Serikali ya ccm na uwekezaji !

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,418
Uwekezaji huu ni kwa manufaa ya watanzania wote au kikundi cha mafisadi? kuna taarifa kuwa serikali imesaini mkataba na kampuni ya Orphir Energy ya mjini London mkataba wa $50m kuchimba mafuta baharini sehemu za Mtwara kutokana na makubaliano ya mkataba huo Tanzania itapata asilimia 12 ya mapato yatakayopatikana, ninachouliuliza huu ni uwekezaji au ni mwendelezo wa deal za Richmond? Wadau mliopo London jaribuni kutafuta ukweli wa jambo hili maana hii ni kali kuliko ya Richmond, Rigs ya kuchimbia mafuta ipo njiani kutoka South Korea, je CCM imeshawaeleza wananchi juu mkataba huu?
 
May mwaka huu William Ngeleja alisaini mkataba wa dola bilioni 7 na hii kampuni ambao niliona ni mkubwa sana kama $7billion ni kwa ajili ya Exploration, development and oparation.

Hii $50m ni part ya hiyo bilioni 7? N hiyo asilimia 12 wanapata baada ya "cost oil"? Hivi vitu wasipo viweka wazi tutaendelea kuliwa kila mkataba wanao saini.
 
asilimia 12 ni baada ya kutoa matumizi kitu ninacho doubt bei ya mafuta hivi sasa ipo juu, itakuwaje hao wawekezaji wachukue asilimia 88, hao viongozi wetu wanachoangalia ni maslahi yao binafsi.
 
Halafu ni aibu sana waziri kijana kama huyu kusaini mkataba ambao utakula nchi yake kwa muda mrefu! Haoni haya wenzie watakapochukua nchi waiibue hii aibu wakati yeye bado anataka kutanua! Bure kabisa waTZ, hatuonaji mbali zaidi ya pua yetu
 
asilimia 12 ni baada ya kutoa matumizi kitu ninacho doubt bei ya mafuta hivi sasa ipo juu, itakuwaje hao wawekezaji wachukue asilimia 88, hao viongozi wetu wanachoangalia ni maslahi yao binafsi.
Unapoona magazeti yanapo mpamba waziri kusaini mkataba mkubwa wa dola bilioni 7 bila kuhoji ni za nini, tuna matatizo makubwa ya kutoelewa mambo?

mkataba wa bilioni 7 kampuni kuchukuwa asilimia kubwa sitashangaa.Lakini wasi wasi wangu huko ni kweli haya makapuni yanatumia pesa nyingi kwenye matumizi yao au ni njia ya kutunyonya?

Haya makampuni yana spend so much money on accountants kujaribu kuficha vitu kama hivyo kupanda kwa bei za mafuta.
 
Back
Top Bottom