Nchi yetu si maskini Mkuu bali tuna "Viongozi" (huwa nasikia vibaya sana kuwaita Viongozi) ambao ni mafisadi ambao wanahamishia utajiri wote wa nchi yetu mifukoni mwao. Wale wote wanaojiita ni Viongozi na ambao wamewahi kushika nafasi za juu kabisa za uongozi ndani ya nchi yetu hawakuwa mabilionea miaka michache tu iliyopita lakini leo hii baada ya ufisadi mkubwa waliofanya kuhusu Rada, Richmond/Dowans, Ndege ya Rais, Helicopters na magari ya jeshi, Kiwira Coal Mining, NBC, Mikataba ya madini, EPA, Meremeta, Kagoda n.k. wengi wao ni matajiri wakubwa sana na wana assets nyingi sana ndani na nje ya nchi. Unaona hata Wabunge wanachukua chao mapema inabidi kila Wizara katika kipindi cha bajeti itenge "bulungutu" la karibu shilingi bilioni moja ili kuhakikisha tu bajeti zao zinapitishwa na "waheshimiwa" Wabunge.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.