Serikali Tanzania imekosa viongozi wenye kauli za kuitawala mfano wa Mrema na Lowassa

chachu

Senior Member
May 17, 2011
141
16
Sakata hili la mafuta limenitia shaka kwa utendaji wa serikali hasa kwa waziri mwenya mwenye dhamana.

Tuna mifano hai ya mawaziri wawili wa zamani akiwapo Augustine Mrema na E. Lowassa katika utendaji wao. Mrema kutoa siku kwa majambazi kurudisha silaha na kufanya hivyo, Lowassa kwenye wizara ardhi na kwingineko, leo hii sakata la mafuta waziri muhusika hadi awe boosted na bunge na pamoja majibu hayo hayaonyeshi quick solution wakati watanzania wanateseka kwa huduma hiyo na wala hawapewi bure ni fedha zao.

Je, ni kweli serikali ni kweli serikali ina kigugumizi au inaogopa wafanyabiashara? Kwa serikali ya CCM, ingekuwa ni uchaguzi leo ningempatia Lowassa ndiye mwenye uthubutu.

Wana JF, nawakilisha
 
hapo umenena angekuwa mrema ni waziri angeshatoa amri na wafanya biashar. wote wangetii amri. kusingekua na ujinga huu. uongozi ni kipaji sio elimu tu. hawa mawaziri wa sasa vipaji hawana...
 
Kwanini umetumia mfano wa viongozi ambao Wamefeli? Lowassa kajiuzulu kwa sababu ya ufisadi. Na Mrema hana muelekeo kwa sababu ya kupayuka ovyo ovyo bila ya ushahidi.
 
Sakata hili la mafuta limenitia shaka kwa utendaji wa serikali hasa kwa waziri mwenya mwenye dhamana.

Tuna mifano hai ya mawaziri wawili wa zamani akiwapo Augustine Mrema na E. Lowassa katika utendaji wao. Mrema kutoa siku kwa majambazi kurudisha silaha na kufanya hivyo, Lowassa kwenye wizara ardhi na kwingineko, leo hii sakata la mafuta waziri muhusika hadi awe boosted na bunge na pamoja majibu hayo hayaonyeshi quick solution wakati watanzania wanateseka kwa huduma hiyo na wala hawapewi bure ni fedha zao.

Je, ni kweli serikali ni kweli serikali ina kigugumizi au inaogopa wafanyabiashara? Kwa serikali ya CCM, ingekuwa ni uchaguzi leo ningempatia Lowassa ndiye mwenye uthubutu.

Wana JF, nawakilisha

Ilikuwa nafasi ya Salim A. Salim lakini huyu mkwe-re akaleta ngonjera na kuwanunua Magamba na kumfitini SAS. Sasa angalia madudu yake.
 
<br />
<br />
Nakubaliana na wewe kabisa, ilitakiwa iende kwa huyo SAS hii nchi isingefika hapa ilipo!
 
Back
Top Bottom