Serikali, Tunaomba Majibu ya Matibabu ya Loliondo

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Babu wa Loliondo katutingisha sana. Serikali yote ilihamia Loliondo kunywa kikombe. Wabunge walitiririka, raia wa kawaida tukaamini kwamba Tulipata ukombozi wa Kiafya. Kila mtanzania angeyapata haki yao ya kimsingi. Baada ya muda kupita sasa, tunaomba serikali yetu tukufu itupe majibu au ripoti ya uchunguzi kuhusu tiba ya babu wa Loliondo. Watanzania tumechoka kudanganywa na kuibia. Serikali ya CCM tunaomba majibu
Mwasapile.jpg
 
Sawa uliyosema,lakini! Kwanini umetengeneza picha ya mvuta bangi ukaweka kichwa cha babu wa loliondo? Unania ya kutuambia nini juu ya picha hiyo yakuunga mwili wa mtu mwingine na kichwa babu wa loliondo?
 
Wadau JF, naomba kwa yeyote anayejua nini kilitokea hadi serikali kumpa promo BABU WA LOLIONDO wakati ikijua kuwa alikuwa hatibu kama ilivyokuwa ikipiga promo. Na je kama leo serikali inaweza ikakili adharani kuwa ilifanya makosa na kama itakuwa tayari kuwalipa wale waliopata madhara ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha kwa kuwa ni wao walioaminisha UONGO HUO. Mwenye kufahamu ukweli kuhusu huyu BABU tafadhali atujuze maana mimi naamini ilikuwa MBINU CHAFU ZA SERIKALI DHAIFU na ni ushaidi wa kuwa hatuna huduma bora za afya ndiyo maana wakawambia wananchi waende kwa babu kwa kuwa wao hawana uwezo wa kutoa huduma bora. Ni mtizamo wangu juu ya huyu babu na serikali DHAIFU, tubadilishane mawazo tafadhali.
 
Nilikuwa nawashangaa sana waliokuwa wanakwenda kwa babu wa loliondo. Kipindi kila mtoto wake wa kumzaa alifariki kwa ugomjwa wa Malaria! NIMR wakakimbizana kupima ule mti wakaeleza mambo meeengi, kuwa inatibu Kisukari! Ni ujinga tu!
 
Niliwahi kusema hapa JF lakini nikapuuzwa lakini sasa wanaona jinsi ilivyo! Huu ni ushetani na unyama! Watu walisema walifunuliwa DECI na babu akasema amefunuliwa,ipo siku ataibuka mchungaji au askofu aseme amefunuliwa kuwa ushoga halali na ndoa hizo za ibilisi zifungwe kanisani!
 
Mkuu jamaa naweza kusema ana akili ya hali ya juu, he managed to fool millions of Tanzanians na mpaka sasa anadunda.
 
Babu wa Loliondo yalikuwa ni matokeo ya kutoboresha hospitali zetu
na kuwafanya wananchi kujaribu tiba mbadala...
 
Wadau JF, naomba kwa yeyote anayejua nini kilitokea hadi serikali kumpa promo BABU WA LOLIONDO wakati ikijua kuwa alikuwa hatibu kama ilivyokuwa ikipiga promo. Na je kama leo serikali inaweza ikakili adharani kuwa ilifanya makosa na kama itakuwa tayari kuwalipa wale waliopata madhara ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha kwa kuwa ni wao walioaminisha UONGO HUO. Mwenye kufahamu ukweli kuhusu huyu BABU tafadhali atujuze maana mimi naamini ilikuwa MBINU CHAFU ZA SERIKALI DHAIFU na ni ushaidi wa kuwa hatuna huduma bora za afya ndiyo maana wakawambia wananchi waende kwa babu kwa kuwa wao hawana uwezo wa kutoa huduma bora. Ni mtizamo wangu juu ya huyu babu na serikali DHAIFU, tubadilishane mawazo tafadhali.

Wewe jina lako ni njaa mbaya, haikosi njaa yako imekufanya uwe umetumwa. Kweli njaa mbaya!!!
 
Babu ni mjasiriamali, ni mbunifu,amebuni mradi wake na sasa yuko poa. Tatizo wabongo ni wepesi kudanganyika,ndiyo maana CCM pamoja na udhalimu na ufisadi wake bado iko madarakani. Kwa jinsi CCM ilivyo ifisadi nchi hii na wabongo wangekuwa hawadanganyiki ingekuwa kila anapoonekana kiongozi wa CCM angepigwa mawe kama nyoka anavyopigwa kila aonekanapo machoni pa binadamu. Kuinuka kwa babu wa Loliondo ni UDHAIFU wa serikali ya CCM.
 
Niliwahi kusema hapa JF lakini nikapuuzwa lakini sasa wanaona jinsi ilivyo! Huu ni ushetani na unyama! Watu walisema walifunuliwa DECI na babu akasema amefunuliwa,ipo siku ataibuka mchungaji au askofu aseme amefunuliwa kuwa ushoga halali na ndoa hizo za ibilisi zifungwe kanisani!
God forbid!!!
 
Kwa nini bado hawajampandisha kizimbani kwa mauaji na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu?
 
Njaa Mbaya, unaposema serikali ilimpa promo unamaanisha nini? Na kwamba serikali ilikuwa inajua fika kuwa dawa haitibu? Umeshapitia document ya Muhimbili hospitali (najua ipo Fikra Pevu)? Muhimbili walisema kuwa ule mti una 'medicinal character' lakini hakuna ushahidi kuhusu dose sahihi na kama inaponya magonjwa yaliyotajwa. Baada ya hapo sidhani kama serikali ilifanya zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kama serikali yako inathubutu kusema hakuna vifo vya ziada vilivyotokea kutokana na mgomo wa madaktari, utasemaje kuwa babu amesababisha vifo na kujikusanyia pesa kwa udanganyifu?
Kwa nini bado hawajampandisha kizimbani kwa mauaji na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu?
 
Back
Top Bottom