SERIKALI na VITA YA KWELI NA MAFISADI AU SANAA ZA KAWAIDA??

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
Serikali yatangaza kiama kwa mafisadi Send to a friend Monday, 28 March 2011 21:35 0diggsdigg

Ramadhan Semtawa
KATIKA kile kinachooonekana ni kusikia kelele za umma, serikali inatarajia kupeleka muswada bungeni wa mabadiliko ya sheria mbalimbali, licha ya mambo mengine kosa la rushwa litakuwa ni uhujumu uchumi.
Siku za karibuni nchi imejikuta ikitiswa na vitendo vya rushwa kubwa, ikiwamo mikataba ya kampuni za Richmond na Dowans, huku wananchi wakitaka hatua zaidi kubana watuhumiwa.

Hata hivyo, katika hatua inayoonyesha serikali kusikia matakwa hayo ya umma jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, aliwasilisha muswada huo wa mabadiliko ya sheria mbalimbali 14, mbele ya Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala.

Katika mapendekezo hayo yaliwasilishwa mbele ya kamati hiyo na wadau kwa ajili ya kupata maoni, Werema alisema wameamua kufanya hivyo baada ya kung’amua rushwa ni tatizo.Werema alifafanua kwamba, mabadiliko hayo yamo kwenye sehemu ya saba katika Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi sura ya 200.

Alisema mapendekezo hayo ya marekebisho yanatoa pia mamlaka kwa mahakama za hakimu mkazi kupokea kesi za uhujumu uchumi.

Aliongeza kuwa kama muswada huo utakubalika, mahakama hizo sasa zitakuwa na mamlaka ya kupokea na kusikiliza kesi hizo, tofauti na sasa ambako husikilizwa na mahakama kuu pekee.

"Sehemu ya saba ya marekebisho katika Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi, sura ya 200. Sehemu hii inapendekeza marekebisho katika kifungu cha 29 ili kuzipa mahakama za hakimu mkazi kuwa na uwezo wa kupokea na kusikiliza kesi za uhujumu uchumi,” alisisitiza Werema na kuongeza:
"Makosa ya rushwa sasa yanafanywa kuwa ni miongoni mwa makosa ya uhujumu uchumi."
Katika hatua nyingine, muswada huo pia unatarajia kuongeza adhabu kwa watu wanaokutwa na makosa ya uchawi, ikiwamo kutozwa faini ya Sh1 milioni na kifungo jela.

Pia, Werema alisema sehemu ya muswada huo, umeweka kipengele cha marekebisho kwenye kifungu cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, sura ya 16, yanayolenga kutoa adhabu mahsusi kwa mtu mwenye umri wa miaka chini ya 18 anayetuhumiwa kubaka.

Muswada huo wa serikali ambao umegusa sekta mbalimbali, umeweka bayana kwamba kifungu cha 192, kinapendekeza marekebisho ili kuipa mahakama kuu uwezo wa kusikiliza awali, mashauri ya jinai pale ambako mshtakiwa atakuwa amekana shtaka dhidi yake kama ilivyo kwa mahakama ya wilaya.

Akichangia maoni yake, Mbunge wa Singida Kusini, Tundu Lisu, alionyesha wasiwasi kama kuna umuhimu kwa sasa kuweka sheria ya uchawi wakati ilitajwa kwenye Tume ya Jaji Nyalali miaka 20 iliyopita kama sheria mbaya.

Tundu ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alionyesha shaka pia kipengele cha sheria ya uchawi, akisema kitakuwa na madhara makubwa, kwani kitamnyima haki mtuhumiwa ya kujieleza na kujikuta akitupwa jela na kulipa faini.
 
Ndo wanakumbuka leo eeh?
Maji ya shingo hayuo...na wenye akili zetu tushajua kuwa SERA ZA CDM zinafanyiwa kazi kwa gharama yoyote!~
 
Ni usanii mwingine, ndivyo kamati ya fitna ilivyomshauri JK ili angalau imani irudi kwa wananchi ambao walianza kuamini serikali ipo usingizini haina macho. Sheria hizo sidhani kama zitakuwa na tija kubwa.
 
Back
Top Bottom