Serikali na Mzimu wa makaburu ya mabaniani

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,081
5,061
Hapo zamani za kale palikuwa na kipindi katika RTD kikiitwa mazungumzo baada ya habari.Mojawapo ya simulizi zake ilikuwa kuhusu mzimu katika makaburi ya mabaniani.Iliaminika kuwa palikuwa na mzimu ambao uliua watu.Hii ilifanya watu wasitafakari sababu za kifo bali kukimbilia kuhusisha chanzo cha kifo kwa maiti yoyote iliyookotwa katika eneo hilo kuwa kimetokana na mzimu huo.
Jana zimetokea vurugu Mwanza na tayari wakubwa wanzihusisha na Chama cha siasa.Hawataki kufikiri hata kidogo;hebu tujiulize,
  • Nani anayeruhusu uvunjaji wa sheria kama sio serikali?
  • Nani ameruhusa watu wapange biashara popote mpaka barabara hazipitiki?
  • Nani kafungua mashina ya wakereketwa mpaka kwenye hifadhi za barabara?
Tumelea uvunjaji wa sheria mpaka watu wamezoea na kuona ni haki yao.Tusilaumu chama cha siasa ila tuilaumu serikali iliyoshindwa kusimamia sheria kwa muda mrefu na sasa kila jambo majibu yake ni "chama kimoja cha siasa"
 
Vijana ni bomu linalosubii kulipuka; na litalipuka soon kwani hakuna mkakati maalum wa kuwaendeleza vijana. Kila wanapojaribu kujitafutia kipato wanajikuta wanabamizwa na kupoteza mali zao. Hali hii haitaendelea millele!
Soon watajitokeza pia wakulima kwani kwa mkakati wa serikali, mapande makubwa ya ardhi yenye rutuba yatagawiwa kwa makampuni ya nje kwa mikataba ya miaka 99 na kutolipa kodi kwa miaka 10!
 
Back
Top Bottom