Serikali: Tunawajengea uwezo wakulima kuuza nje matunda

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
David%20mathayo%283%29.jpg

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. Mathayo David.



Serikali imeanza kuandaa mazingira maalum ya kuwajengea uwezo wakulima ili waweze kuuza matunda wanayozalisha katika soko la nje.
Akijibu swali bungeni, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. Mathayo David, alisema miradi hiyo ni pamoja na mradi wa kuendeleza uzalishaji na masoko ya mazao ya ndizi katika mikoa ya Kagera na Kigoma.
Alisema Wizara kwa kushirikiana na mfuko wa pamoja wa bidhaa za kilimo na Chama cha Wakulima wa maembe katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Lindi, wameweza kusambaza kwa wakulima jumla ya miche bora ya miembe 27,500.
“Lengo la mradi ni kuzalisha miche bora 47,000 ifikapo 2010/2011.
Aidha Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), tumeweza kuendeleza kilimo cha maparachichi bora kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi katika mikoa ya Mbeya na Iringa,” alisema Dk. David.
Dk. David alikuwa akijibu swali la mbunge wa Chakechake (CUF), Fatma Maghimbi, aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kujenga mazingira ya kuwawezesha wakulima kusafirisha matunda nje ya nchi.
Katika majibu yake, Dk. David alisema Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikishirikiana na Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko na wadau wa mazao nchini wameanzisha Baraza la kuendeleza mazao ya matunda.
Alisema Baraza hilo linahusika katika kuandaa na kuratibu utekelezaji wa mazao ya bustani kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wakulima wanapata masoko ya uhakika ya mazao yao ndani na nje ya nchi. Alisema Serikali pia imekuwa ikiainisha aina ya matunda na ubora unaotakiwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili kuwapatia wakulima vipando bora.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom