Serikali na neno Mbunge MMOJA wa Chama Kimoja!!!

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
6,146
7,000
Nimemshangiaa N/ waziri wa mambo ya ndani Kagasheki kusema eti serikali inamjua mbunge MMOJA wa chama kimoja alietoka kwenye jimbo lake na kwenda kuchochea fujo Tarime.

Hii ni kauli ya kichovu na uoga ya serikali kama mbunge wa chama hicho aliepo Tarime ni Lema ambae pia ni waziri wa mambo ya ndani (Kivuli). Sasa sijui ni sheria gani imevunjwa kwa Mh Lema kwenda Tarime ama ni kosa kukuta watanzania wenzako wemeuwawa ukawapa pole.

Kagasheki si uje Tarime hapa ujue shida ya watu wa Tarime?

Lema amekuja kutupa pole ni haki kabisa sasa sijui unataka nini wakati mnaua watu wetu jiheshimu wewe Kagasheki ujue kama sio sisi wana TARIME wewe ungekua mganda mana Amin alishachukua Bukoba yote, sisi tulipigana kuwaokoa nyie.

Mnaua watu kila mara hapa Tarime tangu hata Lema hajawa Mbunge ama ndie yeye alikua anawapa risasi? Acheni uzushi na udaku na TBC LENU hilo.
 
Hizo ni dalili za kutokuwa na leadership vision. kila kitu wewe unamtafuta mchawi mpaka hapo hapo ccm wanapumlia machine icu na wasiongaliwa vizuri kuna watakaoishia Mire...mbe.
 
inachekesha kweli sasa hivi wameambizana wasitaje chadema labda wanadhani wanawapandisha chati,wakati nguvu ya umma imewapa ujiko ,hata jana kulikuwa na naibu meya wa manispaa ya kinondoni alikuwa anasema chama kimoja ha ha ha serikali inaogopa chama cha siasa
 
kweli sasa nimeamini,JK Hana wazir mzuri hata mmoja, yaani huyu waziri baada ya kufanya kazi hata kwa kwenda mara kuangalia hali halisi,yeye anakaa na kulalamika, mbunge mmoja mbunge mmoja chama kimoja cha kimoja, KAGASHEKI ACHA KULALAMIKA CHUKUA HATUA.
 
kweli sasa nimeamini,JK Hana wazir mzuri hata mmoja, yaani huyu waziri baada ya kufanya kazi hata kwa kwenda mara kuangalia hali halisi,yeye anakaa na kulalamika, mbunge mmoja mbunge mmoja chama kimoja cha kimoja, KAGASHEKI ACHA KULALAMIKA CHUKUA HATUA.

Ndugu yangu aende Mara!!!!!!!! huko si WatamNYAMBARI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:israel:
 
Mwoga sana huyu Hamisi alivyokuwa anasema kwa kujiamini hadi misuli ya uso inamtoka nikajua atakitaja hicho chama chenyewe. Sasa yeye kama waziri mwenye dhamana ya ulinzi anaogopa kukitaja hicho chama anataka nani akitaje?
 
Mnyika bwn! Mnyika kiboko! Tangu atake kumburuza sofia simba basi wameanza kusema mbunge mmoja ta chama kimoja. Cdm nzima ikienda Tarimu sijui wataweka kwenye wingi? Wabunge wengi wa chama kimoja, ...wauh kagasheki unawahaibisha wahaya! Au jina lako linakusaliti?
 
Hivi serikali haijui kuwa Mh. Lema ni waziri kivuli wa Mambo ya Ndani? Nilitegemea wenyedhamana serikalini wangeshafika eneo la tukio kuliko kuongoza kwa remote control. Pia haya matatizo yote ya Nyamongo kama yanavyofahamika ni Mh. Lema aliyasababisha huko. Binafsi nilishawahi kufika na nilijionea baadhi ya mito ikiwa na maji yenye rangi nyekundu iliyosababishwa na shughuli za uchimbaji. Hawa watu hawajawahi kuwa compersated, na ni Mh. Lema ndiye hakutekeleza hilo, na ndiyo waliouvumbua huo mgodi na wengine ilikuwa ndiyo shughuli yao ya kujiendeshea maisha kama wachimbaji wadogowadogo wasio rasmi, ila Mh. Lema ndiye alikwenda kuwafukuza na kuwamilikisha wawekezaji (Barick Gold Mines).

Watu wanaugua maradhi ya ajabu kutokana na kutumia maji yenye sumu na mifugo yao imekuwa katika afya mbaya na mingi kufa kutokana na maji yenye taka za sumu toka migodini na wamekuwa wakiipigia serikali kelele na baadaye ikaundwa tume na hatujasikia kilichoamuliwa, ila ni Mh. Lema ndiye aliyesababisha hawa watu wasipewe haki yao inayostahili. Tunaomba serikali iwe inatekeleza wajibu, badala ya kutafuta visingizio visivyo na ukweli. Kauli kama za Mh. Balozi Kagasheki zinazidi kutuondolea imani na serikali yetu. Kama hili dogo hawana uwezo, je hayo mengi makubwa si wanaingizana chaka tu kama walivyomuingiza mtoto waMkulima Hon. P.M. Pinda.
 
Back
Top Bottom