"Serikali na Vikao Vya Usiku wa Manane!. Sii Bure!, Lazima Kuna Jambo"!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Niko hapa mjini Dodoma kwa ya kwangu, haya na yale. Saa hizi ni saa saba za usiku!, kwa maana nyingine ni usiku wa manane, nimepita hapa ukumbi wa Ustawishaji Makao Makuu, Kuna Kikao muhimu cha serikali mpaka saa hizi!.

Kuanzia Mukulu, Vice na PM wote wapo na hapa nje kumesheheni yale magari yenye plate number zinazoanzia W.... na hizi nyingine zinazoanzia NW na zile Prado mpya za mapiesi!.

Kwa vile huu ni usiku mkubwa, kiafrika watu wanaofanya shughuli usiku hivi huitwa wanga!, ili kuhalalisha serikali yetu haifanyi vikao vya kuwanga usiku hivi, hii inamaanisha kuwa vikao hivi sii bure, lazima kuna jambo kubwa la dharura!.
 
je wakuu wa bakabaka wamo nao? Pengine wana-discuss ku-give up ziwa nyasa kufuatia mkwar wa malawi! Ingekuwa enzi za mwalimu ultimatum ingeshatangazwa....'adui katuvamia, nia tunayo, dhumuni tunalo....'
 
me nahisi maadhimisho ya 88
 
Labda utuambie Pasco, kikao kilianza usiku huo wa manane au kilianza mapema but mpaka mida hiyo kilikuwa bado hakijaisha!!!
 
je wakuu wa bakabaka wamo nao? Pengine wana-discuss ku-give up ziwa nyasa kufuatia mkwar wa malawi! Ingekuwa enzi za mwalimu ultimatum ingeshatangazwa....'adui katuvamia, nia tunayo, dhumuni tunalo....'

Vita ni pesa na sirikali ya jeikei hela yote wamekula wanaogopa kutangaza maana tunaweza chapwa wakaja kuchukua hadi ikulu.
 
Kaka hapo kwenye uwepo wa mkulu umetuongopea kwakua mkulu hayupo nchini hebu pitia upembuzi wako kwa kina, na kuhusu kuwepo kwa vikao vya usiku ni kwa ajili ya uwepo wa Bunge na huu mfungo wa ramadhani kwahiyo kama kuna vikao vya kiserikali hawana namna ya kuanza vikao mapema lazima waanze late hivyo kwa kufika muda huo na maadam havifanyiki uchi na ni halali waacheni wavifanye
 
Pinokyo Jujuman, unatisha sana.

Umeweka sababu ambazo kwa harakaharaka zina mashiko, lakini kama ni jambo la dharura la kiserikali, hujui kuwa Executive ni Mhimili unaojitegemea na hausubiri wajumbe wamalize kwanza Bunge ndipo wakutane! Chezeya sirikali wewe!

Hapo lazima AIBU YA CHENGE kuwa MKiti wa kamati ya Bunge na chenchi ya rada vinajadiliwa.
 
Last edited by a moderator:
Kaka hapo kwenye uwepo wa mkulu umetuongopea kwakua mkulu hayupo nchini hebu pitia upembuzi wako kwa kina, na kuhusu kuwepo kwa vikao vya usiku ni kwa ajili ya uwepo wa Bunge na huu mfungo wa ramadhani kwahiyo kama kuna vikao vya kiserikali hawana namna ya kuanza vikao mapema lazima waanze late hivyo kwa kufika muda huo na maadam havifanyiki uchi na ni halali waacheni wavifanye

Acha ubishi wewe mkulu yupo dom na anasepa leo
 
Labda kuna dili ya madini ilikua inajadiliwa na kila mtu anataka kujua cha kwake ni kiasi gani
 
Nchi inaelekea sivo na CDM wanachukua popularity mno. Kwani wao wajinga, si umeona walivokimbia kupeleka hoja ya fao la kujitoa mapema. Inanikumbusha tulivokuwa watoto na ukiwa mmbeya unavowahi kusema kwa mama.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom