kitarudisha baadhi ya mambo ya misingi ya taifa letu.

Hili linawatisha. Sitoshangaa muda si mrefu viongozi wa juu wa CCM wataaanza kumpuuzia Nyerere hadharani.

Tayari wameendelea kuinyanyasa taasisi ya Mwalimu Nyerere na kuinyima kibali cha kujenga ghorofa sita pale na kuna uwezekano kabisa wanataka kuona wale waasisi waliokuwepo pale wote wanatoka ili waweze kupandikiza watu wao. NI mojawapo ya migogoro ambayo inaendelea chini kwa chini.
 
Nyerere ni vigumu sana kumwondoa kwenye mioyo ya watu, he was really a man of people! Vilevile kupitia utunzi wake wa vitabu, wanafunzi wanasoma na kupenda machapisho yake! Hotuba zake hazichuji, hazichoshi kusikiliza! Waliosoma na kupata matibabu "enzi za Mwalimu" walipewa huduma bure! Alijenga viwanda: Nguo, Zana za Kilimo (UFI), Mbolea, Saruji, Tanganyika Pakers, Mabwawa ya kufua umeme, just to mention few! Alipambana na rushwa kwa vitendo! Sasa hivi, esp wakati wa JK, kama huna vijisenti, sahau fomu ya kugombea uongozi ndugu, utaaibika! Atakayesahau legacy ya Mwalimu au kuipuuza ana lake jambo, aogopwe kama ukoma!
 
Hivi ni mtumishi gani au ofisa gani wa ngazi zajuu anayeheshimika kimataifa na kitaifa ambaye ni zao la uongozi wa Mwinyi, Mkapa au Kikwete?
 
sio kumchafua nyerere tu, kazi yao ni kuwapunguza wale wanaofanya kazi kwa bidii na kupata credit kwa wananchi kama kina magufuli etc....anataka sifa zote yeye ndo achukue, hadi mazuri ya mkapa atayafunika wakati yeye hajafanya chochote zaidi ya kutembelea nchi kadhaa duniani kukinga bakuli bila mafanikio.
 
Ndugu wanaJF

Katika kuelekea uchaguzi october 2010 nimeona hili niliweke wazi, Baba wetu wa taifa ameanza kuchafuliwa katika media mbalimbali ikiwemo jf, inawezakana alifanya mabaya lakini kumchafua mtu ambaye ameishachukuliwa na Mungu sio haki.

Hii inaweza kuwa mbinu ya JK na sirikali yake kujitakatisha kuelekea uchaguzi.

JK baba wa Taifa kafanya mengi muache apumzike otherwise Mizimu yake itakuibukia siku za mbeleni

Ni hayo tu

WanaJF mnasemaje??

Hivi nyinyi lini mtakuwa na shukurani kwa huyu Jk ?amekufanyieni mengi katika kipindi chake cha miaka mitano ya mwanzo leo nchi inatambulika lika pembe wawekezaji wanapiga hodi kila siku maisha ya Binadamu wa nchi hii hajawahi kuwa maisha ya kuvutia kama yalivyo katika kipindi chake amekupeni fursa za kwenda mahali popote pale ikiwa unauwezo amejenga miji leo hii ndio mnayojivunia kuwa Tz tambarare wacheni Kumsakama Kiongozi kiasi hicho kuweni na shukurani ,hivi leo kila mtu amekuwa mrembo wakati wa amu hiyo mnaitaja ya Kambarage tulikuwa tunakogea masabuni ya kuosheya punda tuklivaa sare kama watioto wa shule, hakukuwepo na ruhusa ya kufanya lolote lile ,mpeni sifa nzuri kwa mazuri aliyoyafanya Jk na sio katika hali hii manyo muongelea ( nakumbuka mwali aliwahi kusema kumwambia marehemu karume kuwa hataki watu wake wawe na Tv kwani watafuta mambo ya nje )leo angalie watu wake wnayafanya yale ambayo hakutaka wayafanye kuiga maiha ya west.,lakini hamlitaki kuliongea hilo ni chungu kiasi kama shubiri.
 
sio kumchafua nyerere tu, kazi yao ni kuwapunguza wale wanaofanya kazi kwa bidii na kupata credit kwa wananchi kama kina magufuli etc....anataka sifa zote yeye ndo achukue, hadi mazuri ya mkapa atayafunika wakati yeye hajafanya chochote zaidi ya kutembelea nchi kadhaa duniani kukinga bakuli bila mafanikio.

Una uhakika kinachokuuma hapa ni SIFA BORA ZA NYERERE ama kwako wewe unadhani kinachoendelea ni UDINI wa hao wa upande mwengine ambao ukweli yawezekana hawana tofauti na udini wa upande wako?

Ukweli ni kuwa kuna juhudi za makusudi za kuchafua na kuzika kabisa legacy ya Nyerere lakini sio wote wafanyao hivyo wanasukumwa na hulka zao za udini na sio JK wala serikali ya JK. Suala hili lipo juu zaidi ya watu ama serikali ya fulani. Hili ni suala la kiitikadi ambapo wale wapiga chepuo wakuu wa kila wakiitacho MFUMO WA SOKO HURIA wakikwepa kuita ni UBEPARI wanaona kila kitu kinachohusu UNYERERE ni kama unaa ama kizingiti kwa maslahi ya ajenda zao. Pia vita hii inaendeshwa na hata wakuu wangine wa kidunia ambao wengine ni wakristu wazuri tu. Hivyo ni busara kuangalia suala hili kwa umakini na upana wake na sio hizi emotions zilizogubikwa na mwashawasha wa udini uanozidi kujikita katika fikira zetu za kisiasa na kijamii.

Omarilyas
 
Alijaribu Che Nkapa kufuta "legacy ya Nyerere' hakufanikiwa ije iwe huyu wa leo?

Hawawezi kumchafua Mwalimu bwana! Maana history siku zote husema kweli na bado kuna Watanzania wengi ambao wana kumbukumbu nzuri sana za Mwalimu kama kiongozi, hakuwa perfect lakini alikuwa ni kiongozi mkweli, hakuwa na makuu wala tamaa na uroho wa utajiri wa haraka haraka kama hawa wa leo, aliipenda Tanzania na Watanzania kwa moyo wake wote na siku zote maamuzi yake yalijali zaidi ni jinsi gani ambavyo Watanzania wangeathirika na maamuzi hayo. Hivyo kamwe hawataweza kumchafua Mwalimu.

 
Back
Top Bottom