Serikali tumia muda huu kupanua barabara Tageta-Bagamoyo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,593
8,734
Kwasasa barabara ya Mwenge-Tegeta inapanuliwa ingekuwa nafasi nzuri ya serikali kutafuta pesa au wahisani wa kupanua barabara ya Tegeta-Bagamoyo kwani itapunguza gharama. Sasa ni wakati wa ujenzi na ndiyo muda mzuri wa kupanua barabara badala ya kungojea kipande kimoja kiishe halafu baada ya mwaka moja tunafunga barabara tena kupanua kipande kingine. Imefika wakati wa Tanzania wa kufikiria mbali badala ya kufikiria kutatua matataizo kwa kupuliza kila siku!! kila mtu anajua barabara inatakiwa kupanuliwa mpaka Bagamoyo sasa ni kwanini wasiongee na hao wafanisi au hizo bank na kukamilisha upanuzi wote badala ya vipande vipande!!
 
Tatizo akili hiyo hawana hawa jamaa ukiwambia watasema budget hakuna!!
 
mi nilisikia wanataka kuanzisha usafiri wa pantoni toka bagamoyo hadi Dar es salaam na pesa wanayo sasa sijui kianze kipi
 
Kwasasa barabara ya Mwenge-Tegeta inapanuliwa ingekuwa nafasi nzuri ya serikali kutafuta pesa au wahisani wa kupanua barabara ya Tegeta-Bagamoyo kwani itapunguza gharama. Sasa ni wakati wa ujenzi na ndiyo muda mzuri wa kupanua barabara badala ya kungojea kipande kimoja kiishe halafu baada ya mwaka moja tunafunga barabara tena kupanua kipande kingine. Imefika wakati wa Tanzania wa kufikiria mbali badala ya kufikiria kutatua matataizo kwa kupuliza kila siku!! kila mtu anajua barabara inatakiwa kupanuliwa mpaka Bagamoyo sasa ni kwanini wasiongee na hao wafanisi au hizo bank na kukamilisha upanuzi wote badala ya vipande vipande!!

Yaani watazania tumezoea kulalamika sana,barabara zisipopanuliwa tunalalamika upanuzi ukianza tunalalamika ni lini sasa tutakaa hata tuonyeshe appreciation,kumbuka kuna sehemu Tanzania hakuna hata barabara.
 
Hapa hakuna malalamiko anachosema mwana JF ni ukweli usiofichika kwani ukijenga kwa vipande vipande kama ilivyo sasa gharama yake ni kubwa sana.
 
Tumeona wenzetu huku wanavyofanya kwasababu watu kwa sasa hawatumii hiyo barabara wakati ujenzi unaendelea ni rahisi zaidi kumalizia badala ya kufanya kwa vipande vipande
 
Back
Top Bottom