Elections 2010 Serikali: Walioachana mswada wa mapitio ya Katiba Zenji Wahuni

... tena ni wa CCM kwa maslahi yao kwani ndio wanaofaidi.
Hapa tusiwatetee upinzani. Hata upinzani, mfano CHADEMA, hawajawahi kutangaza openly and forthrightly kwamba hawataki Muungano. Na kwa Zanzibar, wa kina Muhamed Rashid wa CUF nao sijawasikia kutangaza hawataki Muungano. Wanafaidika nao binafsi.

Kwa hiyo, sio CCM peke yake wanaong'ang'ania Muungano.
 
Samia, kikwete, na mafisadi wenzao wote ndio wahuni. Haki ni haki bila kujali ni nani anaitetea. Imam alikuwa sahihi kuuchana muswada kwa sababu ni wa kihuni na waliouandaa wote ni wahuni tu.
Hata kama muswada ni wa kihuni kwani hawezi kutumia njia za kistraabu, wanapokataa maandamano ya Chadema wakati wao wanafanya vituko vya aibu hata mimi ningemuita mhuni, Imam mzima tena kiongozi wa waislam anafanya hivyo je anaowaongoza.
 
asilimia 4.5 kwa zanzibar ni kubwa sana ukizingatia uwiano wa idadi ya watu. kama watu 1m wanapata 4.5% na watu 43m wa nchi ileile wanabaki na 95.5% tu, kwa kweli hiyo si haki kabisa

halafu hilo la kudhaminiwa na serikali ya muungano, maana yake nchi ya zanzibar ikikataa kulipa, itailazimu nchi ta tamzania (bara) kubeba mzigo huo! hapa nahisi matope yalichukua nafasi ya ubongo ndani ya vichwa vilivyofikia uamuzi huu. kwa kweli maamuzi kama haya ndiyo yataharakisha kuvunjika kwa muungano huu

mwisho sio sawa kwa waziri kuwaita wote wasiokubaliana na mawazo yake, ya chamachake na ya serikali yake kuwa ni wahuni. hapo anapaswa kuomba radhi kwa wazanzibari wenzake.

huyu mama kama sikosei alichaguliwa kuwemo kwenye CC mpya ya ccm, kwa msingi huu, naamini ccm haijajivua gamba bado

Wengine wanachekesha kweli? Yaani unagombania msaada wa mtu mwengine? Na hili la kutowa dhamana maana yake nini, na Tanganyika wanafanya hivyo?
 
hawana shukrani kabisa hawa, ni sawa na kumsaidia mtu kisha anakutukana. huu muungano ni product ya cold war, una manufaa kwa wazanzibari kuliko watanganiyika. muungano wa hovyo kuliko yo yote iliyopo duniani.


Shukurani kwa pesa za msaada unaoomba kwa jina la wotee. Mbona wasomi nyie mnachekesha sana. Lau ingekuwa pesa zenu basi hata sijui maneno yangekuwaje?
 
Angesema hayo mwingine tungesikia 'matamko' toka kila kona. Lakini kwa sababu ni 'mwenzetu' kuko kimyaaa! Atueleze 'hao wahuni' ni raia wa wapi.

Hayo ni maoni yake lakini kwa Wazanzibari tunajuwa muhuni yeye na mambo yake!
 
Muhuni ni yeye huyu samia suluhu hassan,analewa,anafanyiwa viLE VILE,muangalieni muslamu gani anatembea kichwa wazi,kwa uwislamu tunakuita wewe muhuni,,,kudadadekiiii

Tuombe radhi tafadhali zako,hapa huru sheik wetu tumeunga nae pia muhuni ? Viongozi wetu pia wahuni ? WEWE Takecare ohooo

Akija zenji ndo anajidai kujifanya kujistiri akija bongo kumbee ndo hivyoo mara unamuona kwa macheniiiView attachment 27236

Hana Stara yoyote mwanmmke anaemwendea mumewe kinyume kwa tamaa ya ukubwa!
 
Huo ni ukweli usiopingika. Kwa nini bara ing'ang'anie kuwabeba watu hao wasiothamini fadhila wanazozipata kutoka bara? Muungano uvunjike tu kwa sasa ili wajitegemee na wapate kuonja joto la jiwe kutokana na ubaguzi wao ambao naamini utawatafuna wao kwa wao.

Mimi elimu yangu ya madrasa inanifanya nikuone kuwa pengine elimu dunia yako haijakusaidia. Shukurani gani iwapo hizo pesa ni za msaada? Huo msaada unapoombwa unaombwa kwa jina gani na unakusudiwa nchi gani? Tuwe wa wazi kama siku zote tunakataa kuwa Tanganyika sio inayofaidi Muungano huu sasa inakuwaje pesa zilizotolewa kwa Tanzania mzifanye kuwa zenu (Tanganyika)

Ama kweli kwenye malalamiko mnajidai Tanganyika haipo lakini kwenye maslahi tunapigana mafungu kati ya Zanzibar na waliobakia (sijui nani tena kama si Tanganyika)
 
Hamad Rashid acha ubaguzi
Nyerere united Tanganyika with impurities(islies),leo mmekuja na udini uku bara mnatuchefua jamani nyie CUF.

The last resort regardless CDM or CCM ni udini. Kwani mlipoamuwa kutukumbatia mlikuwa hamjui kuwa tuna Dini tofauti na nyie msiyonayo?
 
Sie bara hatuna neno Adui,nyie ndo mna Upemba na U-unguja,karibu kwetu kiwanja utapata mkuu,mke utapata n.k hatubaguani na hatutabaguana kamwe.Nchi nyingi zinawaza unification wewe unawaza separation.
Duh na vile vita vya makabila ni kofi la mahaba?
 
nyie wenzetu wasunni hamuijui uislamu na mnataka kudandia dandia tu treni. Kwani kuvaa kibarakashee ndoo uislamu!! Au kuvaa kanzu ndio tija. Kanzu sio vazi la kiislamu ni vazi tu la waarabu ambao kuna wakristo na wasio kuwa na dini. Ndio maana wengine wanadhani kuvaa hijabu ni vazi rasmi ambayo dini yetu imetoa ktk koruani. Na wako tayali kupigana sabab ya hilo. Huo ni upotoshaji jamani. Kasome tena ndugu yangu
masalaama

Hebu tuelekeze wapi tukasome ambako kumeruhusiwa mwanamke asijifunike nywele zake? Kama Dada powa pia tuko Waislamu powa tunaoikejeli misingi ya dini kwa kutaka kuonekana tu watu wa sasa!
 
Hata kama muswada ni wa kihuni kwani hawezi kutumia njia za kistraabu, wanapokataa maandamano ya Chadema wakati wao wanafanya vituko vya aibu hata mimi ningemuita mhuni, Imam mzima tena kiongozi wa waislam anafanya hivyo je anaowaongoza.

Hana kosa kwa mujibu wa dini yake! Amejipima akajiona ana uwezo wa kuondoa mabaya kwa mkono wake! Tusioweza basi tunachukia moyoni na wala hatuwasaliti wenzetu kama alivyofanya suluhu!
Hata hivyo kwa CHADEMA hukohuko Zanzibar wameuchoma moto. Wahuni ni wengi si kidogo kama alivyofikiria Samia Suluhu!
 
Huku ni kukosa kazi, dunia nzima wanatafuta namna ya kuungana nyie mnazungumzia kutengana, hivi mpo dunia gani hiihii au? Watu tunafikiria east african federation na baadaye united states of africa nyie mnafikiria zanzibar kujitenga, mmepitwa na wakati.Kwa hilo halitawezekana,kwa nini turudishwe nyuma kwa ajili ya uroho wa madaraka wa watu wachache?
 
Samiha yeye ndio muhuni na mnafiki analinda kazi yake na mabilioni ya pesa alizopatiwa na CCM kwa mpango wa kufanya kampeni za kuendeleza muungano udumu wakati anajua ukweli na agenda ya wazanzibari kuwa 90% hawautaki tena muungano huu.

serikali ya CCM bara vile vile wanajua kuwa imefikia wakati huu mpaka wa Tanganyika na wao wamesha choka na stori hizi za Muungano fake!!!

Muungwana Wakati ni huu Tunaitaka Tanganyika yetu
Wakati tukiwa na Raisi Kikwete ambae yeye ndie aliekuwa mpiganiaji wa jambo hili alipokuwa akisota bungeni ,kinachohitajiwa ni kusituliwa tu na kuambiwa ule wakati ndio huu.
Tunaitaka Tanganyika.
Tunataka kufuta kasoro za Muungano.
Tunataka Raisi wetu.
Tunataka Bendera yetu.
Tunataka Serikali Tatu.
1 ) Mkataba wa Muungano, 1964, ulitoa sura ya kuwepo kwa shirikisho la serikali tatu ambapo hapangekuwa na serikali moja iliyo na mamlaka makubwa kushinda nyingine.

2 ) Mkataba wa Muungano ulitaka kuwepo kwa serikali tatu au mamlaka ambazo zingeundwa kiuunganishi ambazo katika waraka huo zilitajwa kuwa ni mmoja wa mamlaka kuwa ni Tanganyika, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano.
Hicho kifungu hakikuitaja CCM na wahafidhina wake kuwa ndio wamiliki wa nchi mbili hizi hivyo inatakiwa kutojihusisha kabisa na madai na kujifanya wao ndio walindaji wakubwa kumbe ni mafisadi wakubwa.

3 ) Serikali ya Muungano unapoilinganisha na kuipima na Zanzibar au Tanganyika ambayo haipo, ni salio la uzawa wa nchi hizo na haiwezi kuwa na mamlaka yake wenyewe, isipokuwa kwa yale mamlaka iliyomegewa. hapa kunaifanya Zanzibar iwepo kama Nchi yenye maamuzi yake na Tanganyika haina.

Sasa ni mfumo wa Vyama vingi na hivyo hivyo ili mambo yaende sambamba kunahitajika serikali nyingi , kwa vile Muungano wetu unashirikisha nchi mbili kunahitajika serikali Tatu , ili kuvutia nchi nyengine nazo ziweze kujiunga ,jirani zetu wanataka kujiunga lakini wazo la kupoteza serikali yao ndio kikwazo kikubwa naamini kabisa ikiwa tutaamua kuweka serikali Tatu basi Muungano huu utakuwa na kuzivutia nchi nyingi jirani na hivyo kuweza kupata East African Block.
Hivi tujiulize kama Burundi atataka kujiunga na Muungano wa Tanzania atatakiwa afanye nini ? Na tutazame mfano wa European countries how they manage to get on top of their union na kuifanya fedha yao kuwa juu kuliko dola.
Leo Tunajulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania japo siku hizi neno Muungano limeondolewa kinyemela nyemela na Chama tawala ambacho kimejitangazia kushika hatamu ,sasa ukiangalia kuna Muungano wa East Africa
,imewezekanaje kuwepo kwa Muungano huo wakati ndani yake kuna nchi mbili nazo zina Muungano ,ndio nikasema huu Muungano tulio nao sio sahihi kwa hapa tulipo ni lazima kuwepo na Tanganyika ili kuweka sawa mambo ya Muungano kwa eneo zima la East Africa.​
 
Msimamo wa CUF kuhusu Muungano unaeleweka tokea Chama kinaanzishwa na wala hatuhitaji Hamad Rshid au kiongozi mwengine aseme, nao ni mfumo wa Serikali tatu.

CCM nyie mnasema Serikali mbili kuelekea moja. Hili halitawezekana kamwe kwa Zanzibar.

Nakubali kabisa kuwa wako viongozi (wa pande zote) wanaofaidi lakini overwhelming majority hawakubali set up ya Muungano ulivyo sasa.

Nimesema CCM kwa sababu wao ndio wanaoshika nguvu za Dola kwa sasa na wengi wao hawataki kubadilika.
 
Hili neno Che. Ni kweli kabisa maneno yako. Hebu tujiulize, Zanzibar inasemewa na nani katika EAC kwa mambo yasio ya Muungano?
 
Back
Top Bottom