Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,857
- 30,205
Tatizo ni waislam wenyewe..mimi ni mkristo na nimesoma na waislam wengi tu na wamefaulu vizuri na wapo BOT,TRA wengine wanafanya UN Agencies,sijaona waislamu wakikandamizwa tatizo lililopo ni wazazi hawapendi kupeleka mtoto shule,ni rahisi kupima mtoto wa kiislam atachapwa kwa kutokwenda madrasa na sio shule!!!!hili lipo wazi!!!mfumo wa wazazi wa kiislamu si mzuri kwa kweli wanahitaji kubadilika...hawana mpango na shule...Nimebahatika kukulia katika mazingira ya waislamu wengi katika jamii na nimeona watyoto wengi wenzangu wakiacha shule kwa sababu mbalimbali,madawa ya kulevya,umalaya,mimba za mapema,ulevi wa wazazi na kutojali shule.Jiulize lifuatalo..Chukua mfano familia mbili zenye maisha magumu na dini tofauti..Utaona familia ya kikristo inapambana ili mtoto/watoto wao wasome lakini wenzetu hawana hata habari na shule Je Utaulaumu mfumo au Ujinga wa Baadhi ya watu?Sheikh Ponda na mwenzie waulize watoto wao wamewapeleka shule?Pata jibu kisha rudi kwa thread hii.
Yapo majibu humu humu ndani.
Soma na tuwasiliane Insha Allah.