Serikali, Wenye Hisa za NICOL ndio wameliwa au...?

Ikena

JF-Expert Member
Oct 24, 2007
553
392
Kila nikitaka kuuza hisa zangu naambiwa haziuziki, sasa ndo kusema nimeliwa au nivute subira?

Sasa kwanini wasiturudishie fedha zetu kabla hisa hazijazidi kushuka thamani zaidi? Hvi nitawezaje kupata fedha zangu iwapo kampuni hii itaingia mitini?

Naombeni mchango wenu wa mawazo.

========
UPPDATES:
========

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka mkutano wa NBAA, CMSA, BRELA na DSE kuhusiana na NICOL

Katika Mkutano uliofanyika tarehe 27 Octoba 2009 ukishirikisha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Wakala wa Usajili na sheria za Biashara (BRELA), and Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) zikiwa ni taasisi zinazosimamia shughuli za kampuni chini ya sheria mbalimbali, mambo yafuatayo yalijitokeza.

I. Yaliyojitokeza
1. Kukiuka Kanuni za Kimataifa za Kihasibu (IFRS)
Baada ya NICOL kuwasilisha taarifa ya hesabu za fedha zilizokaguliwa kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2008, katika kupitia taarifa hizo, CMSA ilibaini kuwa utayarishaji wa taarifa hizo haukuzingatia kanuni za kimataifa za uandishi wa vitabu vya hesabu za fedha (uhasibu) yaani International Financial Reporting Standards (IFRS) na pia ilibainika kuwa hesabu hizo zinapotosha hali halisi ya kifedha ya Kampuni ya NICOL (financial position) na faida ambayo NICOL iliripoti. Mkutano huo ulithibitisha kuwa:

(a) CMSA na NBAA kwa pamoja walitoa maagizo kwa Wakaguzi wa hesabu wa Kampuni ya NICOL wamtake mteja wao, NICOL kuwa:-
(i) aondoe taarifa za hesabu za mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2008 kwa kuuarifu Umma (press release)
(ii) atayarishe upya taarifa hizo kwa kufuatana na kanuni za kimataifa za kihasibu na kuziwasilisha kwa ukaguzi kulingana na Kanuni za kimataifa za Ukaguzi wa hesabu yaani International Standards on Auditing (ISAs)..

Sababu kubwa ya kuitaka NICOL iondoe taarifa za hesabu zake ni kuwa taarifa hizi za hesabu za fedha zilikuwa hazitoi ukweli kuhusu hali halisi ya kifedha ya kampuni na hivyo kupotosha Umma.

(b) Wakaguzi wa Hesabu wa NICOL walikiri kufanya makosa kwa kutoa hati safi (unqualified audit opinion) kuhusiana na taarifa hizo za hesabu za kampuni ya NICOL na Kumtaka mteja wao atayarishe upya hesabu hizo kufuatana na kanuni za kimataifa za Kihasibu na kuziwasilisha kwao kwa ukaguzi kabla ya kuzitoa kwa Umma.

(c) Endapo taarifa za hesabu za Kampuni ya NICOL zingetayarishwa kuendana na kanuni za kimataifa za uandishi wa vitabu vya hesabu za fedha hali ya kifedha ya NICOL na faida iliyoripotiwa ingekuwa tofauti kabisa na ripoti yao potofu inavyosema.

2. Kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanahisa Kinyume na Matakwa ya Sheria ya Makampuni
Katika kulinda maslahi ya Wanahisa wa NICOL, CMSA na DSE waliiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya NICOL wasifanye mkutano wa Mwaka wa Wanahisa (AGM) bila kuwa na Taarifa za Hesabu sahihi na zinayokubalika kwa mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2008 kama Sheria ya Kampuni ya mwaka 2002 inavyoelekeza. Kwa mujibu wa sheria ya Makampuni, uwasilishaji wa taarifa za fedha zilizokaguliwa ni moja ya kipengele cha lazima katika ajenda za Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa.

3. Kukaidi Kutekeleza Maagizo na Kutoa Taarifa Potofu kwa Wanahisa
(a) Wakurugenzi wa kampuni ya NICOL pamoja na kutakiwa na Mamlaka tatu za usimamizi, NBAA, CMSA and DSE walikaidi agizo la kutayarisha upya taarifa za fedha za Kampuni kwa Mwaka Ulioishia tarehe 31 Desemba 2008.

(b) Pamoja na kukumbushwa mara kadhaa na kushauriwa na Wakaguzi wa Kampuni, Wakurugenzi wa NICOL walikaidi agizo la kuondoa taarifa hizo za hesabu. Kibaya zaidi Wakurugenzi wa NICOL waliweka kwenye ripoti ya Mwaka Maoni ya Wakaguzi (audit opinion) huku wakijua kwamba tayari wakaguzi hao walishaondoa maoni yao.

(c) Wakurugenzi wa NICOL waliendelea kuitisha mkutano tarehe 24 Octoba 2009 na wakagawa kwa Wanahisa pamoja na nakala nyinginezo, Ripoti ya Mwaka ambayo ina mahesabu ambayo Mamlaka za usimamizi ziliagiza ziondolewe kwa sababu zilikuwa zikitoa taarifa potofu kwa Wanahisa.

(d) Wakurugenzi wa NICOL wamekaidi kurekebisha taarifa zao kama Mamlaka za Usimamizi zilivyoelekeza. Wakurugenzi wa NICOL walitakiwa kutekeleza kwanza maagizo waliyopewa kabla ya kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanahisa ili wasiwape wanahisa taarifa potofu.

4. Wakaguzi Kuondoa Maoni yao Kuhusiana na Mahesabu na Hatima yake
Kutokana na kukosekana ushirikiano kutoka kwa Wakurugenzi wa NICOL, Wakaguzi wa Hesabu kupitia barua yao nambari MACO/NICO/10/09 ya tarehe 8 Octoba 2009 waliondoa maoni yao (audit opinion) juu ya taarifa hizo za hesabu za Fedha za NICOL kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2008 na kumtaka mteja wao arudishe kwao nakala zote zilizosainiwa za mahesabu hayo. Kuondolewa kwa Maoni kuhusiana na hesabu maana yake ni kuwa NICOL haina taarifa za hesabu za fedha zilizokaguliwa kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2008.

5. Kampuni ya NICOL Kufanya Maamuzi ya Uwekezaji Bila Kufanya Uchunguzi Yakinifu
Baada ya zoezi la ukaguzi lililofanywa na CMSA (onsite inspection), ilithibitika pia kuwa, Wakurugenzi wa Kampuni ya NICOL wamefanya maamuzi mbalimbali ya Uwekezaji bila ya kufanya uchunguzi yakinifu (Due Diligence) na hivyo kuwa na uwekezaji wenye ubora hafifu kama ilivyowekeza kwenye makampuni ya Interchem Pharmaceutical and Beverage Limited (IPBL) na Twiga Feeds Ltd na hivyo kuhatarisha maslahi ya wanahisa. Wakurugenzi wa NICOL waliagizwa waajiri Mtaalamu wa Mambo ya Uwekezaji (Fund Manager) ili awashauri katika kufanya maamuzi ya uwekezaji. Mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo pamoja na kukumbushwa mara kadhaa.

II. Maoni na Mapendekezo ya Mamlaka Zinazosimamia Kampuni kwa Mkutano wa Wanahisa Uliopangwa Kufanyika Tarehe 31 Octoba 2009
Kufutia maelezo hayo hapo juu, ni wazi kuwa Wakurugenzi wa kampuni ya NICOL wamekuwa wakaidi na wameshindwa kutimiza wajibu wao. Wanahisa wana haki katika Mkutano Mkuu kuteua Wakurugenzi na inapoonekana muhimu kuwaondoa. Mamlaka zinazosimamia shughuli za kampuni tuna maoni na mapendekezo yafuatayo kwa Mkutano wa Wanahisa uliopangwa kufanyika tarehe 31 Octoba 2009.

Wakurugenzi wa kampuni kwa kipindi kinachoishia tarehe 24 Octoba 2009 hawana sifa ya kuendelea kuwa wakurugenzi na hivyo wajiuzulu au waondolewe. pia hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002.
Bodi mpya iahidi kwamba itatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mamlaka za Usimamizi.

III. Kushindwa kwa Wanahisa Kutekeleza Mapendekezo ya Mamlaka za Usimamizi
Wanahisa wanatakiwa watambue kwamba wakishindwa kutekeleza kwa ukamilifu mapendekezo ya Mamlaka za Usimamizi itapelekea Mamlaka hizo Kuchukua hatua kali dhidi ya Kampuni kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zilizopo.

More updates:
Resign, Bomani advises NICOL board members

By FARAJA MGWABATI | Daily News | 29th October 2009

FORMER board member of the National Investment Company (NICOL), Judge Mark Bomani has advised current members to step down to pave the way for investigations into alleged financial scam.

The Nicol board faces a series of allegations involving preparing false financial statements to deceive its shareholders.

Bomani's comments comes a day after the Capital Markets and Security Authority (CMSA) issued a warning to board members for failure to comply with its directives regarding proper presentation of 2008 financial statements.

"I think the board members must follow the authority's advice because CMSA is the supervising authority of companies such as NICOL," Bomani said in a telephone interview.

"It would be better if they stepped down and give room for investigations and reduce tension to shareholders," said Bomani, adding that he withdrew from the board more than a year ago after he reached statutory age of 70 years.

The CMSA in a joint statement with Business Registration and Licensing Agency (Brela), Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) and National Board of Accountants and Auditors (NBAA) on Wednesday asked the shareholders to force the board members to resign and take them to court if they refused to heed.

Commenting on CMSA's statement, NICOL's Board Chairman, Mr Felix Mosha, yesterday admitted that the company's financial statements were not clean.

The chairman, who together with other shareholders, has been in friction with CMSA for a while, said yesterday that they are currently rectifying the mistakes.

"It's true there was problems in our financial statements&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];we are correcting them and we are in discussion with the CMSA over the matter," said Mr Mosha.

Mr Mosha yesterday assured shareholders that their money invested in the company were safe, saying "85 per cent of their money is safe with National Bank of Commerce."

The chairman, however, declined to comment on CMSA's view that they should resign or be kicked out of the board, or taken to court.

The CMSA also alleged that they observed after on spot inspection, that NICOL Directors made investment decisions without undertaking proper due diligence which resulted into questionable quality of investments in the companies such as Interchem Pharmaceutical, Beverage Limited (IPBL) and Twiga Feeds Ltd.

CMSA's statements came just few days after NICOL convened its annual general meeting last Saturday which was deemed illegal by the authorities. The meeting was postponed to tomorrow.

The verdict is expected to be delivered tomorrow by shareholders at the meeting, though CMSA maintained in their statement that they should not present financial statements to the shareholders because their books were not clean.

According to NICOL's website, board members comprise prominent personalities including Ibrahim Kaduma, Idd Simba, Hashim Mbita, Dr Martha Qorro and Thabita Siwale. Others like Reginald Mengi and Nehemiah Mchechu resigned recently after the revelation of the questionable report in NICOL
August 21, 2009

Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) wametoa 'Public Notice' kuhusiana na NICOL (National Investment Company Limited).


Kwa kifupi ianaelekea NICOL wameshindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yao kama kampuni iliyosajiliwa katika soko la hisa la Dar es Salaam na hivyo imesimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia 21 August 2009.

Kwa kuwa hii ni kampuni ya 'umma' (Public Limited Company - PLC), hali hii inatishia uwekezaji wa wananchi wengi walioufanya katika kampuni hii (Kama itakuwa de-listed moja kwa moja!)

Ni nini kinaendelea ndani ya NICOL?
Kampuni ya NICOL hatarini kufutwa katika soko la hisa

Na Ramadhan Semtawa | Mwananchi | Septemba 29, 2009

BARAZA la Uongozi wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), limeisimamisha kwa mwezi mmoja Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL), katika orodha ya makampuni yanayopaswa kuuza hisa kwenye soko hilo.

NICOL ni kampuni iliyosajiliwa kwenye orodha ya makampuni ya kuuza hisa DSE na Julai 15, mwaka jana ilipewa kampuni mbiu ya 'Kampuni ya Wazawa'.

Kwa mujibu wa tangazo kwa umma ambalo gazeti hili ina nakala, DSE licha ya kuisimamisha NICOL kwa kipindi hicho, pia imetishia kuifuta katika orodha ya makampuni yanayopaswa kuuza hisa kwenye soko hilo endapo itashindwa kutoa na kuwasilisha vielelezo kwa maelekezo iliyopewa.

Kwa mujibu wa DSE, NICOL iliwasilisha taarifa kwenye soko hilo, ikionyesha kuwekeza fedha kutoka vyanzo mbalimbali, ikiwemo kiwanda cha Inter-chem Pharmaceuticals& Beverages Ltd (IPBL) na Tanzania Fisheries Development Co.Ltd (TFDC).

Hata hivyo, ilibainika kwamba, IPBL ni moja ya kampuni ambayo iliwekwa katika orodha ya kupigwa mufilisi.

"Baadaye DSE ikaelekeza NICOL ieleze umma mambo matatu, kuhusu athari za mufilisi wa IPBL katika thamani halisi ya mali za kampuni hiyo ya taifa," inasema sehemu ya tangazo hilo.

NICOL pia ilitakiwa kueleza, endapo ikitokea kuwepo kwa madeni au kupata msukosuko wa kifedha, ina mpango gani wa kunusuru hali hiyo.

"Hata baada ya kukumbushwa na DSE, bado NICOL ilishindwa kutoa taarifa kwa umma kwa wakati husika," inasema sehemu ya tangazo hilo.

Kwa mujibu wa DSE, Baraza la Uongozi la DSE katika mkutano wake wa kawaida wa 43, uliotishwa Agosti 21, 2009, ilijadili taarifa ya NICOL na kubaini kwamba ilishindwa kutimiza maelekezo hayo.

"Kwa hiyo, Baraza lilikubali kuisimamisha NICOL kutoka katika orodha ya kuuza hisa kwa kipindi cha mwezi mmoja kutoka siku hiyo ya Agosti 21, 2009.

"Baraza pia limeagiza NICOL katika kipindi hicho ambacho imesimamishwa, ifanye mambo ambayo ilielekezwa awali," inasisitiza sehemu ya tangazo la DSE.

Mambo mengine, NICOL pia inapaswa kueleza uzalishaji halisi wa sasa wa makampuni hayo, mawili ya IPBL na TFDC, ikilinganishwa na matarajio yake ya awali.

DSE pia imeagiza NICOL kuwasilisha tena taarifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, ambayo iko katika viwango vinavyotambuliwa kimataifa na IFRS ikiwa pia ni maelekezo ya Soko la Mitaji na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu.

Katika maagizo hayo, NICOL pia inapaswa kuwasilisha uthibitisho wa wakurugenzi wake wenye umri wa miaka zaidi ya 70 na ustaafu wao, kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002.

NICOL pia inapaswa kuonyesha timu ya menejimenti na wataalamu wake, wenye uzoefu wa kuendesha makampuni ya uwekezaji.

"Endapo NICOL itashindwa kutimiza maelekezo yaliyotolewa hapo juu, itasababisha Baraza la Uongozi la DSE kuifuta kutoka katika orodha ya kumbukumbu zake," ilieleza sehemu ya tangazo hilo. NICOL ilianzishwa kwa mgongo wa Kampuni ya Uwekezaji ya Wazawa, lakini miaka ya karibuni imekuwa kimya kutoa taarifa kwa umma.
July, 2011

Kampuni ya NICOL (Tanzania Investments Comopany Ltd) imeondolewa (delisted from) DSE (Dar Es Salaam Stock Exchange) kuanzia tarehe 6 July 2011. Kwa mujibu wa press release ya DSE, "The DSE wishes to inform the public that as per DSE Governing Council directive issued on 31st May, 2011, the National Investments Company Limited (Nicol) has been delisted from the DSE, effective 6th June 2011."

Tangazo la DSE halitoi sababu kuindoa Nicol kwenye soko la hisa, lakini kuna taaifa kuwa kampuni imeshindwa kuzingatia majukumu yake kwenye soko la hisa. Kampuni hajapeleka audited financial statements tokea mwaka 2009!! Pia Nicol imekuwa ikifanya maamuzi bila kupata a "go ahead" toka DSE kama inavyotakiwa na kanuni za soko la hisa. Mojawapo ni kitendo cha Nicol kuuza hisa ilizokuwa nazo NMB bila kuruhusiwa na DSE.

Nicol itabidi itume maombi tena upya ikiwa ni pamoja na kuandaa prospectus kama kampuni mpya. Hata hivyo, bodi ya wakurugenzi imesimamishwa na CMSA (Capital Markets and Securities Authorities). Kabla ya kuondolewa kampuni ilikuwa ime-list jumla ya hisa 69.178 million.


Kuna mtu yoote aliye kuwa amenunua hisa za hii kampuni?
 
Ikena

Mkuu naona umeingia wasiwasi, sifahamu vizuri perfomance ya hisa za NICOL lakini sijapata tetesi ya kuteleleka kwake kwenye soko! Hivyo kama umejaribu kudispose hisa ulizonazo na hupati mteja, inaweza kuwa na sababu nyingi tu not necessary ikawa thamani yake imeshuka, kwa mfano inaweza kuwa watu wanaisikilizia hii Financial crisis kama itakuwa na madhara kny makampuni na ya hapa kwetu, so wako reluctant kuachia cash au broker unayemtumia si mzuri kumake deals pale DSE au zipo hisa chache sana zinazouzwa sasa (pengine za kwako tu) na watu wanataka nyingi kwa mkupuo mmoja etc

Nakushauri mtumie broker mzuri kwa ushauri na kuuza hisa zako hope utafanikiwa!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naona umeingia wasiwasi, sifahamu vizuri perfomance ya hisa za NICOL lakini sijapata tetesi ya kuteleleka kwake kwenye soko! Hivyo kama umejaribu kudispose hisa ulizonazo na hupati mteja, inaweza kuwa na sababu nyingi tu not necessary ikawa thamani yake imeshuka, kwa mfano inaweza kuwa watu wanaisikilizia hii Financial crisis kama itakuwa na madhara kny makampuni na ya hapa kwetu, so wako reluctant kuachia cash au broker unayemtumia si mzuri kumake deals pale DSE au zipo hisa chache sana zinazouzwa sasa (pengine za kwako tu) na watu wanataka nyingi kwa mkupuo mmoja etc

Nakushauri mtumie broker mzuri kwa ushauri na kuuza hisa zako hope utafanikiwa!


Mkuu sidhani kama crisis hii ipo kwenye nico pekee, ukiangalia masoko mengine ya hisa yanakwenda vizuri.
Hapo DSE ndio hawazipokei kabisa, na wanadai tangu mwezi wa 8 hazinunuliki kabisa, na thamani inazidi kushuka.

Sasa ndio ndio nauliza tutakuwa tumeliwa @ the end of the day ama vp?
 
Mkuu sidhani kama crisis hii ipo kwenye nico pekee, ukiangalia masoko mengine ya hisa yanakwenda vizuri.
Hapo DSE ndio hawazipokei kabisa, na wanadai tangu mwezi wa 8 hazinunuliki kabisa, na thamani inazidi kushuka.

Sasa ndio ndio nauliza tutakuwa tumeliwa @ the end of the day ama vp?

Ikena,

Ndo maana nikasema itabidi uwaone watalaam wa stock exchange kama kina Orbit, Solomon etc wako wengi sana, watakupa ushauri wamaana zaidi!

Ila kama umeona thamani ya hisa za NICOL pale DSE zinashuka is true kwamba thamani ya uwekezaji wako inapungua as well, yaani unapata hasara...lakini haya mambo huwa yanatokea itabidi uvute subira zianze kupanda tena ili uweze kuziuza kwa faida, ukiuza sasa (kama utafanikiwa) utapata hasara!

Angalia kama hawa jamaa wa TOL, hisa zao zilikuwa down kama kwa miaka mitatu hivi consecutively, lakini baadaye zilianza kuwa stable tena!

Hiyo ndo business mkuu...ups and downs huwa zipo!
 
Kila nikitaka kuuza hisa zangu naambiwa haziuziki, sasa ndo kusema nimeliwa au nivute subira??

Sasa kwanini wasiturudishie fedha zetu kabla hisa hazijazidi kushuka thamani zaidi??
Ivi nitawezaje kupata fedha zangu iwapo kampuni hii itaingia mitini?

Naombeni mchango wenu wa mawazo.

Kuuza hisa mpaka upate mtu wa kumwuzia, kwa DSM nadhani wanunua hisa sio wengi sana labda ndo maana unapata shida kuziuza, pia labda wanunuzi wanaamini bei yake ni kubwa kuliko inavyotakiwa kuwa.

Sijui ni nani unataka akurudishie hela, kampuni hailazimiki kununua hisa zake kama mtu anataka kuziuza, labda waamue wenyewe.

Kushuka kwa thamani ya hisa na hata kampuni kufilisika ni moja ya risk za kununua hisa. Kampuni ikifilisika ndo umekula hasara kabisa, kwa sababu shareholders wanakua wa mwisho kufikiriwa kwenye kugawa mali za kampuni.

Note: Sijui anything specific kuhusu NICOL!!
 
Hata mimi ukiniambia ninue share za NICOL kwa sasa nitasita-- afadhali ninunue za Viwanda vya Cementi au Bia.. maanke watu wanakunywa bia na kujenga kila siku
 
Ikena kwa kweli Hisa za nikola kwa sasa hivi huwezi kuuza hata ukimtumia broker wa namna gani watu kila siku wanalalamika ziko kwenye Q tangu october hazijanunuliwa na wahusika hawajatangaza gawio na bei yake imeshuka sana sasa hivi ni sh,285/= kuhusu swala la wewe kupata hasara sijui labda usubiri kupata gawio lakini swala la kuuza sahau.

Mimi nafanya kazi huko hisa za tol, nicol, dcb sasa hivi hazina soko kabisa na nmb zinashuka kabisa japo wametangaza gawio la sh, 30 ni kwa wale wenye hisa nyingi ndo watapata faida wale wenye hisa kidogo bora wauze tu kwa bei iliyopo ya 900 maana zimeover supply na bei itazidi kushuka.
 
Ikena kwa kweli Hisa za nikola kwa sasa hivi huwezi kuuza hata ukimtumia broker wa namna gani watu kila siku wanalalamika ziko kwenye Q tangu october hazijanunuliwa na wahusika hawajatangaza gawio na bei yake imeshuka sana sasa hivi ni sh,285/= kuhusu swala la wewe kupata hasara sijui labda usubiri kupata gawio lakini swala la kuuza sahau.

Mimi nafanya kazi huko hisa za tol, nicol, dcb sasa hivi hazina soko kabisa na nmb zinashuka kabisa japo wametangaza gawio la sh, 30 ni kwa wale wenye hisa nyingi ndo watapata faida wale wenye hisa kidogo bora wauze tu kwa bei iliyopo ya 900 maana zimeover supply na bei itazidi kushuka.
Dada Joyceline vipi kuhusu hisa za TWIGA hali ikoje? Nina vi hisa vyangu huko na kwa sasa niko nje ya nchi.
 
Samahani, naomba niulize hivi NICOl imeorodheshwa katika soko la hisa au bado ni over the counter kama CRDB?

Maana kama ni OTC basi hawawezi ku-deal nazo madalali wa hisa, inabidi mkuu usubiri mpaka ikiorodheshwa katika soko la hisa ndo uweze kununua na kuuza.

Kama imeorodheshwa basi ni lazima wanahisa mpewe taarifa.

lakini kama una mashaka yoyote kawaone CMSA - wako PPF wakupe information zaidi.
Asante
 
Susuviri

Wao walijiadvertz kuwa wanampango wa kujiunga DSE baada ya kuchukua machinjio ya Dodoma, sina uhakika kwasasa kama washajiunga.
 
Last edited by a moderator:
Kuuza hisa mpaka upate mtu wa kumwuzia, kwa DSM nadhani wanunua hisa sio wengi sana labda ndo maana unapata shida kuziuza, pia labda wanunuzi wanaamini bei yake ni kubwa kuliko inavyotakiwa kuwa.

Sijui ni nani unataka akurudishie hela, kampuni hailazimiki kununua hisa zake kama mtu anataka kuziuza, labda waamue wenyewe.

Kushuka kwa thamani ya hisa na hata kampuni kufilisika ni moja ya risk za kununua hisa. Kampuni ikifilisika ndo umekula hasara kabisa, kwa sababu shareholders wanakua wa mwisho kufikiriwa kwenye kugawa mali za kampuni.

Note: Sijui anything specific kuhusu NICOL!!


Sidhani kama bei ni kubwa, nimegundua kampuni haina mvuto na niliuvaa mkenge
 
Sidhani kama bei ni kubwa, nimegundua kampuni haina mvuto na niliuvaa mkenge

Pole Ikena, ndiyo bongo land ilivyo.
Waambie wazee wa uzawa (Mengi, Idd Simba, Felix na wenzao wengine) wakupe jibu.

Tanzania ni kulizwa kwa kwenda mbele. Ukigeuka kulia unalizwa na wazee wa uzawa ukigeuka kushoto unalizwa na wazee wa vijisenti na richmonduli, ukiangalia makaratasi unalizwa na waandishi ukiangalia juu unalizwa na mzee wa mahujaji (Mattaka na Atcl yake). Hiyo ndiyo Tanzania bwana kula uliwe.
 
R mashuri hisa za kununua kwa sasa ambazo huwezi kupata hasara ni TBL, TTC, TWIGA CEMENT, TANGA CEMENT TATEPA NA EAST AFRICA BREWERIES
 
R mashauri: Twiga kwa sasa ni sh. 1600 mpaka leo sasa sijui mpaka hiyo siku utakayouza kutakuwa na badiliko lolote
 
Sidhani kama bei ni kubwa, nimegundua kampuni haina mvuto na niliuvaa mkenge

Namaanisha bei ni kubwa ukifananisha na kiasi ambacho watu wako teyari kulipa, nina uhakika ukiamua kuuza at a big loss kuna mtu atanunua. Yaani hakuna uwiano kati ya supply na demand.

Labda jaribu kuangalia long term, kama unaamini campuni itafanya vizuri baadae basi kaa nazo, otherwise uza for a loss.
 
Biashara ya hisa siku zote ni mchezo wa wakubwa, yaani watu wenye mipesa mingi. Kwa watu wadogo wadogo, ujanja huwa ni kwenye Initial Public Offer (au IPO). Unanunua halafu zikianza kuuzwa immediately unauza usisubiri. Ukisubiri dividend mara nyingi huwa ni amount ndogo sana.

Taratibu na sheria za masoko au uendeshaji wa biashara unatoa nafasi ndogo sana kwa wamiliki. Wameliki wenye mkono katika uendeshaji ndo wanafaidika. Wamiliki wadogo wadogo kama wewe mnakuwa watu wa mwisho kufikiriwa. Kwa mfano kampuni likitengeneza faida, makolokolo yooote hukatwa, kiwango kinachobaki ndo hulipwa kama gawio kwa wenye hisa. Waendeshaji hawalazimiki kulipa gawaio na mara nyingi huwa wanazua visa kibao kama uwekezaji, n.k. ili kuacha kulipa gawio. Gawio hata likilipwa inakuwa kigogo mno kiasi cha kuleta tofauti yoyote kwa mwenye hisa chache. Kampuni ikifirisika wenye hisa ni watu wa mwisho kufikiriwa na mara nyingi hawaambulii chochote na sheria na taratibu zinaruhusu hilo.

Maana yake ni kuwa kujiingiza kwenye soko la hisa inabidi uwe na fedha za kutosha kukuwezesha kuingilia utendaji wa kampuni. Vinginevyo ni sawa na kucheza chekundu na cheusi. Outcome mara zote huamliwa na mchezeshaji anaweza kuruhusu ule, au uliwe tuu. Waendeshaji wa makampuni (wenye shea nyingi) huwa wanaamua watoe gawio au wasitoe. Wao wanazo jinsi nyingi za kupata fedha yao kupitia michakato mbali mbali ya uendeshaji wa makampuni.

Kwa hiyo kabla ya kununua hisa kitu cha kwanza unachotakiwa kujiridhisha nacho, ni uendeshaji wa kampuni. Hiza kama za NICOL kwa kweli ilikuwa ni kama mchezo wa karata tatu. Hivi ulikuwa unajua NICOL inafanya biashara gani in the first place? Ulikuwa na uhakika wa jinsi inavyoendeshwa? Sasa hivi rekodi yao ya utoaji wa gawio ndo itakayofanya share zako zinunuliwe au zisipate mnunuzi. Ikiwa kampuni haieleweki eleweki, hakuna atakayekuwa tayari kununua share hizo kwa sababu hiyo hali ya kutoeleweka eleweka inaongeza kitu ambacho kinaitwa RISK.

Wanaojua biashara za hisa hawawezi kununua hisa zenye RISK KUBWA ikiwa hazina mapato makubwa!! Hiyo ndo kanuni ya masoko ya hisa.

Hisa zako zisiponunuliwa mwambie dalali wako ashushe bei. ikiendelea kushuka itafikia kiwango ambacho wale wenye hisa nyingi au wanaoendesha kampuni wataamua kuzinunua za kwako kwani kuendelea kushuka kwa bei za hisa kunashusha thamani ya kampuni.
 
Kipimapembe, u have some valid points ila kumbuka mkuu, watu waliokuwa wana-back NICOL walikuwa ni watu wazito sana kama vile Felix Mosha nadhani hata Mengi yumo, sasa wananchi lazima watawaamini.
Kwanza unafahamu kuwa neno risk kwa maana yake halisi halipo katika vocabulary ya Kiswahili, sasa utamweleza vipi mwananchi wa kawaida kuwa share fulani ina risk?
 
Hilo ni kweli kuwa RISK watu wengi hawaelewi ni kitu gani. Lakini ndo hivyo kwenye masoko ya mitaji RISK MARA nyingi haiwezi kuhesabiwa with absolute certainity. Hata marekani watu bado wanaliwa kwenye hisa. Fikiria kina Madoff!!! Kwetu sisi hii ndo nafasi ya watu kujifunza. Lakini ukikumbuka TOL imewala sana watu na share zake. Watu hawakujifunza kwa TOL??

Wanunuzi wadogo wadogo kwenye hiki kinachoitwa masoko ya mitaji siku zote ni kama dagaa. Samaki woote wakila wakashiba dagaa hubaki. Kinachowafanya waendelee kuwepo ni wingi wao tuuu. Lakini ukweli halisi hawafaidiki na chochote.

Vivyo hivyo kwenye soko la mitaji. Tena kwa nchi maskini kama yetu ambayo hata serikali ni rahisi kununuliwa, you can't trust soko la mitaji. Watu inatakiwa wajue kuwa hakuna fedha ya dezo. Hakuna mtu atakayefanya kazi halafu mwisho wa mwaka akulipe kitita.

Ni afadhali tuzame katika SME kuliko kuwaingiza watanzania kwenye hili gubeli linaloitwa soko la mitaji. Ukiwa na vimilioni vyako vitano, sita, au ishirini ni afadhali ufungue kibiashara chako na ukisimamie. Ukiwekeza kwenye soko la mitaji ni sawa na kuipoteza kwani hiyo ni kuwapa gawio wenye mipesa mingi.

Watu wakishaliwa sana, hatimaye watajua. Of course ujinga huwa ni kitu muhimu katika masoko ya mitaji, huwa wakati mwingine share zinapanda bei sana hata kama hakuna cha maana. Hapo ndo wajanja wanakulaga bingo, halafu wengi wanazamishwa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom